Mzee wa Rula
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 8,169
- 3,361
Jibu ni rahisi tu ukiangalia sifa za kugombea ubunge, moja wapo ni kuwa mwanachama wa chama cha siasa kilichokupendekeza kugombea nafasi hiyo. Kwa kuvuliwa uanachama, Kafulila anakosa sifa ya kuwa Mbunge. Hapa ndipo 2naona umuhimu wa mgombea binafsi, pia umuhimu wa kufuta suala la chaguzi ndogo za Ubunge na udiwani.
Katika kesi kama hii, kundi la watu wasiofikia mia moja, litaipa gharama serikali kufanya uchaguzi mdogo Kigoma Kusini bila kujali hali ngumu ya uchumi tunayokabiliana nayo.
Kama vipi sheria zibadilishwe tu aliyeshika nafasi ya 2 achukue jimbo.
Mbona naona tuko page moja, Kafulila ikithibitika kavuliwa uanachama basi mbona ni simple tu na Ubunge hana!! Simple and clear!!!
Naona maoni ya wengi yanafanana kabisa lakini ukweli ni kuwa kama Kafulil kavuliwa uanachama automatically na ubunge hana. Sababu zieshaelezwa na wengi waliochangia.
Hii itabaki kuwa changamoto kwa siku za usoni.
Kaka hapo kwenye bluu tuhakikishe tunashiriki katika maoni ya katiba mpya ingawa sheria yake ilichakachuliwaJibu ni rahisi tu ukiangalia sifa za kugombea ubunge, moja wapo ni kuwa mwanachama wa chama cha siasa kilichokupendekeza kugombea nafasi hiyo. Kwa kuvuliwa uanachama, Kafulila anakosa sifa ya kuwa Mbunge. Hapa ndipo 2naona umuhimu wa mgombea binafsi, pia umuhimu wa kufuta suala la chaguzi ndogo za Ubunge na udiwani.
Katika kesi kama hii, kundi la watu wasiofikia mia moja, litaipa gharama serikali kufanya uchaguzi mdogo Kigoma Kusini bila kujali hali ngumu ya uchumi tunayokabiliana nayo.
Kama vipi sheria zibadilishwe tu aliyeshika nafasi ya 2 achukue jimbo.
Ni maajabu kwa sababu wananchi waliompeleka bungeni.sio.waliomkataa ni kikundi cha watu.wasiozidi.arobaini.na wala hawatoki.jimboni kwakeHawezi kuendelea kuwa mbunge tena endapo atakuwa amevuliwa uanachama kwa sababu aliogembea kiti cha ubunge kupitia chama hicho.
Sasa we vp? Umekuja hapa kuomba uelekezwe manake hujui sasa unaelezwa ukweli ulivyo hlf unaleta ubishi we mwe.u au? Wewe umeshaambiwa kafulila alikuwa mbunge wa jimbo la kigoma kusini kupitia tiketi ya nccr sasa kafukuzwa na mle bungeni hamna mbunge au waziri mkuu, spika, mwanasheria, mawaziri n.k wote wana vyama vyao sasa kafulila atakuwa mbunge wa chama gani? Katiba iliyopo hairuhusu mgombea binafsi unataka ueleweshwe namna gani? We kweli mb.rula, hatuna muda wa kubishana na wewe hapa kama kafulila ni ndgu yako ujue imekula kwako.
Lkn wanajamvi vp khs zile mil90 alizokopwa kununu gari atazilipaje? Sijui RA naye kama alirudisha.
Kauli kama hizi ndizo zinazotusumbua, kwa nini unashindwa kutaja jambo zito kama hili katika sheria mama. Kwenye hali kama hii tunamalizanaje? Maana kwa ujumla hayo ni mawazo yako tu.