Kabila la Kiiraqw laweza kupotea kabisa Tanzania

hawawezi kupotea wairaqw Taifa kubwa labda wewe uliyepost ni mnyatturu au mmasai.Wamasai ndo waka katika hatari ya kutoweka maana wamejazana mijini wakilinda nyumba za watu

tuache kudanganyana, taifa kubwa mtakuwa wairaqw? labda kwa uvivu, umalaya, na ushamba. Kila mahali nyumba ya wageni kwanini ? hafu guest house zenyewe za chap chap! du mnatisha.
 
Kuna uwezekano mkubwa wa kabila la Kiiraqw lilopo mkoa wa manyara kupotea kabisa au asili ya watu hawa kupotea kabisa siku za mbeleni. na hasa ukizingatia na udogo wa kabila lenyewe. Hii ni kutokana na sheria zao kali za kimila zinazoweka mazingira magumu sana ya wenyewe kwa wenyewe kuoana na kusababisha asilimia kubwa ya watu kulazimika kuoa au kuolewa na makabila mengine, sisemi kama kuna ubaya kuoa au kuolewa na makabila mengine. Katika hili kabila kuna kitu kinaitwa DAWI, maana ya DAWI ni uhusiano wa kikoo au kidamu kati ya watu wawili, hata kama ni kitukuu wa kitukuu ambaye Bibi yake ni ukoo wako basi huwezi kumuoa au kuolewa naye kwasababu atakuwa ni DAWI yako. Sasa kutokana na udogo wa hili kabila vijana wengi walioanzisha uhusiano wamejikuta wameingia kwenye huo mtego na kushindwa kuoana.

Tuepuke - 'Irange'
 
Herufi huwa zinawakilisha sauti. Kwa hiyo hata kama hakuna herufi 'Q' sauti zinazotumia kaakaa laini zinawakilishwa
na herufi zipi kama sio X,Q, /? Jifunza elimu ya fonolojia kabla ya kuanddika.[/QUOTE
Mi naongelea maandishi ya kiswahili hakuna Q,sijaongelea matamshi.
 
