Makonda atimiza ahadi ya kumfuta machozi mwalimu aliyetapeliwa gari

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,771
15,252
Unaweza kusema ziara ya Paul Makonda mkoani Kagera imemlipa mwalimu Adela baada ya kupewa gari mpya na Makonda baada ya kumlilia kutokana na shida yake ya kutapeliwa gari lake la kwanza mara tu alipolichukulia mkopo.

Mwl Adela amelia machozi na kumshukuru Rais Samia kwa kumteua mtetezi wa wanyonge Paul Makonda aka Bashite.


View: https://youtu.be/aQZFYNFAIgM?si=_QADiZ-xinlkUCbk
 
Sheria zingefuatwa kama zilivyoandikwa sidhani kama huu usanii ungekuwepo
Kama sheria zinafuatwa huyo mwalimu angepata haki yake
Mambo mengi ya kishenzi yanafanyika nchi hii kwa sababu viongozi wanalegeza sana na wao wamo kwenye kupindisha sheria kila sekta na kila wizara na kila sehemu ya maisha yetu

Hakuna haja ya kutatua mmoja mmoja maana wote wanaonewa kwa namna moja ama nyingine
Dr anapokea rushwa ili amhudumie mwenye hela
Nesi anamtukana mama mjamzito huku polisi anamlamba vibao mwizi bila ushahidi mahakamani
Hakimu analamba chake, mjeda anamkata mabuti kijana kisa kavaa t-shirt ya mjeda wa America alionunua mtumbani
Wengine wanakusweka ndani masaa 24 kisa umemchukulia hawara yake
Sheria hazifuatwi hapo inatakiwa kero zote zinapitiwa upya na hukumu yake iwekwe bayana na asiezifuata yeye ndio awajibike kwa kuwekwa hadharani

Kama ni mwizi wa mamilioni ahukumiwe tuone kala mvua ngapi
Acheni usanii
 
GSM wamerudishiwa nyumba iliyoporwa na Makonda?


Yule jamaa aliyeporwa benzi na Makonda karudishiwa? Makonda aache janja janja.

Waandishi bado mna maswali mengi sana ya kuwauliza mama zenu (Makonda)
Mpeleke mahakamani, kama huwezi kaa kimya
 
Kwanza alaumiwe mwalimu anayetakiwa kuwafundisha watoto ila anakuwa kama mtoto
Utoto wake ni nini?

Swala la kutapeliwa hata wewe unatakiwa tu

Inatapeliwa nchi ishindikane mtu ?

Kama kesi kukwama polisi au mahakamani ni kawaida tu kwa mazingira ya nchi yetu kwa kuwa rushwa imejaa
 
Back
Top Bottom