Kama kawaida,mbunge wa jimbo la bukoba mjini balozi Khamis Kagasheki baada ya kukutana na waumini Kikirsto na kutoa misaada mbalimbali sasa ametoa swadaka ya mazulia (miswala) ,vitabu na mavazi katika misikiti iliyoko jimboni bukoba na kwenye baadhi ya madarasa ikiwa ni maandalizi ya ya waislam kujiandaa na ibada ya mwezi mtukufu wa ramadhani.
Hii ni jadi ya Mbunge huyu na amekuwa akifanya hivyo bila kujali imani ya watu wawe wakristo,waislam,wapagani na wasio na dini katika jimbo na ameshiriki katika shughuli zao za kijamii.
Kwa wakazi wa Bukoba,Kagasheki ni Zaidi ya Mbunge.
Picha zinafuata!
Wachina wana msemo "mtoto wa jirani mpe samaki, mtoto wako mpe ndoano."
Kagasheki ni mbunge anayependwa sana na wakazi wa Bukoba bila kujali dini zao lakini sipendi utaratibu wa kutoa misaada,inabidi wananachi wajengewe utaratibu wa kujitafutia
Na hapo ndipo lilipo gonjwa letu watz.
Hilo ndilo tatizo la Kagasheki.Matatizo ya wananchi hayawezi kuondolewa kwa kumwaga fedha za kununua ubwabwa wa siku moja,bali kuweka mikakati itakayowawezesha kujitegemea.Hata hivyo amejitahidi ukilinganisha na watangulizi wake.
Ukiwa nacho, wasaidie wasio nacho.
Ameshindwa kusimamia ujenzi wa stand ya kisasa ikaisha yeye yuko busy na waumini ..mbona soko nalo limemuwia kitendawili
Badala ya kufanya harambee kubwa ya kukusanya fedha kwa ajili ya kujenga hospital ya kisasa kubwa zaidi ya bungando,kcmc itakayopata ruzuku,msamaha wa kodi toka serikalini,yeye anagawa nguo.
Ukiwa nacho, wasaidie wasio nacho.