Kagasheki atoa miswala,vitabu na mavazi ya sh mil 25 misikitini Bukoba!

DJ Baraka

Senior Member
May 15, 2013
177
82
Kama kawaida,mbunge wa jimbo la bukoba mjini balozi Khamis Kagasheki baada ya kukutana na waumini Kikirsto na kutoa misaada mbalimbali sasa ametoa swadaka ya mazulia (miswala) ,vitabu na mavazi katika misikiti iliyoko jimboni bukoba na kwenye baadhi ya madarasa ikiwa ni maandalizi ya ya waislam kujiandaa na ibada ya mwezi mtukufu wa ramadhani.

Hii ni jadi ya Mbunge huyu na amekuwa akifanya hivyo bila kujali imani ya watu wawe wakristo,waislam,wapagani na wasio na dini katika jimbo na ameshiriki katika shughuli zao za kijamii.

Kwa wakazi wa Bukoba,Kagasheki ni Zaidi ya Mbunge.

DSC04848.JPG

DSC04869.JPG

DSC04018.JPG

DSC04139.JPG

DSC04154.JPG
 
Ni yule baraka wa Radio Kasibante! Kila la kheri wewe na mbunge
 
Kama kawaida,mbunge wa jimbo la bukoba mjini balozi Khamis Kagasheki baada ya kukutana na waumini Kikirsto na kutoa misaada mbalimbali sasa ametoa swadaka ya mazulia (miswala) ,vitabu na mavazi katika misikiti iliyoko jimboni bukoba na kwenye baadhi ya madarasa ikiwa ni maandalizi ya ya waislam kujiandaa na ibada ya mwezi mtukufu wa ramadhani.

Hii ni jadi ya Mbunge huyu na amekuwa akifanya hivyo bila kujali imani ya watu wawe wakristo,waislam,wapagani na wasio na dini katika jimbo na ameshiriki katika shughuli zao za kijamii.

Kwa wakazi wa Bukoba,Kagasheki ni Zaidi ya Mbunge.

Picha zinafuata!

Wachina wana msemo "mtoto wa jirani mpe samaki, mtoto wako mpe ndoano."
 
Pamoja na mambo ya siasa lakini Kagasheki ni mmoja wa wabunge wachache wanaokubalika jmajimboni mwao.

Safi sana mh.mbunge
 
Hilo ndilo tatizo la Kagasheki.Matatizo ya wananchi hayawezi kuondolewa kwa kumwaga fedha za kununua ubwabwa wa siku moja,bali kuweka mikakati itakayowawezesha kujitegemea.Hata hivyo amejitahidi ukilinganisha na watangulizi wake.
 
Nani anaishi bila msaada? bajeti ya nchi yako inategea misaada kwa 75% sasa kuna ubaya gani mh kusaidia jamii,watu wamepatwa na mafuriko nk,unafikiri msaada wa mbunge wa haraka ni nini? huyu mbunge ni zaidi ya wabunge bongo! kuabli msikubali
 
Badala ya kufanya harambee kubwa ya kukusanya fedha kwa ajili ya kujenga hospital ya kisasa kubwa zaidi ya bungando,kcmc itakayopata ruzuku,msamaha wa kodi toka serikalini,yeye anagawa nguo
 
Badala ya kufanya harambee kubwa ya kukusanya fedha kwa ajili ya kujenga hospital ya kisasa kubwa zaidi ya bungando,kcmc itakayopata ruzuku,msamaha wa kodi toka serikalini,yeye anagawa nguo.
 
Ameshindwa kusimamia ujenzi wa stand ya kisasa ikaisha yeye yuko busy na waumini ..mbona soko nalo limemuwia kitendawili
 
Uliza watu wa Bukoba wakueleze mchakato wa soko ulivyo mkuu,kama hujui jambo we uliza tu siyo kulaumu tu!
mipango ya ujenzi wa soko unajua inaanzia kwa nani?
 
Badala ya kufanya harambee kubwa ya kukusanya fedha kwa ajili ya kujenga hospital ya kisasa kubwa zaidi ya bungando,kcmc itakayopata ruzuku,msamaha wa kodi toka serikalini,yeye anagawa nguo.

Keep watching................ kamanda!
 
Wameshaanza kuhongwa wazee wa ubwabwa, ili wamchague 2015
 
Ukiwa nacho, wasaidie wasio nacho.

Miaka ya nyuma rushwa ya uchaguzi ilikuwa ikitolewa kwenye makundi ya kijamii yasiyo ya kiimani mf. vikundi vya wanawake, mahospitalini n.k kama misaada. Ukweli mchungu ni kuwa uchaguzi ujao support ya makundi ya kidini itakuwa ni uwanja mpya wa mapambano.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom