Kafulila: Bei ya mafuta Nairobi ni ghali sana pamoja na Ruto kuwa Rais, Dar bei iko chini. Hongera Rais Samia

Huyo Bwana Kafulila nadhani hajafikiria sawa sawa, hivi unaweza vipi kuwapima MaRais mmoja mwenye miezi 18 madarakani na mwingine akiwa na siku 5?

Tunajua unaongea yote haya Kwa kuwa unalenga Teuzi lakini isiwe Kwa namna hii.

Tukubali kuwa Kiongozi wetu bado hajashughulikia kisawasawa suala la mfumko wa bei. Haiwezekani bei ya Petrol ishoot kutoka shilingi 1858 ya JPM hadi kufikia 3342 wakati wake tena ndani ya Mwaka Mmoja tu wa Uongozi wake 🙆
 
Naona tumbili anapalilia uteuzi akitarajia kupata zali kama la chalamila, yaani analinganisha bei za bidhaa kwenye nchi mbili tofauti zenye viwango tofauti vya kiuchumi na vipato vya watu. Halafu anafanya conversion ya currency kufanya ulinganifu huo. Kwa utaratibu huo bado anaweza kutuaminisha petroli ni bei ghali sana Marekani hivyo wamarekani maisha yao ni magumu sana kuliko wadanganyika kwani mama amefanya petroli imekuwa bei chee. Pathetic!!​
 
Tanzania mafuta yameshuka sana, lazima tukubali Rais Samia na January Makamba ni watu makini Sana.

CHADEMA MMEJIFICHA WAPI AU HAMNA MAGARI?

Hivi wewe unaweza pongezwa kwa wajibu wako?

Jukumu lao hilo hawapaswi kupongezwa wajichanganye wapandishe bei ndo watatoa maelezo ya kuridhisha
 
Kwani Ruto alisema ana visima vya mafuta nyumbani kwake? Mwambieni Kafulila ndiyo imetoka hiyo. Ajiandae kumwangukia Mbowe tu, asitegemee kurudi....mkumbo ameshaanza taratibu na katiba kumtajataja samia haitamsaidia. ccm ina wenyewe
Upo mbali kabisa na mada, umeruhusu povu litawale akili yako kitu ambacho hakimfai kabisa mtu makini anayetumia jukwaa hili katika kujenga hoja na kuhabarisha na kuwa tayari kuhabarishwa na wengine.
 
Tanzania mafuta yameshuka sana, lazima tukubali Rais Samia na January Makamba ni watu makini Sana.

CHADEMA MMEJIFICHA WAPI AU HAMNA MAGARI?
Hatushindani na kenya hapa bali tunaangalia maisha yetu, bei ya mafuta imeshuka nauli hazijashuka sasa imenisaidia nini mimi ninaetumia public transport?
 
Tanzania mafuta yameshuka sana, lazima tukubali Rais Samia na January Makamba ni watu makini Sana.

CHADEMA MMEJIFICHA WAPI AU HAMNA MAGARI?
Ngoja wanyooshwe kwanza hao kenge na huyo Hustler ..

Na siku Machadomo yakishika Nchi in case itakuja kutokea itawanyoosha maskini wa Sasa na wengine hadi akili ziwakae sawa maana yanaaminishwa ujinga na yanakubali..

Utasikia utitiri wa Kodi,sijui tozo na blaaa blaa zingine as if Chadomo hawatakusanya Kodi 😆😆
Usifananishe bei ya mafuta tu baina ya Tanzania na kenya vile vile fananisha na kima cha mshahara, kenya mshahara yao ni ya juu kuliko kwetu na uchumi wa kenya uko juu kuliko wetu mkitowa habari kama hizi mfanye utfiti kwanza hata ukichukuwa bei ya mkate kwa shilingi ya Tanzania utakuta iko juu kenya kuliko tanzania.
 
Wewe usiwe tumbili,Cost of living ya Kenya iko juu Sana kuanzia makazi hadi vyakula hakuna wali wa buku jero wala chumba Cha 20,000 kule.
 
Back
Top Bottom