Igunga: Jinsi wakala wa CHADEMA alivyouliwa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Igunga: Jinsi wakala wa CHADEMA alivyouliwa...

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by MgungaMiba, Oct 12, 2011.

 1. M

  MgungaMiba JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 80
  Taarifa rasmi inaeleza kuwa Marehemu Mbwana Masoud, aliekuwa Wakala wa CDM kutokea Ubungo DSM, alipotea tar 2/10/2011, siku ya uchaguzi, lakini ukweli ni kuwa siku hiyo ndiyo ilipogundulika kuwa amepotea baada kuhitajika kupelekwa kituoni kwake na kukosekana.

  Hali halisi ni kuwa Mbwana Masoud usiku wa tar 1/10/2011 (Mkesha wa kuamkia siku ya uchaguzi) baada ya kula chakula cha jioni alitoka kunyoosha miguu, ingawa palitolewa Hali ya tahadhari lakini hali ilionekana iko shwari. Kumbe kulikuwa na kundi la mabaunsa wanne wa CCM wakimfuatilia, na inaelekea walikuwa wakiwasiliana kwa simu na gari lao, kwani mara walipomvamia, tena mbele za watu, gari hilo aina ya L/Cruiser Hardtop jeupe lenye namba T***ARD, mali ya CCM, Mara nyingi katika kipindi cha kampeni hizi lilikuwa likitoka usiku na mchana huwa linapaki, dereva wake ni yule alieshiriki kuwapiga mabapa ya mapanga wana CDM waliokuwa wakidai matokeo ya uchaguzi yatangazwe.

  Ingawa Mbwana alijitahidi kujitetea asichukuliwe lakini alizidiwa nguvu, alijaribu kupiga kelele kuomba msaada lakini alipigwa kabari ya nguvu, kabla ya watu waliokuwa karibu hawajajua la kufanya (kwani tukio lenyewe lilifanywa kwa kasi, pia walijifanya kama ni watu wanaofahamiana ila wana mzozo fulani) walimtia kwenye gari Hilo na kuondoka nae kwa kasi kuelekea upande wa Mwanzugi.

  Mafedhuli hao wa CCM, Mateso waliyomtesa Mbwana Masoud kabla ya kumtoa roho ni Mungu na wao wenyewe ndio wanajua, lakini kwa jinsi hali ya maiti yake ilivyokutwa baada ya kutupwa kwenye vichaka karibu na Magereza siku ya tar 9/10/2011 inaonesha dhahiri unyama aliofanyiwa hata huko Somalia walikozoea kuuana hakuna unyama wa aina hii.

  Alikutwa na suruali tupu bila shati, SHINGO YAKE ILIKUWA IMEVUNJWA KWA NGUVU, MACHO YAKE YAMETOBOLEWA NA HAYAONEKANI, KICHWA CHAKE KIMEPASULIWA KWA NYUMA CHINI YA KISOGO, KIFUA CHAKE KIMEBABUKA KAMA VILE AMEMWAGIWA AINA FULANI YA TINDIKALI, mwili wake unaonesha alipigwa sana kabla kuuawa kinyama.

  Kilichotushangaza ni kuwa mwili huo uliotupwa hapo unaonesha dhahiri hakuuliwa siku hiyo ya tar 9/10, lakini haukuwa umevimba Kama kawaida bali ulikuwa unaonesha dhahiri kuwa ulitiwa dawa ya kuhifadhia maiti, kwa vyovyote vile wauaji wake hawakuwa majambazi wa kawaida wa mtaani ambao huua na kuishia zao, bali ameuliwa na Organization kamili yenye motive ya kuua wakala wa CDM, ikumbukwe kwamba Serkali ya CCM awali ilitangaza kukataza mawakala kutoka nje ya jimbo, baada Wakili Tundu Lissu kwenda kumfundisha sheria Msimamizi wa Uchaguzi Igunga, ndipo wakaruhusiwa kwa shingo upande, lakini njiani walisumbuliwa sana na maaskari kwa maelekezo ya wakubwa w CCM.

