TANZIA Kada Maarufu wa CCM Jijini Dodoma, Egra Mamoto afariki dunia ghafla

Mwendazake Bi Egla Mamoto alikuwa Kiongozi wa CCM Jijini Dodoma.

Taarifa hii ya kushtukiza na kusikitisha zimeripotiwa na gazeti la Mwananchi la leo Disemba 27, 2020.

Tunatoa pole kwa familia na Chama kwa msiba huu mkubwa.

----
Aliyewahi kuwa Kaimu Katibu idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Egra Mamoto amefariki dunia.

Mamoto ambaye katika uchaguzi wa mwaka huu aligombea ubunge kupitia kundi la wazazi, amefariki katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma alikokimbizwa kwa matibabu baada ya kujisikia vibaya usiku wa kuamkia leo Jumapili Desemba 27, 2020.

Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM Taifam Leonard Singo ametoa taarifa iliyoeleza kuwa Mamoto aliugua ghafla.

Singo amesema marehemu alikuwa hazina katika kipindi cha uhai wake na kuwa hakupenda kuona CCM kinashindwa katika uchaguzi wowote.

Katika uhai wake alikaimu Katibu wa uhamasishaji Taifa katika kipindi cha mwaka mmoja 2015/16 ambapo katika kipindi hicho alikuwa mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana wa Uvccm.

Baadhi ya watu ambao wapo katika kundi moja la WhatsApp wamesema hadi saa nne usiku wa kuamkia leo Mamoto alikuwa akichati kwenye kundi hilo akiwatakia watu maisha mema na kumaliza mwaka salama.

Chanzo: Mwananchi
Da, ina maana CCM wameshindwa kuwatumia polisi, wakurugenzi na TISS kumzuia israil asiondoke na roho yake?
 
Kabebwa na Green guard :(
Japo binadamu sote siyo wakamilifu lakini ni vema, angalao kwa matukio kama haya, greenguards wasingrkuwa wanahusika.

Hawa wanaweza kuharibu tukio zima kutokana na historia mbaya waliyo nayo, hasa ushiriki wao katika matukio ya kishetani ya kuteka, kuua na kushambulia watu kwa sababu tu ya tofauti za mitizamo ya kisiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwili wa Mwendazake huyo aliyekuwa Kada wa CCM umepumzishwa kijijini kwao Mpwayungu Dodoma.

Pichani baadhi ya waombolezaji walioshiriki maziko hayo yaliyofanywa kwa heshima zote za Kichama

Amelala mpiganaji wetu
Mungu ampe pumziko la amani
Nimeona jeneza lina thamani kubwa kuliko nyumba ya mpendwa wetu. R.I.P dada yetu
 
Japo binadamu sote siyo wakamilifu lakini ni vema, angalao kwa matukio kama haya, greenguards wasingrkuwa wanahusika.

Hawa wanaweza kuharibu tukio zima kutokana na historia mbaya waliyo nayo, hasa ushiriki wao katika matukio ya kishetani ya kuteka, kuua na kushambulia watu kwa sababu tu ya tofauti za mitizamo ya kisiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini yeye katokea wapi?
 
Kama alilala upande wa Bwana siku akirudi mara ya pili atafufuliwa ktk ufufuo wa kwanza ili aurithi ufalme kinyume na hapo atafufuka ufufuo wa pili ambao ni wa waovu hivyo mauti ya milele

Ee Bwana tusaidie sisi tulio hai tuendelee kuwa upande wako kwa kutujalia moyo wa hekima amina
 
Duh mwenye picha yake ambayo iko full atuweke

Any way apumzike mahali panapo mstahili

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Nakumbuka kipindi anasoma pale UDSM kuna vijana walikuwa wanaenda kusali chapel ibada zile za jioni na mikesha kwa ajili ya bibie kwa kuwa alikuwa mlokole kweli kweli . Apumzike kwa Amani Egla
 
Acha ujinga wewe!! Facebook kila siku watu wanapost misiba ya ghafla tangia dec kuanza!! Tulipumzika kuanzia July mpaka Nov ila Dec vimeibuka upya!!
Kama wewe ni wa facebook sina sababu sana ya kujaribu kukubishia,ntapoteza tu muda..Corona tusione ndugu wala jirani ila ninyi tu wapuuzi
 
Kama wewe ni wa facebook sina sababu sana ya kujaribu kukubishia,ntapoteza tu muda..Corona tusione ndugu wala jirani ila ninyi tu wapuuzi

Nina accounts kwenye social media zote mkuu ,nina account hadi marafiki/darchar ya 2006 ,hi5 ,megafriends ya 2002 etc facebook kwa ajili ya kupata ndugu/marafiki niliopotezana nao wakiona jina ni rahisi kuwasiliana kwahiyo facebook natumia kwa ajili ya friends na sio kutafuta wachumba au kupost upuuzi.

Dipotivo second wave linatutandika acheni kudanganya watu!!

Marafiki2.jpg


FriendFinder.jpg


You better respect The OGs ...2005 huko Mpitimbi unacheza kombolela.
 
Back
Top Bottom