chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 12,000
- 20,653
Hii ni issue niliyoambiwa na mmoja ya waalimu wa chuo kikuu binafsi aliyekuwa anafundisha sheria. Aliingia chuo hicho (sikitaji) akiwa na bidii kubwa,. Anaingia Kila kipindi kwa wakati, anakuwa mkali pale wanafunzi wanapochelewa, na katika mtihani alikuwa hana mzaha.
Mmoja wa wanafunzi akamfuata, akamueleza kwamba yeye na wenzake wamechanga fungu nono la fedha ili awalegezee wafaulu vizuri. Akakataa, na akawanyoosha vizuri kwenye mtihani. Walichofanya lile fungu walilipeleka ngazi ya juu.
Ngazi ya juu wakamwita, wakamwambia kwamba wao biashara yao ni hao wanafunzi, anawafelisha halafu chuo kitoe wapi mapato? Akaambiwa awafaulishe au aache kazi. Jamaa akaacha kazi!
Kipindi hicho, chuo kikuu hicho lilikuwa kinatoa first class karibu darasa zima. Na ajira za vyeti, wakawa waaajiriwa kirahisi sana. Baadae waajiri wakaanza kuwalalamikia na kukataa kuwaita katika usaili.
Mwanachuo wa hivyo akutane na cream ya waalimu, wasiotaka Cha juu. Waalimu ambao serikali imewahakikishia mishahara, na chuo kinaendeshwa kwa fedha za serikali, hata kama akibaki mwanafunzi mmoja, chuo kinaenda.
Hivi tunasahau digrii za ngono mara hii? Digri za hivyo huwa zinakwama katika professional bodies kama Law School na Bodi ya uhasibu na kwingine.
Tuache maharage yarukeruke, ndio kuiva kwake! Waachie wachezee disco na supu, ndio wanaiva.