  Alitekwa ili kuwatisha mawakala wengine waogope kuwajibika, uongozi wa CDM ulitumia busara kutopiga kelele na badala yake kwenda kutoa taarifa Polisi kimyakimya, ingawa Polisi yenyewe haikuchukua hatua yoyote ya msako, mawakala wa CDM waliwajibika vilivyo vituoni na hakuna kura iliyoibiwa, ikabidi Serkali iisaidie CCM ishinde kwa nguvu kwa kuwazuia maelfu ya Vijana waliofika vituoni kupiga kura ingawa walipoteza shahada zao, kwa kujaza form No 17, mwanzo waliwaruhusu kupiga kura Kama sheria inavyotaka, lakini walipoona wanazidi kuwa wengi, ilipofika saa 4 asubuhi Mkurugenzi aliagiza wasiruhusiwe kupiga kura, wakafukuzwa, wengine hawakukuta majina yao kwenye daftari, wengine walikataliwa kupiga kura kwa kuwa waliorodheshwa kuwa wamekufa! Just imagine unaenda kituoni na shahada yako kupiga kura unazuiwa usipige kwa sababu wewe umeshakufa!

  Haya; pamoja na kutumia vibaya mahindi ya msaada kama rushwa siku moja kabla uchaguzi, na kampeni potofu siku ya uchaguzi kuwa mgombea wa CDM amejitoa kwa hiyo haina haja kumpigia kura, ndiyo yalichangia ushindi kiduchu wa CCM.

  Nirudi kwenye mada ya msingi ya mauaji, nisameheni najichanganya kwani Nina machungu mengi, Maiti ya Mbwana Masoud ilipookotwa, ilikutwa na kipande cha karatasi ambacho wauaji walitaka iaminike kuwa marehemu aliiandika baada ya kuuawa akitaja majina ya waliomuua, Polisi waliipuuza karatasi hiyo ingawa bado wanaishikilia, inazidi tu kuthibitisha kuwa wauaji wamejaribi kuficha kitendo chao na hivyo kukamilisha misingi ya First Degree Murder!

  CCM Arusha iliua kwa kutumia Polisi wa serkali yake, lakini Igunga CCM imeua kwa kutumia Mungiki wake iliowalipa na kutumia gari lake, gharama zitokanazo na kodi zetu, Masoud akiwemo.

  Salaam kwenu enyi Wauaji CCM, mnahubiri Amani na Utulivu majukwaani lakini Mikono yenu imetapakaa Damu ya wasio na Hatia, hakuna waliofanya hivyo wakafanikiwa mafanikio ya kudumu, mmepata Spasmodic Victory lakini Hakika mtaSuffer Eternal, Shameful Defeat!

  Enyi wauaji CCM, Salaam kwenu kutoka kwa maelfu ya vijana wa Igunga waliodhulumiwa haki Yao ya kupiga kura kwa makusudi, Tunawaambia, Sukilizeni Vizuri enyi Mafedhuli, Haki itatendeka Igunga, however long it might take, lakini HAKI LAZIMA ITATENDEKA TU!

  Tunajua hamuamini Mungu Enyi Wauaji na Wazinzi wa Wake za Watu, lakini Mungu alishasema " HAKI IKIDHIHIRI, BATILI HUJITENGA, HAKIKA BATILI NDIO HUJITENGA!" Kama mnajidai hamumuamini wala kumuogopa Mungu basi Hakika Mtakumbana na Nguvu za Umma ambazo ni Kubwa kuliko nguvu za Dola!

  Umma wa Igunga una Hasira na Nyie Mafedhuli wakubwa, mnajua, Mbona hamkusherehekea vilivyo ushindi wenu hapa Igunga? Mlilipua fastafasta mkaenda kusherehekea Singida na Dar ambako mlifanya sherehe kubwa na maandamano ya kumpokea Mbunge wenu wa huko mliekuja kumtengenezea Igunga.
   
 2. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ooo!

  Shujaa wetu Masoud, Mungu peke yake na aiweke roho yako mahali pa mashujaa peponi. Hata Yesu walimfanya hivyo sababu anawaambia watu waache dhambi na kumheshimu Mungu.

