Emoj
JF-Expert Member
- Oct 9, 2015
- 838
- 1,302
Wapendwa natumaini valentine ilikuwa njema kwenu.
Kuna vitu ambavyo inatakiwa mvijadili na kukubaliana na mwenza wako kabla hamjaingia kwenye ndoa. Vitu kama Dini, mzae watoto wangapi, na sehemu ya kuishi vinapaswa mkubaliane kabla hamjaingia kwenye ndoa.
Ndoa nyingi mume na mke hawaelewani kwasababu kabla hawajaoana hawakukubaliana. Unakuta wameoana dini tofauti, hawajakubaliana kwamba yupi afate dini ya mwenzake au kila mtu abaki na dini yake, mwishowe wanajikuta wako ndani ya ndoa wanapishana kuhusu dini; huyu anataka hivi yule anataka vile.
Suala la mzae watoto wangapi yawapasa mlijadili kabla hamjaingia kwa ndoa ili kuepuka utata wa mume anataka watoto wanne mke anataka watoto wawili.
Suala la mtaishi wapi, nchi gani, mkoa gani yawapasa pia mlijadili kabla, maana mnaweza ingia kwa ndoa mkashindwa kuelewana mnaishi wapi, mume anataka muishi Dar mke anataka muishi Mbeya.
Kwa mnaoingia kwenye ndoa masuala ya Dini, watoto na makazi, yawapasa muyajadili kabla ya ndoa.