Kafanya kosa kuoa house girl? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kafanya kosa kuoa house girl?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by HorsePower, Dec 5, 2011.

 1. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Juzi nilikwenda mapumziko Tanga baada ya kuchoshwa na shughuli zangu za kikazi za wikii nzima na foleni za hapa Bongo zisizo na tija! Nikiwa TA nilipata wasaa wa kumtembelea kwa mara nyingine rafiki yangu mpendwa ambaye mwaka juzi alifiwa na mkewe.

  Kabla ya kufariki kwa mkewe, kaka huyu alikuwa akiishi na mdada wa kazi ambaye ki umri hakupishana kabisa na mkewe. Dada huyu ambaye nilifanikiwa kumuona mara kadhaa kila nimtembeleapo rafiki yangu ni mpole mtaratibu na mwenye tabia njema.

  Katika mazungumzo yake, mkuu alinidokeza kuwa ameamua kufunga ndoa na msichana huyu kwa sababu amemsaidia sana tangu mkewe alipofarikia na hata watoto wawili walioachwa na marehemu, amekuwa akiwatunza na kuwahudumia kana kwamba ni watoto wa kuzaa mwenyewe.

  Nilipomuuliza kama alikuwa na mahusiano hapo kabla ya mkewe kufariki, alikana kabisa kuwa hakuwahi kufanya hako kamchezo ila kwa sasa focus yake ni nani hasa anafaa kuwatunza watoto wake. Ndugu zake wamekuja juu kupinga uamuzi wake na sasa ameamu kuomba ushauri kutoka kwangu.

  Wadau naomba ushauri nimshauri nini kaka huyu.

  Wenu,

  HP
   
 2. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2011
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Hivi huku duniani bado kuna watu na ndugu wanaochagulia wenzao wenzi? Waache hizo hao, wanataka ku-ruin tu future ya watoto wa ndugu yao, na ndugu yao wenyewe kisha waje kumcheka miaka michache tu ijayo. Mwambie atie akili, haolei ukoo anaoa kwa sababu zake mwenyewe anazozijua yeye.
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  sasa amuoe nani?
  Na mara nyingi hausi gelo kama ni mzuri na anajituma, mama mwenye nyumba akiondoka akina baba wala huwa hawaumizi kichwa.
  Wanahalalisha kiulaini.
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  afuate moyo unataka. Haolei ndugu,anaoa yeye na yeye ndo ataishi na mkewe c ndugu
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Huyo nae, kwanza kabisa kama anajali sana ya watu wengine awaambie wamchagulie.

  Pili , anamuoa dada wa watu kisa kamlelea watoto tu basi? Nauliza maana sijaona sehwmu inayosema "anampenda".Kama hampendi badala ya kumuingiza dada wa watu kwenye ndoa isiyo na mapenzi bora aendelee kumlipa tu dada mpaka dada atakapobahatika kupata mtu anaeeleweka. Hivyo kama hana mapenzi nae sishauri, atakua hamtendei haki dada wa watu.Ila kama anampenda aangalie kwanini hao ndugu wanamnyima.Kama kisa ni vile anewahi kuwa dada wa kazi awapotezee hao ndugu na kumuoa huyo dada ikiwa nae anaridhia.
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Lizy,

  Hata kama haijasemwa, ila nimeelewa kuwa anapenda house girl wake wa zamani kwa sababu anawapenda watoto wake na kuwalea vizuri. Na kwa mjane, hilo ni jambo kubwa sana.

  Is that not a strong reason to justify his love for the maid???

  Babu DC!!
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  HP,

  Huyo jamaa ndiye anayejua anachokitaka...Kama H/girl wake anacho, kwa nini asakamwe??

  Mwambie asimame imara na kufanya maamuzi magumu kwa maslahi na mstakabali wake mwenyewe...Akiwachekea nyani atakiona cha moto!!!


  Babu DC
   
 8. h

  hayaka JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ilimradi hilo ndo analolitaka yeye, afumbie macho maneno ya ndugu na asonge mbele na maisha yake.
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Dec 5, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  Helo Babu DC,

  Mie dada mkubwa salimia wewe.
  Naomba lift.
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Dec 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Babu DC bado sijashawishika kwamba anampenda bali anam-appreciate na anatafuta namna ya kumfunga huyo dada kamba ili aendelee kuwepo.Na hata kama anampenda kwa sababu hiyo tu, bado sioni kama inatosha kumtia dada wa watu pingu alafu baadae aanze kumwambia "mtu mwenyewe nilikuoa tu ili uendelee kunilelea watoto". . . . sio haki kwa mdada.
   
 11. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  kama anampenda na ameridhika nae,maneno ya nini?h/gal ni wasichana kama wengine na wanapenda pia!!aoe tu kama kweli anamaananisha
   
 12. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,333
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  ningekuwa mimi wala nisingeumiza kichwa. house girl anafaa na ndo mke huyo, mambo ya kuanza ku data na kudanganyana na maduu sina time.
   
 13. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,500
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Km kweli anampenda kwa dhati mwambie amuoe asisikilize maneno ya watu! :A S-coffee:
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Babu Mzima wa afya...Anaota jua!

  Kama wewe ni size 9/10 panda twende....Mbali ya hapo nitakutafutia boda boda!
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Lizzy please,

  How many times should be saying this....

  Ni vigumu sana, tena sana kwa mwanamume kupenda aisee....Tatizo ni kwamba ama mnasahau haya maneno au hamuyaamini.. Na mbaya zaidi mnadhani tuko sawa!! Mwanamume anatafuta maslahi na vigezo vyake kabla hajaanza kuu-condition moyo wake kumpenda mwanamke!!

  Ngoja niishie hapa kwanza!!
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Dec 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Babu endeleeni hivyo hivyo na ugumu wenu, mimi bado ntaendelea kupinga na sitomshauri mtu aoe/aolewe na mtu iwapo yeye au huyo mwenzake hampendi kwa dhati maana ndio mwanzo wa kutengeneza viota nje bila kusahau kuleteana dharau na magonjwa ndani.
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Lizzy,

  Kuna vitu ni vigumu sana kuvibadilisha...Wenzio tumeishi na bibi zenu hadi tunazeeka ila hatukuwahi kuwa na vitu nyie mnaita love at first sight...Mwanamume unampenda mwanamke baada ya kuwa ama vigezo vyako vimetimia au vingine umeachana navyo.

  Kama huamini wewe endelea hivyo hivyo...ila ipo siku utaujua ukweli...I wish ungerudi haraka kumsimulia Babu DC!!
   
 18. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #18
  Dec 5, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
   
 19. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #19
  Dec 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,135
  Likes Received: 6,629
  Trophy Points: 280
  kwani ni nini kimemtanguliza huyo shemejiyo.
  msije mwingiza na mjakazi wa watu kwenye hilo janga.
  kama ni marazi ya kawaida, sioni kama kuna tatizo la ndoa hapo.
   
 20. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #20
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Jamaa si anaoa mwanamke na sio housegirl?

  Kuna watu wengi sana waliooa wanawake wenye status na imeshindikana!

  Aweke ndani!
   
Loading...