Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,304
Jana kwenye mtandao wa kijamii niliona jinsi watu walivyokuwa kiishambulia kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania baada ya kuendesha sherehe za Miss Tanzania 2011 kwakweli hali ilikuwa mbaya zaidi kwa dada yetu Mwamvita Makamba lakini baadae nilifarijika kuona Vodacom wametoa namba za kuchangia kwa walioadhirika na maafa ya Zanzibar. Naleta hoja mbele yenu je Vodacom wamefanya sawa kuchangisha pesa baada ya kilichojiri usiku wa Jumamosi?
Binafsi nadhani bado kuna kitu kina miss maana tangazo lao linaeleza unatuma msg unakatwa shs 1000 na utume pesa kwa njia ya m pesa kuanzia shs 1000 ina maana hizi pesa ni sisi wenye majonzi ndio tunaoweza kuzituma ikisha zikawakilishwa kwa walioadhirika na janga lile na sio wao kama wao? Au pengine nitakuwa sijalielewa vizuri tangazo lilio kwenye tweeter na nitakuwa radhi kusahihishwa.
Naomba niwakilishe na mtoe mawazo yenu.
Shukran.