Kafa mara mbili. Huko aliko atakuwa bado anateseka sana

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,347
11,447
Karibia mwezi mzima....nmeteseka sana mimi. Sikuwa nikilala...hata mchana tu nmekuwa nakaa room kwa mashaka. Documents zangu zimeharibiwa na pesa zangu zaidi ya mamilioni ya shilling. Ni kama billion 2 hivi.

Maana nlikuwa nmeandaa project moja yaani min ningepata bil 2. Ikaharibiwa vibaya sana. Nlikuwa na uchungu kuwa why mtu anifanyie ukatili hivi.

Huyu panya hakuwa wa kawaida...alitumwa kabisa. Niamini mimi.nlikuwa namwekea mtego haukamati. Nikamwekea zile sumu za vidonge vya mifupa na nyama. Hali. Kwenye nyanya hali. Kwenye samaki hali.

Nikawaza nikasema pengine anatumia kitimoto...ingawa ni kharamu kwangu...ila nikapiga moyo konde. Nikaenda chukua vipande kwa Shayo... Ikaleta mzozo....maana sister alipandisha maruhani yake...hata sijui alijuaje nimeleta hiyo issue. Ingawa najua shem baba abdul huwa anakula huko huko anasukutua na konyagi.

Basi ikawa issue ndani dhambi zote nikabebeshwa mimi...laana na makhurutisiwa yote nikamwagiwa mimi. Nikasema lahaulaah lakwata... Sisi wengine tuna damu ya kunguni.

Basi nikawaza karibia week nzima.nikanda nunua sumu kwenye box kama utambi mwekundu....nikamwekea. akala vizuri akashushia na maji...nikamwona tu mchana kabisa hivi anapita tu akipiga mluzi...nlichoka sana.nikamfuata muuza sumu maana alinambia ile ndo kiboko.

Muuza sumu akasema issue pale ilikuwa ni maji.kuwa panya yule alipoona sumu imembana akaenda kunywa maji.nikamwambia basi hamna shida anipe na sumu nyingine ya kuweka kwenye maji.

Nikapewa nikaenda tandaza room yote sumu kiasi kwamba usiku sikulala maana nlihisi ngeweza ota ndoto nakula tambi nyekundu kumbe ndo nakula sumu.basi nikaweka na maji yenye sumu kali sana.naamini ile sumu ingemuua hata tembo.

Panya akaona nmeweka tambi...akacheka sana..si ashajua anakula tambi anashushia na maji anaenda kulala. Akala tambi ambazo ni sumu. Akaenda shushia na maji yenye sumu... Babaaaake....alikauka pale pale...alikufa mara mbili.mara ya kwanza kwa kula tambi sumu mara ya pili kwa kunywa maji sumu.

Sasa hivi home kumetulia sana...sina tena wasiwasi room.nawaza huko aliko panya atakuwa anapata mateso sana...maana amekauka amekuwa mweusi kama kachomwa moto. Ile sijui ni sumu gani....hatari sana..

Sasa napumzika huyu panya room ameenda kuzimu kwao. Shenzi zake...mazafanta kabisa.
 
Humu Kuna vituko vingi aise.haya Sasa leo tumeletewa panya mjanja na mtega sumu!! mmmmhhhh, bil.2 hivi ,shekhe zilikuwa shekeli halali !!? au .tunaweza kumlaumu panya kumbe alikuwa sahihi.ila pole kwa kupoteza 2 bil.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom