Kadi yangu ya CCM niifanye nini?

Yaani hivi vijamaa vinanikera?.....Viswahili sana!....Mbaf...Ndo Makamba kaweka historia ya Katibu Mkuu asiyekuwa na digrii!...

Sometimes, nashindwa kujizuia machozi nikiwakumbuka viongozi mahiri waliowahi kuongoza sekretarieti kuu ya ccm, miongoni mwao kwa uchache wakiwemo Daudi Mwakawago na Philip Mangula. CCM ya leo imepoteza dira, haina mwelekeo wala mvuto kwa wananchi. Kidumu Chama cha Mapinduzi kipi, hiki hiki au kingine? Mangula kama unanisoma tafadhali ingia jamvini JF utupie japo mistari miwili ya kutujenga wanaccm wa ukweli tuliosalia. Jinsi JK anavyoirostisha ccm ni sawa na kundi la kondoo lililokosa mchungaji, ni kama kusema 'mchungaji katokomea kusikojulikana, na kundi la kondoo wake limetawanyika' . Wapi Gama, wapi Tandau, wapi Ali Ameir? Turudishiwe CCM yetu tukomae nayo kivyetuvyetu na mafisadi wote tuwatose!
 
kuna jambo moja tu, nasubiri then hiyo kadi nitaitumbukiza chooni,am fed up vibaya mno. na huyo Makamba kusema milango imefunguliwa kumenipa hasira vibaya mno......tumekitumikia chama leo,mpuuzi mmoja kisa tumehoji kuhusu DOWANS anasema milango imefunguliwa.....lets see,am happy when they are frustrated......tuko wengi tu kila siku tunajadili tufanyeje na hizo kadi.......bora usiwe na chama kuliko uwe na chama kinachokuangamiza wewe na kizazi chako......umeme tabu,huduma za afya mbovu,miundombinu ndo hiyo,elimu ndo hiyo yaani........:A S 20:

Michelle, naona kama jamaa wa ikulu wamekanusanusa haka kathread, maana kuna dalili za mageuzi makubwa ya uongozi wa juu kwa kuanzia na Makamba kabla ya mwisho wa mwezi huu. JK naye jana kakubali yaishe yacje kumkuta ya misri na algeria, ndio maana karidhia kwa shingo upande DOWANS iclipwe, tusubiri tuone mwisho wa mwezi cmbali. Ila wakigeuka geuka kama vinyonga, cha moto watakiona, wanaccm hatutakaa kimya ng'o!
 
Tuko maelfu kwa maelfu wanachama hai kabisa wa chama cha mapinduzi, lakini tumechoshwa kabisa jinsi chama kinavyozidi kutumbukia shimoni kila kukicha, tufanyeje? Na hizi kadi zetu tumeshazilipia hadi Dec.2011, tuzifanye nini? JK uenyekiti umemshinda, na Msekwa umri umesonga, Makamba ndio ucseme, naona tupangue sekretarieti nzima tuanze tena moja kama mwaka 1977, au wana ccm wenzangu mnasemaje? Tukidharau mwiba, guu litaota tende na wananchi wanazidi kuteseka. Viva ccm viva, ila ufisadi ni kansa na dawa ya kuutokomeza tunayo sisi wananchi!
irudishe ulipoitoa
 
bado una kadi ya ccm?
Bado ninayo maana naamini katika mapinduzi ya dhati sambamba na azimio la arusha(misingi ya utu). Kwa sasa silipi ada! Uchaguzi mkuu uliopita sikukipa kura yangu mimi na rafiki zangu maana tunataka mapinduzi yale tuliyolilia na enzi za Mwaaaalimu.
 
kidumu chama cha mapinduzi. Mapinduziiii.........daimaaaaa!
 
Tuko maelfu kwa maelfu wanachama hai kabisa wa chama cha mapinduzi, lakini tumechoshwa kabisa jinsi chama kinavyozidi kutumbukia shimoni kila kukicha, tufanyeje? Na hizi kadi zetu tumeshazilipia hadi Dec.2011, tuzifanye nini? JK uenyekiti umemshinda, na Msekwa umri umesonga, Makamba ndio ucseme, naona tupangue sekretarieti nzima tuanze tena moja kama mwaka 1977, au wana ccm wenzangu mnasemaje? Tukidharau mwiba, guu litaota tende na wananchi wanazidi kuteseka. Viva ccm viva, ila ufisadi ni kansa na dawa ya kuutokomeza tunayo sisi wananchi!

Hizo kadi zenu ziwekeni kama kumbukumbu (souvenir) siku moja mtasimuila wajukuu zenu na pengine kuwaeleza mlivyoshiriki kulifikisha Taifa hapa lilipo.

Wanachama wa ccm Historia itawahukumu kwani kwa kiasi kikubwa mnawajibika kwa matokeo ya uongozi tulio nao sasa hivi, na pengine kwa asilimia kubwa ndio wamekuwa wanufaika wakubwa wa bakshishi nyakati za chaguzi kupitia takrima, posho za vikao, mikopo ya vikundi na hata pesa za kununulia kura. Uwingi wenu hamjautumia kutuwekea uongozi mzuri bali mmekuwa mkiangalia zaidi mnachopewa wakati ule na baadae kujaribu kutupa lawama kwa wasiohusika.
 
Edson, kadi yangu ya ccm ninayo na ina picha yangu na risiti ya ada niliyolipia hadi Dec.2011 hilo si jambo baya hata kidogo. Sasa problem ni uongozi ndani ya chama chetu, ujue uongozi ukiwa mbovu chama kinadorora dorooo...lakini uongozi ukiwa imara hakuna fisadi atakayekatiza na watz wote wataipenda ccm. Hoja si kukihama chama au kutupa kadi chooni, mimi naijua vema ccm ilikotoka ila kwa kweli inakokwenda ndio ckujui. CCM ya jana sio hii inayosherekea kuzaliwa kwake leo, believe me! Niifanye nini kadi yangu ya ccm jamani, nina uchungu na taifa langu!

usiitupe, mimi ninayo nilichofanya nimekuwa mwanaharakati imara.Nikifungua droo naitazama na kutokwa machozi.Lakini uwezo wa kufanya jambo sina,kwani tungekuwa na mshikamano tungeandamana wanachama na kudai mabadiliko ya ungozi wa juu wa chama kukinusuru.
 
Tuko maelfu kwa maelfu wanachama hai kabisa wa chama cha mapinduzi, lakini tumechoshwa kabisa jinsi chama kinavyozidi kutumbukia shimoni kila kukicha, tufanyeje? Na hizi kadi zetu tumeshazilipia hadi Dec.2011, tuzifanye nini? JK uenyekiti umemshinda, na Msekwa umri umesonga, Makamba ndio ucseme, naona tupangue sekretarieti nzima tuanze tena moja kama mwaka 1977, au wana ccm wenzangu mnasemaje? Tukidharau mwiba, guu litaota tende na wananchi wanazidi kuteseka. Viva ccm viva, ila ufisadi ni kansa na dawa ya kuutokomeza tunayo sisi wananchi!

Acha ujinga kama umekichoka Chama basi rudisha kadi yao na chukua ya chama unachokitaka. Vile vile kuwa na kadi ya chama zaidi ya kimoja sio dhambi wala uvunjifu wa sheria.

fanya maamuzi sahihi na sio kuleta hoja mgando hapo. Kuna wengi wanajiunga na wengi wanajitoa lakini chama kimayea na kuchukua ushindi wa sunami.

Jitoe tu wengine wengi wanataka kuingia.
 
Endelea kulipia kadi yako ili uwe mwanachama hai, nashauri usichoke kutoaushauri wako katika chama chako. si mna vikao kwan vikao vyenu vimekwisha?
 
Acha ujinga kama umekichoka Chama basi rudisha kadi yao na chukua ya chama unachokitaka. Vile vile kuwa na kadi ya chama zaidi ya kimoja sio dhambi wala uvunjifu wa sheria.

fanya maamuzi sahihi na sio kuleta hoja mgando hapo. Kuna wengi wanajiunga na wengi wanajitoa lakini chama kimayea na kuchukua ushindi wa sunami.

Jitoe tu wengine wengi wanataka kuingia.
mAKAMBA POLE SANA MKUU! ILA CCM IMECHOKA MKUU!
 
Unanikumbusha jinsi tulivyokuwa tunabambikiziwa JKT hizo kadi baada ya propganda kali za kada wa chama. That time ilikuwa mkiingia kweye kipindi cha siasa inakuwa mapozeo ya mitulinga jeshini.
 
Tuko maelfu kwa maelfu wanachama hai kabisa wa chama cha mapinduzi, lakini tumechoshwa kabisa jinsi chama kinavyozidi kutumbukia shimoni kila kukicha, tufanyeje? Na hizi kadi zetu tumeshazilipia hadi Dec.2011, tuzifanye nini? JK uenyekiti umemshinda, na Msekwa umri umesonga, Makamba ndio ucseme, naona tupangue sekretarieti nzima tuanze tena moja kama mwaka 1977, au wana ccm wenzangu mnasemaje? Tukidharau mwiba, guu litaota tende na wananchi wanazidi kuteseka. Viva ccm viva, ila ufisadi ni kansa na dawa ya kuutokomeza tunayo sisi wananchi!
wewe nakushauri uhamie chadema
 
Ngoja tuone watakavyofanya DOWANS, ndio kitaeleweka. Maana dado kuna watu wanaleta mchezo.

Hakuna la kusubiri. Wewe utakuwa sikio la kufa lisilosikia dawa. Maovu yaliyofanywa na CCM hayana ata kipimo. Mtu mwenye akili na mcha Mungu awezi kuendelea kuwa CCM. Maovu yanayoendelea ni zaidi ya bln 94 za DOWANS. Kadi chaomeni. Mwombe Mungu akunusuru maana wewe umeshatengenezwa msukule wa CCM. Kwa kifupi wanachama wa CCM wamekuwa kama toilet paper ambayo haina maamuzi kutumika maala pachafu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Mungu nibariki
 
Back
Top Bottom