EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,713
- 35,524
Kati ya wanafunzi 821 waliofanya wa kuhitimu kozi ya uwakili (stashahada ya juu ya sheria kwa vitendo) kutoka shule ya Sheria Tanzania (Law School of Tanzania), wamefaulu 23 tu ambao ni sawa na 2.8% huku 97.2% wakidaiwa kufeli.
Mwaka jana walifanya mtihani 633 wakafaulu 26 pekee sawa na 4.1%, hali iliyoibua malalamiko mengi kwa wadau wa elimu na kufanya Waziri wa Sheria na Katiba, @damasndumbaro_official kuunda Kamati ya uchunguzi.
Kamati hiyo iliyoongozwa na @harrisonmwakyembe iliwasilisha taarifa kuwa tatizo ni uwezo mdogo wa wanafunzi unaotokana na vyuo walivyosoma. Lakini matokeo ya mwaka huu yanaongeza tafakuri zaidi.
Kwanza Kamati ya Mwakyembe ililalamikiwa kuhoji walimu zaidi kuliko wanafunzi. Wanafunzi waliohojiwa ni wale tu waliopewa maelekezo na uongozi wa chuo (walipangwa). Haikufanyika rundom sampling. So inawezekana kuna matatizo mengi zaidi ya kile kilichoelezwa na Mwakyembe. Huwezi kufundisha darasa la watu 100 wakafaulu wawili tu, halafu ukajitetea eti ni uwezo mdogo wa wanafunzi. Kuna tatizo ambalo halitajwi. Uchunguzi zaidi unahitajika.!
:Malisa GJ