Kadi yangu ya CCM niifanye nini?

Mchekechoni

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
279
19
Tuko maelfu kwa maelfu wanachama hai kabisa wa chama cha mapinduzi, lakini tumechoshwa kabisa jinsi chama kinavyozidi kutumbukia shimoni kila kukicha, tufanyeje? Na hizi kadi zetu tumeshazilipia hadi Dec.2011, tuzifanye nini? JK uenyekiti umemshinda, na Msekwa umri umesonga, Makamba ndio ucseme, naona tupangue sekretarieti nzima tuanze tena moja kama mwaka 1977, au wana ccm wenzangu mnasemaje? Tukidharau mwiba, guu litaota tende na wananchi wanazidi kuteseka. Viva ccm viva, ila ufisadi ni kansa na dawa ya kuutokomeza tunayo sisi wananchi!
 
Ngoja tuone watakavyofanya DOWANS, ndio kitaeleweka. Maana dado kuna watu wanaleta mchezo.
 
Hamjalazimishwa kuweko huko hata mwalimu aliwahi kusema "CCM sio baba yangu na wala mama yangu". Isijekuwa mmekichoka chama kwa kuwa walitegemea mbebwe mmesahaulika kama ndo hivyo hata mkiingia kwenye vyama mbadala mtachemsha tu. Tafutane chama mbadala mjiunge nacho mkishindwa kukipata kuweni raia msio na vyama ila wanaharakati.
 
Libaba umeongea point, ila hatujakichoka chama chetu cha mapinduzi na kukihama kwa sasa si muhali, maana bado ccm ni tegemeo pekee na tumaini la kweli kwa mamilioni ya watanzania. Sema tu haka kaupepo kabaya ambako kanakolezwa na uongozi mbovu wa ngazi za juu aidha kwa makusudi kabisa au kwa kiburi na kujikweza, ndio tumefika njia panda kiasi cha kujiuliza sisi kama wanachama wa kawaida kabisa wa ccm tufanye nini na kadi zetu? Tufanye mapinduzi ndani ya chama kumng'oa JK na sekretarieti yake au tubadili katiba ya ccm ili mwenyekiti wa chama taifa kamwe asiwe na kofia mbili, yaani akiukwaa tu urais wa jamhuri automatically unaitishwa uchaguzi kumpata mwenyekiti mpya! Tuchangie hoja wanaccm na wananchi wote kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa letu.
 
Tuko maelfu kwa maelfu wanachama hai kabisa wa chama cha mapinduzi, lakini tumechoshwa kabisa jinsi chama kinavyozidi kutumbukia shimoni kila kukicha, tufanyeje? Na hizi kadi zetu tumeshazilipia hadi Dec.2011, tuzifanye nini? JK uenyekiti umemshinda, na Msekwa umri umesonga, Makamba ndio ucseme, naona tupangue sekretarieti nzima tuanze tena moja kama mwaka 1977, au wana ccm wenzangu mnasemaje? Tukidharau mwiba, guu litaota tende na wananchi wanazidi kuteseka. Viva ccm viva, ila ufisadi ni kansa na dawa ya kuutokomeza tunayo sisi wananchi!
Mimi kadi yangu ipo nimeiweka tuu! siilipi ada niwalipe MAFISADI!
 
Henge, Mzimu wa Sokoine bado umo ndani ya CCM, Subiri kidogo uone. Mbona nimeona mengi. Hata Mhe Mnyika anajua. Muulize.
 
Endeleeni kuwa nazo! Siku ya mabadiliko ya kweli zitatusaidia kuwajua ambao wameendelea kuwapa kiburi na sababu wanyonyaji na wezi wa nchi hii!! Anayesiadiana na mwizi katika kitendo cha wizi au kumficha naye ni mwizi!
 
Misiri bwana wee. Kuna wasomi, wanafanya kweli, nyinyi giza litawafanya muwe weusi kama mkaa. Hivi siku ya kuwalipa Dowans kadi hii Duhhh!
 
bado una kadi ya ccm?

Edson, kadi yangu ya ccm ninayo na ina picha yangu na risiti ya ada niliyolipia hadi Dec.2011 hilo si jambo baya hata kidogo. Sasa problem ni uongozi ndani ya chama chetu, ujue uongozi ukiwa mbovu chama kinadorora dorooo...lakini uongozi ukiwa imara hakuna fisadi atakayekatiza na watz wote wataipenda ccm. Hoja si kukihama chama au kutupa kadi chooni, mimi naijua vema ccm ilikotoka ila kwa kweli inakokwenda ndio ckujui. CCM ya jana sio hii inayosherekea kuzaliwa kwake leo, believe me! Niifanye nini kadi yangu ya ccm jamani, nina uchungu na taifa langu!
 
Vumilia kwani yataka moyo kuingia kwenye gari usiloelewa linaelekea wapi, na hauna maamuzi ya kulishawisha lielekee mahali salama. Nahisi kuna ukosefu wa maoni ndani ya viongozi wa chama ndo maana mnaona mazonge. Cha kufanya achaneni na njaa (kuhongwa T-shirt, pilau na Sh 5000) na muziishe kanuni za cham- rushwa kwangu mwiko, kisha mchaguwe viongozi bora kama bado wamo ndani ya cham. Natumai hapo mtakuwa mmejitendea haki nyinyi wenyewe wanachama, lakini kwa kuendekeza njaa hakika shimoni mtaingia na mtasaidia kujifukua wenyewe. Nawakilisha
 
Unatupa taarifa au unauliza swali. Kama ni swali Jibu unalo. Kama ni taarifa tunashukuru kujua wewe ni kada.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom