Idd Azzan atishiwa kunyanganywa kadi;Ataka Sekretarieti ya CCM Mkoa na k/mati ya Siasa ijivue gamba

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797




Na Anneth Kagenda

MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni, Bw. Idd Azzan amelalamika kuwa kuna watu ndani ya chama hicho mkoa wa Dar es Salaam wamemtishia kumnyanganya kadi
yake uanachama, jambo ambalo halimtishi.

"Kuna mtu mmoja aliniambia kwamba tutakunyanganya kadi yako ya uanachama kwa madai kuwa ninataka Sekretarieti ya CCM Mkoa na Kamati ya Siasa ijivue gamba, hata wakiitaka leo nitawapa lakini ni lazima tuseme ukweli ili kukinusuru chama chetu," alisema.

Hayo aliyasema Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya kuweka msisitizo kwamba hababaishwi na maneno ya baadhi ya watu pale anapotaka kusema ukweli ndani ya CCM kwa nia ya kukinusuru chama.

Alisisitiza kwamba Sekretarieti ya Mkoa na Kamati ya Siasa lazima ijiuzulu ili chama kiweze kujipanga na kujiwekea mikakati endelevu ya kushika dola bila kukumbwa na kashfa za hapa na pale zinazoendelea ndani na nje ya chama.

"Sekretarieti ya Mkoa inanitisha eti kwanini nilisema wajivue magamba, wananiambia watanionyesha, lakini mimi ninachoamini ni kwamba pale ukweli unaposemwa wazi wazi bila kificho huwa unauma lakini lazima tuuseme kila wakati.

"Viongozi wa Mkoa wamegawanyika katika makundi mawili ambayo yamechangia kwa asilimia kubwa kukidhorotesha chama tangu mwaka 2007. Yaliwaengua madiwani wa Kata na wale wa viti maalumu waliokuwa wakipendwa na wananchi, na kusababisha wananchi kuvipigia kura vyama vya pinzani," alisema.

Aidha alisema kuwa Aprili 14, mwaka huu Katibu wa CCM Mkoa, Bw. Kilumbe Ng'enda aliitisha kikao cha makatibu kata na madiwani na kuwaambia kwamba hajivui magamba ng'o na kusema kuwa alitakiwa kujibu kwa hoja siyo blabla.

Bw. Azzan aliongeza kwamba nia yake ya kutaka sekretarieti hizo zijiuzulu ni kutokana na kwamba kuna mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kimakosa ikiwa ni pamoja na viongozi hao kutotaka kuitisha mikutano ambayo watu watatoa dukuduku zao za namna ya kuboresha na kukiendesha chama.

"Tulikuwa tunatakiwa kufanya vikao tangu Novemba au Desemba lakini cha kushangaza mpaka leo hatujafanya kikao chochote, je, ni kwanini hawataki vikao hivyo vifanyike?.

"Sasa mimi ninasema kwamba wasipofanya vikao hivyo ndani ya mwezi huu ili viongozi watoe dukuduku lao juu ya kilichosababisha CCM kushindwa kufanya vizuri kwenye uchaguzi uliopita, nitaitisha mkutano na waandishi wa habari na kuyaanika yale yote waliyoyafanya mpaka chama kikapoteza majimbo mawili na kata nyingi," alisema.
 
Shy-Rose atafurahi Idd Azzan kunyang'anywa kadi ya CCM

Na inanonyesha kuwa Upinzani utalichukua jimbo
 
Baba_Enock bado hajafahamishwa maana ya neno "kujivua gamba"! Kwa mwenye kufahamu maana please msaada wako ni muhimu sana!
 
Baba_Enock bado hajafahamishwa maana ya neno "kujivua gamba"! Kwa mwenye kufahamu maana please msaada wako ni muhimu sana!

An empty stomach is not a good political adviser. Sorry I will when my stomach is full !!!
 
