Yale yale ya kurekebisha ufaulu tutarajie wanafunzi 600 wa Law School wote kufaulu

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,074
Hakika hii Nchi ya Ajabu kabisa kila kitu ni Siasa.Wakati wa Utawala wa Awamu ya 4 kulitokea KUFELI kwa Wanafunzi wengi Badala ya Kutafuta sababu za Wanafunzi KUFELI kuna KIONGOZI MKUBWA aliagiza VIWANGO vya Wanafunzi waliofeli Waongezewe alama za Ufaulu na Matokeo yake Idadi ya Wanafunzi Waliofaulu ikaongezeka na TAIFA likafurahi kuwa na Waliofeli kuongezewa Alama.

Leo limejitokeza la LAW SCHOOL kwa kuwa Tunataka Wanafunzi Wafaulu kwa WINGI bila kujali Uwezo wao basi Tutarajie Wanafunzi 600 WATAFAULU ili TAIFA lifurahi.

Ninachoamini mimi kutokana na Wingi wa Vyuo binafsi vinavyofundisha SHERIA wanafunzi wanaojiunga na Vyuo hivyo wengi wao Waliopata Div 3 huchukuliwa na kujiunga na Vyuo je unatarajia nini kwa huyo Mwanafunzi wa Div 3 atakapofika LAW SCHOOL?

VYUO vingi vinashindwa kuwaandaa Wanafunzi wao ili waweze kufanya vizuri LAW SCHOOL

Pia kuna Changamoto kubwa ya LUGHA na hili hata JAJI MKUU aliwahi kulisemea.

Suala la Wanafunzi wa LAW SCHOOL KUFELI sio kwa TANZANIA bali ni kwa Nchi mbalimbali ikiwemo KENYA ZIMBABWE nk.

LAW SCHOOL Ni Chuo kigumu kutoka na Masomo yake Mwanafunzi asipoandaliwa Vizuri Chuoni alikotoka hakika HATOBOI LAW SCHOOL.
 
wanafunzi wanaojiunga na Vyuo hivyo wengi wao Waliopata Div 3 huchukuliwa na kujiunga na Vyuo je unatarajia nini kwa huyo Mwanafunzi wa Div 3 atakapofika LAW SCHOOL?
Mkuu hebu nipe mfano mmoja tu chuo kinachopokea div 3 mtu kusoma law. Ahsante.
 
600 wote mkuu lugha iwasumbie..!?
Ndani ya 600 humo wamo vichwa kweli kweli.
Na Kati ya 26 waliofauli 22 ni kutoka katika taasisi tofauti yani wanafunzi 4 pekee ndio wametoka vyuo vikuu..!?
Huoni hapo kuna cha kujiuliza..!?
Bora hata wangefaulu 90 atleast l,
Lakini piah ukiangalie tangu kuanzishwa hicho chuo kuna baadhi ya miaka walikuwa wanafaulu wanafunzi wengi tu.
 
Chuo chao kina shida mkubali ama mkatae haiwezekani wanafunzi 26 kati ya woooote , kuna tatizo mahala period msilete siasa hapa,
 
Unazungumzia wanafunzi 600 kwamba siyo rahisi wote kutojua Kiingereza?? Mimi nina uhakika hata wangekuwa 5000 bado Kiingereza ni shiidaa.
 
Chuo chao kina shida mkubali ama mkatae haiwezekani wanafunzi 26 kati ya woooote , kuna tatizo mahala period msilete siasa hapa,
Mkiwa vyuo vikuuu someni vijana, acheni janja janja hapaa.. Ukweli ni kwamba hamsomiii, library hamuendi, wengine hata thesis mnaandikiwa...
 
Waliosoma Law wote hawawezi kuwa Advocate likewise siyo wote waliosoma Accountancy wanapata CPA/ACCA. Wanasota.
 
Siasa haijawahi kusaidia zaidi ya kuharibu kwenye mambo ya kamati kama hya.
 
Sir robby
Nikupe kongole ndugu yangu kwa kuliangalia hili kwa jicho la tatu.

Hapa hata mim naona Kuna mkono wa siasa unataka kuingia kuvuruga mambo

Naamini kabisa hawataishia kuangalia upande wa changamoto zinazofanya wanafunzi na vijana wetu kufeli katika hivi vyuo.

kama vile panataka kutafutwa sababu yakuona Kuna makosa katika ufundishaji, utungaji, usimamizi na usahihishaji katika aina mbalimbali ya vipimo kwa Hawa wanafunzi.

Kuna baadhi ya watu wanasimamia ufanisi wa hizi taalum ili atakaetoka humo basi akawe competent kweli katika nafasi yake.

Hawa niwasimamizi na wafasili washeria na kanuni mbalimbali katika jamii na nchi,

Ndio wanaenda kuwa msaada mkubwa katika upande washeria ambayo imeonekana kuwa nichangamoto kubwa kwa raia walio wengi katika kuitafuta haki.

