TANZIA Kada Maarufu wa CCM Jijini Dodoma, Egra Mamoto afariki dunia ghafla

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,204
4,694
Mwendazake Bi Egla Mamoto alikuwa Kiongozi wa CCM Jijini Dodoma.

Taarifa hii ya kushtukiza na kusikitisha zimeripotiwa na gazeti la Mwananchi la leo Disemba 27, 2020.

Tunatoa pole kwa familia na Chama kwa msiba huu mkubwa.

----
Aliyewahi kuwa Kaimu Katibu idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Egra Mamoto amefariki dunia.

Mamoto ambaye katika uchaguzi wa mwaka huu aligombea ubunge kupitia kundi la wazazi, amefariki katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma alikokimbizwa kwa matibabu baada ya kujisikia vibaya usiku wa kuamkia leo Jumapili Desemba 27, 2020.

Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM Taifam Leonard Singo ametoa taarifa iliyoeleza kuwa Mamoto aliugua ghafla.

Singo amesema marehemu alikuwa hazina katika kipindi cha uhai wake na kuwa hakupenda kuona CCM kinashindwa katika uchaguzi wowote.

Katika uhai wake alikaimu Katibu wa uhamasishaji Taifa katika kipindi cha mwaka mmoja 2015/16 ambapo katika kipindi hicho alikuwa mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana wa Uvccm.

Baadhi ya watu ambao wapo katika kundi moja la WhatsApp wamesema hadi saa nne usiku wa kuamkia leo Mamoto alikuwa akichati kwenye kundi hilo akiwatakia watu maisha mema na kumaliza mwaka salama.

Chanzo: Mwananchi

--- MAZISHI 30 Desemba 2020---

Mwili wa Mwendazake huyo aliyekuwa Kada wa CCM umepumzishwa kijijini kwao Mpwayungu Dodoma.

Pichani baadhi ya waombolezaji walioshiriki maziko hayo yaliyofanywa kwa heshima zote za Kichama

Amelala mpiganaji wetu
Mungu ampe pumziko la amani
FB_IMG_16093186275531674.jpg
FB_IMG_16093186223620229.jpg
 
Kila Nafsi Itaonja Mauti Na Hakuna Atakayebakia Isipokuwa Allaah سبحانه وتعالى. Anasema Allaah سبحانه وتعالى: كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَما الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ...


"Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu."
 
Mtoa taarifa mbona unatoa taarifa kwa hofu kubwa Sana utafikiri Leo ndo watu wameanza kufa ghafla!

All in all Atangulie kwa amani sote ndo njia yetu twaja.
 
Back
Top Bottom