Shy-Rose atafurahi Idd Azzan kunyang'anywa kadi ya CCM

Na inanonyesha kuwa Upinzani utalichukua jimbo


Lingekuwa tayari jimbo la CDM iwapo yule Mtatiro angeacha kwenda CUF kujipima nguvu na Kamanda Mnyika kule Ubunge na badala yake engeingia CDM na kugombea Kinondoni na bila shaka yoyote angeweza kumtokomeza Azzan!
 
Sasa wanamtafuta mchawi na wachawi wapo humohumo ndani ya ccm? Jimalizeni kbs tuchukue jimbo hilo
 
Hivi karibuni CCM imekuja na kauli mpya "MAFISADI WOTE WAJIVUE MAGAMBA KUANZIA TAIFA MKOA MPAKA CHINI KABISA" lakini chakusikitisha chama hicho hicho katika Mkoa wa Dar kimeamua kumpa adhabu kali ya kumtaka Mbunge Iddi Azzan kuto zungumza na vyombo vya habari, pia imempa adhabu ya kuto kugombea nafasi yoyote katika chama hicho kwa muda wa miezi 18 kuanzia jana. Adhabu hizo zimetolewa na Juma Simba Gaddafi.....juzi kupitia magaazeti mbalimbali.

Kisa cha kuadhibiwa Mhe Iddi Azzan nikutokana na kuitaka Sekretarieti ya Mkoa Huo wa Dar es salaam ijivue magamba kutokana na uchafu na ufisadi waliokuwa nao viongozi hao. hasa ukizingatia wameshindwa kuitisha mkutano wa kutathmini uchaguzi mkuu wa 2010 kwa kuogopea kushambuliwa na wanachama wao.

Swali langu kwenu wana Jamii Forums.........JE NI KWELI CHAMA HIKI KINATAKA MAFISADI WAJIVUE MAGAMABA HASA UKIANGALIA ANAESEMA UKWELI NDIO ANADIDIMIZWA?????
 
Wanachama na Chama chao wote ni mafisadi, Magamba yataendelea kuwaparua tu wayavue wasiyavue: kwanini anayejiona ni msafi ndani ya CCM asijiengue na kufuata njia/chama kilicho kisafi??
 
Kwa ujumla Chama Cha Magamba hakiwezi kujisafisha, kwani Chama kimetekwa na mafisadi na lazima waendelee kutetea maslahi yao. Wako tayari kuwafukuza ndani ya chama waadilifu wachache walisalia, lakini maslahi yao yalindwe.
 
USANII MTUPU! Ufisadi umetapakaa ndani ya CCM yote kuanzia Viongozi wa juu kabisa katika ngazi ya Taifa hadi viongozi wa tarafa hivyo kamwe hawataweza kujisafisha.
 
Senema ya masarakasi inaendelea! Langu jicho mkono kwenye shavu. Twende kazi Magambaz.
 
Hakuna msafi ndani ya ccm -Source Sophia Simba.
kuwashughulikia mafisadi ni kuhatarisha usalama wa taifa - source Mtoto wa mkulima.
Wala rusha ninawafahamu na nimewapa muda wajirekebishe - Source mkulu aliyepangishwa pale Magogoni.
Hapo waweza changanya na za kwako kama kuna kitu unaendelea kutegemea kutoka kwa Nyoka, jitie moyo akimaliza kujivua gamba atakuwa na nguvu zaidi ya kushambulia. Dawa ni kumpiga kichwani na kumuua kabisa.
Tafakari
 
An empty stomach is not a good political adviser. Sorry I will when my stomach is full !!!

Kiu kweli naona ccm suala la kujivua magamba wanacheza nalo maana haimkiniki mafisadi hao hao wampe adhabu mtu amabet anawatuhumu wao kwa ufisadi then wao wamuadhibu'
 
Jamani mnakosea mnapojaribu ku support azan, huyu hana jeuri ya kuwaita wenzake mafisadi wakati yeye pia ni fisadi kwani ktk uchaguzi uliopita alionga sana ili kuchaguliwa kwahiyo wenzake wanamlalamikia kwa nini anawaita wenzake mafisadi wakati naye ni mwenzao.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom