Mchekechoni
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 279
- 19
- Thread starter
- #41
Yaani hivi vijamaa vinanikera?.....Viswahili sana!....Mbaf...Ndo Makamba kaweka historia ya Katibu Mkuu asiyekuwa na digrii!...
Sometimes, nashindwa kujizuia machozi nikiwakumbuka viongozi mahiri waliowahi kuongoza sekretarieti kuu ya ccm, miongoni mwao kwa uchache wakiwemo Daudi Mwakawago na Philip Mangula. CCM ya leo imepoteza dira, haina mwelekeo wala mvuto kwa wananchi. Kidumu Chama cha Mapinduzi kipi, hiki hiki au kingine? Mangula kama unanisoma tafadhali ingia jamvini JF utupie japo mistari miwili ya kutujenga wanaccm wa ukweli tuliosalia. Jinsi JK anavyoirostisha ccm ni sawa na kundi la kondoo lililokosa mchungaji, ni kama kusema 'mchungaji katokomea kusikojulikana, na kundi la kondoo wake limetawanyika' . Wapi Gama, wapi Tandau, wapi Ali Ameir? Turudishiwe CCM yetu tukomae nayo kivyetuvyetu na mafisadi wote tuwatose!