  Hakika historia itasema katika Igunga na hao mafedhuli wangojee kiama 2011. Watasambaza mauaji nchi nzima na kufanikiwa?

  Naam, CCM imezoea kuua hata ndani yao wenyewe, tunakumbuka Kolimba walivyomkolimba, Mtikila alipotaka kusema jukwaani wakadai ni mwendawazimu. Sasa ushindi kwa damu mahali penye amani unatafsiriwa vipi?????
   
 3. n

  ngwini JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa style hii,something bad is going 2 happen 2015.
   
 4. MAKOSHNELI

  MAKOSHNELI JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 474
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 80
  Tiss wanahusika lazima,kweli kamdhamini mbwa sio mtu mweusi anapinga jambo la maendeleo yake mwenyewe
   
 5. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,562
  Trophy Points: 280
  Naomba kushauri CHADEMA wafanye yafuatayo:

  Kwanza watangaze kwa nguvu na kulaani tukio hili dunia nzima kwa kuunganisha na matukio mengine lakini kwa ndani kila kiongozi mpaka wa kijiji wa cdm atoe tamko rasmi.

  Pili watangaze kukodisha wapelelezi huru waliobobea kutoka nje ili ufanyike uchunguzi huru na hapa mbinu zote za kisheria zitumike ili lisikwamishwe na waahidi kutangaza matokeo wazi kabisa after specific days.

  Tatu waongee na mabalozi wa nchi zote washinikize serikali kuchukua hatua.

  Kinyume na hapo; CHADEMA watawakatisha watu tamaa. Unyama huu utoe FUNZO!
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Jamani! Jamani! Jamani!

  Hii sasa ni pigo kubwa kwa hawa magamba. Nasema hivyo nikiwa na machungu kwa yaliyomkuta ndg yetu marehemu Masoud.

  Mtazamo wangu wa haraka tena ambayo ningesema ianze muda huu ni kwamba nitakuwa wa kwanza kwa vyovyote vile kwa hawa magamba wenye uchu wa madaraka na wasio na UTU kwa Watanzania maelfu elfu wanagandamizwa na kilichopo ni NGUVU YA UMMA ndiyo ukombozi tu.

  UKOMBOZI NI SASA NA KAMA SI SASA NI SASA HIVI na Mi naona kama mbaya na acha iwe mbaya!

  Rest In Peace Mbwana Masoud!!
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mkuu wameishasema ushindi ni lazima hata kwa kutoa damu kwa wale wanaobishia ushindi huo kila kheli tz na watakao uawa wote..
   
 8. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  nasema hivi,ccm haiwezi kuondoka hivihivi 2015,na kwa taarifa yao mimi niko tiyari hata kwa vita kuwatoa madarakani hawa wauaji na majambazi wa intelijensia.shenz.i zao wote.
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,562
  Trophy Points: 280
  Hapa kisingizio cha siasa kinatumika vibaya, huu ni uhalifu wa kutisha!

  Nategemea reaction kubwa mno kwa tukio hili, sitaelewa likipita hivi hivi, sitaelewa!
   
 10. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,562
  Trophy Points: 280
  Huu ni mzaha!

  Bora viongozi wote wa CHADEMA mfungwe kutetea haki ya hii damu isiyo na hatia, narudia tena and very serious hii damu itoe FUNZO la karne!
   
 11. E

  ESAM JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Dah!

  Yaani inasikitisha sana sana sana. Polisi wanapaswa kufanya uchunguzi na kutoa taarifa ya kina sana kuhusiana na suala hili hasa kuhusiana na maiti kukutwa kama vile iliwkwa dawa na kukaushwa.

  Pia kuhusiana na gari hilolinalotajwa kuhusika katika kumteka Mbwana kama kweli lilihusika nasisitiza kama ni kweli lilihusika dereva wake awe first suspect wa mauaji haya.

  Mtoa mada naomba hiyo ya gari iweke isomeke maana hiyo gari ni muhimu ijulikane ni ya majambazi kama kweli ilihusika nasisitiza tena kama ni kweli ilihusika.