Iweje Sasa mtu wanamna hi asipikwe na akaiva, wataka tuwe na matapeli washeria wasiojua chcht isipokuwa tu kucertify vyeti na kuweka muhuri na saini zao kwenye mikataba yakuuziana viwanja na magari.

Hili haliwezekani kabisa, na usikute hapa Kuna viongozi au watoto wa viongozi wameguswa hapa ndo wanaamua kulivalia njuga kwa staili hii, niseme tu hapana

Low school imejipambanua yenyewe katika vision yake "the school intends to be excellence in practical legal training in East Africa and beyond" Sasa unadhani Ni namna gani wanaweza kufikia hi vision bila kusimamia hi taaluma ipaaavyo!?

Kama Kuna tume imeundwa juu yahili iende ikachunguze kinagaubaga kwa pande zote mbili na hasa kwahawa wanafunzi,

Wanafunzi wetu Sasa hivi wamekuwa mabarobaro hawataki kujiumiza kwenye masomo yao ili wawe Bora na badala yake wanazungukazunguka tu kututangazia Mimi Niko law school mwaka wa Kenda huu,

La maana hakuna leo wanafeli wanatafuta huruma ya namna hii kweliii!??

Kama Kuna Jambo baya haliwezi kuwa hili la miaka yote hapo ubaya uliopo Ni watu kusimamia ufanisi wataalum, tofauti na hapo hakuna!

Wanataka waandike report waseme "tume imeshauri zoezi lipitiwe upya na hivo inashauri kufutwa matokeo yaliyotolewa"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
600 wote mkuu lugha iwasumbie..!?
Ndani ya 600 humo wamo vichwa kweli kweli.
Na Kati ya 26 waliofauli 22 ni kutoka katika taasisi tofauti yani wanafunzi 4 pekee ndio wametoka vyuo vikuu..!?
Huoni hapo kuna cha kujiuliza..!?
Bora hata wangefaulu 90 atleast l,
Lakini piah ukiangalie tangu kuanzishwa hicho chuo kuna baadhi ya miaka walikuwa wanafaulu wanafunzi wengi tu.
kwani tangu kuanzishwa necta huwa hawafauru mbona 2014 walichemka hapo ujatoa hoja mkuu

kama toka vyuo vikuu ni wa 4 basi unakubaliana na mtoa bandiko kwamba vyuo vinazingua kuwaandaa vijana
 
Sir robby
Nikupe kongole ndugu yangu kwa kuliangalia hili kwa jicho la tatu.

Hapa hata mim naona Kuna mkono wa siasa unataka kuingia kuvuruga mambo

Naamini kabisa hawataishia kuangalia upande wa changamoto zinazofanya wanafunzi na vijana wetu kufeli katika hivi vyuo.

kama vile panataka kutafutwa sababu yakuona Kuna makosa katika ufundishaji, utungaji, usimamizi na usahihishaji katika aina mbalimbali ya vipimo kwa Hawa wanafunzi.

Kuna baadhi ya watu wanasimamia ufanisi wa hizi taalum ili atakaetoka humo basi akawe competent kweli katika nafasi yake.

Hawa niwasimamizi na wafasili washeria na kanuni mbalimbali katika jamii na nchi,

Ndio wanaenda kuwa msaada mkubwa katika upande washeria ambayo imeonekana kuwa nichangamoto kubwa kwa raia walio wengi katika kuitafuta haki.

Iweje Sasa mtu wanamna hi asipikwe na akaiva, wataka tuwe na matapeli washeria wasiojua chcht isipokuwa tu kucertify vyeti na kuweka muhuri na saini zao kwenye mikataba yakuuziana viwanja na magari.

Hili haliwezekani kabisa, na usikute hapa Kuna viongozi au watoto wa viongozi wameguswa hapa ndo wanaamua kulivalia njuga kwa staili hii, niseme tu hapana

Low school imejipambanua yenyewe katika vision yake "the school intends to be excellence in practical legal training in East Africa and beyond" Sasa unadhani Ni namna gani wanaweza kufikia hi vision bila kusimamia hi taaluma ipaaavyo!?

Kama Kuna tume imeundwa juu yahili iende ikachunguze kinagaubaga kwa pande zote mbili na hasa kwahawa wanafunzi,

Wanafunzi wetu Sasa hivi wamekuwa mabarobaro hawataki kujiumiza kwenye masomo yao ili wawe Bora na badala yake wanazungukazunguka tu kututangazia Mimi Niko law school mwaka wa Kenda huu,

La maana hakuna leo wanafeli wanatafuta huruma ya namna hii kweliii!??

Kama Kuna Jambo baya haliwezi kuwa hili la miaka yote hapo ubaya uliopo Ni watu kusimamia ufanisi wataalum, tofauti na hapo hakuna!

Wanataka waandike report waseme "tume imeshauri zoezi lipitiwe upya na hivo inashauri kufutwa matokeo yaliyotolewa"

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, kwanini haya malamiko yaje mwaka huu na sio mwaka jana au juzi? Matokea ya TSL yapoje kwa miaka 3 iliyopita?
 
Back
Top Bottom