  Lakini kwa ujumla inasikitisha kweli kama watanzania tumefikia hapa kwa ajili ya cheo cha kisiasa ambacho tunadai kipatikane kwa njia ya demokrasia.

  HAPA SASA IJULIKANE ALIYEINGIZA MAKOMANDOO NI NANI?
   
 12. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Nafikiri kuna kitu kimechelewa au tunakichelewesha
   
 13. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,562
  Trophy Points: 280
  Tusifanye mzaha,CCM wanatuharibia nchi kuliko wakati wowote,maana sasa si maendeleo duni tu bali wanapanda chuki hatari!
   
 14. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,992
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  Hakuna atakae ishi milele hapa duniani,ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga,na wao wajiandae kufa kinyama hivyo hivyo tena watageukana wao kwa wao,NAICHUKIA CCM DAIMA.
   
 15. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,576
  Likes Received: 4,690
  Trophy Points: 280
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete anao uwezo kabisa wa kuzuia nchi isiingie katika machafuko kwa kukemea makada wake walioandaa mauaji haya.

  Kitendo cha CCM kuandaa makambi ya vijana na kuwapa mafunzo ya kijeshi kila kunapokuwepo na chaguzi ndogo ni ushahidi tosha kuwa CCM ndiyo chanzo cha vurugu na ubakaji wa demokrasia hapa Tanzania.

  Pia matamko yaliyotolewa na Nape wakati wa kipindi cha kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga kuwa CCM imeamua kuchukuwa jukumu la ulinzi badala ya kazi hiyo kufanywa na Polisi na kuweka angalizo kuwa wasije kulaumiwa kwa lolote ilkuwa ni sawa na tangazo la vita, kwa haya yaliyotokea ni dhahiri ni matunda ya angalizo la Nape.

  Swali langu kwa JK ni kuwa hivi haikugonga kwenye ufahamu wake kuwa kauli ile ya Nape ilikuwa inachochea vurugu za kisiasa na uvunjifu wa amani?

  Kwa ukimya wa JK juu ya viashiria vya uvunjifu wa amani hadi kupelea mauaji ya kinyama kama haya mimi lawama zangu kwa 100% nazipeleka kwa JK. Kukaa kwake kimya katika mambo kama haya ya mauji ya kisiasa yanayofanywa na chama chake ni ushahidi tosha kuwa maovu haya yana baraka zake.
   
 16. K

  Kigoma 2015 JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Na hapa BAKWATA watoe tamko kwani aliyeuwawa kikatili ni muislam aliyekwenda kulinda haki huko Igunga.
   
 17. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Kinachonishangaza, mtoa mada hajaitaja gari hiyo. Kwanini asiitaje tukaijua? ameishia kuweka xxx
   
 18. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yawezekana likawa lile gari lililohusika katika utekaji wa diwani Nanyaro Efatha japokuwa yeye alinusurika baada ya kupambana nao.
   
 19. K

  Kigoma 2015 JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kipindi cha kampeni Igunga ilitokea tafrani DC akavuliwa ushungi tu CCM+ BAKWATA wakatoa matamko mengi ikiwa pamoja na kusomwa kwa dua mbaya kama Chadema wasingeomba radhi.
  Sasa hili ni zito tena sana la mauaji ya ndugu yetu Masoud Mbwana aliejitolea kwenda kulinda haki ya wana Igunga, mauaji ya kutisha na ya kinyama yaliyofanywa na watu wenye nia mbaya kwa taifa letu. Sasa na hapa napo tunataka tamko na ile DUA kama ni kweli hapa ndipo mahala pake ili wahalif wajulikane na hukumu ifanyike hapahapa.
   
 20. d

  dr. gracemary Member

  #20
  Oct 12, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani jamani nchi yanguTanzania! hapo ndipo kisiwa cha amani kilipofika maskini! kweli? unaua ili kupata ushindi?kwa ajili ya kumwongoza nani? ukweli haufichwi kamwe.....mnauana hata nyie kwa nyie ili kupata madaraka....tuwaombee Mwakembe na Mwandosya tena watu wa kwetu MBEYA kulikoni?
   
Loading...