Historia ya chimbuko, mila na desturi za kabila la WAIRAQW
Utangulizi
Wairaqw ni miongoni mwa rnakabila yanayoishi katika Mkoa wa Manyara Wilaya za
Mbulu, Babati, Hanang na Mkoa wa Arusha Wiiaya ya Karatu.
Asili ya kabila la WAIRAQW
Kwa asili Wairaqw walitokea Mesopotamia Iraq. Uhamiaji wao ulianza katika karne ya 4 - 6
baada ya kuzaliwa kwa Kristo. Wairaqw ni jamii ya Wakushi ambao Walivuka bahari ya
Sham kwa mashua na kutua Ethiopia, waliishi hapo kwa muda kutokana na vita vya mara kwa
mara, waiiendelea kuhama kuelekea kusini magharibi waiipitia bonde la ufa kando ya
ziwa Victoria. Katika kuhama hama huko na kukaa mahali kwa muda vita
vikaanza wakakimbilia na waiiendelea hivyo hivyo kupitia njia ya kati kupitia Singida Iramba
hadi mpakani mwa Dodoma na Iringa. Kwa upande wa kusini kuiikuwa na
mapambano ya Wahehe, Wangoni na Wazimba wakarejea kuelekea kaskazini hadi
sehemu ya Kondoa mahali panapoitwa Guser Tuwalay. Waliishi hapo wakiwa wafugaji
na kilimo kidogo. Ndipo walipoanza mapambano kati yao na Wabarbaig. Waliposhindwa
vita walikirnbilia karibu na mlima Hanang. Wakagawanyika wengine wakaelekea,
Gallapo (Tsea Daaw). Hawa waliitwa Wagorowa na Wairaqw walipandisha mlima Dabil
hadi Guser, Gangaru ambapo walifanya maskani.
Baada ya muda Kiongozi wao aiiyeitwa Haymu Now wa ukoo wa Haytipe aliwaongoza hadi
Nou na walifanya rnaskani yao katika maeneo ya Mama Isara. Aidha inasemakana kuwa eneo
lote la Mama Isara lilikuwa ni ziwa wakati ule, hivyo Haymu na watu wake walifanya maskani
katika maeneo ya milima.
Kiongozi huyo alikuwa na mtumishi wake aiiyeitwa MOYA. Hi kuongeza maeneo ya kilimo
kiongozi huyo alitumia uganga wake kuhamisha ziwa katika eneo la Mama Isara kwa
kumwagiza mtumishi wake kurusha mshale katikati ya ziwa hilo. mtumishi alipofanya hivyo
ziwa lilihama pamoja naye hadi katika bonde la ufa ambalo linajulikana kwa jina la ziwa
manyara kwa sasa na Kiiraqw hujulikana kama "Tlawta Moya".
Baada ya ziwa kuhama kiongozi huyo aliendelea kuishi hapo na watu wake na kuendelea
kutawanyika katika maeneo ya Muray, Kuta, Amoa, Kainam, Suum, Datlaa, Tsaayo Wilaya ya
Mbulu.
Baadaye Wairaqw wakatawanyika taratibu sehemu za Karatu, Babati na Hanang kama makao
makuu yao mpaka leo. Baadhi ya miia na desturi za Wairaqw zinafanana na za Wayahudi
kama matumizi ya kondoo katika jamii.
Chakula cha asili cha WAIRAQW
Chakula chao kikuu kilikuwa nyama ya wanyamapori na ya mifugo waliyofuga. Walichuna
nyama kwa kutumia mawe yenye ncha kali mithili ya kisu. Mapishi yao yalitokana na moto
unaopatikana kwa njia ya kupekecha mti hadi moto unatokea, chombo hicho kiliitwa (Bui na
Daha). Baadaye waligundua mazao aina ya mtama, ulezi, uwele na mboga yao ilikuwa kunde.
Nafaka hiyo ilisagwa kwa kutumia jiwe la mkono na unga uliopatikana ulitumika kupikia
ugali mlaini (Xwante) unaofanana na uji uliopoa. Nafaka hiyo pia hutumika kutengenezea
pombe ya asili ambayo ilinyweka kama viburudisho wakati wa sherehe mbalimbali za kimila.
http://www.safarilands.org/
Michezo ya asili
Wairaqw walikuwa na ngoma aina mbili:-
1. Ngoma ya ndani yaani ya harusi. Ngoma hii huchezwa siku mtoto wa
kike anapoolewa au wa kiume anapooa.
2. ngoma ya nje ya mwaka wakati wa mavuno huitwa "Gilo". Ngoma hii huchezwa wakati wa
mavuno kama ishara ya furaha na shukrani kwa Mungu.
Nyimbo ya "Mudeli" huimbwa wakati wa harusi kwa kumpongeza bwana harusi na bibi harusi,
na nyimbo hizp huimbwa na akina mama.
Wakati wa kuweka sherehe ya shukrani kwa mwaka, Wairaqw wana utaratibu wa maombi
yaani inaitwa "slufay" pamoja na "Giriyda". Giriyda hi nyimbo maalum ya kuomba mambo
rnazuri na kuepusha mambo mabaya.
Nyimbo maarufu kwa akina mama inaitwa "sibeli" ni nyimbo ya shukrani kwa
Mungu.
Mavazi
Mavazi ya asili ya Wairaqw ni ngozi. Ngozi hizo zililainishwa vizuri na kushonwa mithili ya
shuka, sketi au kanga. Vazi la kiume lilikuwa moja ambalo lilifunikwa kama shuka. Vazi la
kike lilikuwa sketi na shuka ndogo iliyofanana na kanga. Pia wanaume na wanawake walivaa
viatu vilivyotengenezwa na ngozi.
Uchumi wa jadi ya WAIRAQW
Uchurni wa jadi wa Wairaqw ulikuwa ufugaji, kilimo, na utengenezaji wa zana mbalimbali za
kilimo na ulinzi. Hapakuwa na biashara ya fedha taslimu ila ilikuwa kubadilishana mali au
mifugo kwa vifaa au zana.
Zana za kilimo
Majembe ya asili yalitengenezwa kwa kutumia miti iliyochongwa kama mithili ya jembe.
Majembe hayo yalitumika kulimia na kushindilia udongo juu ya nyumba ya Tembe. Jembe hilo
liliitwa "Taqhwani", pia kwa ajili ya kutindua shamba jipya walitumia chimbuo
lililotengenezwa na miti migumu na ilichongwa upande mmoja mithili ya chimbuo. Jembe hilo
liliitwa 'Dughsay". Baadaye waligundua zana zilizotengenezwa kwa udongo wa mfmyanzi
uliotoka Mbugwe. Zana hizo zilitumika hadi majembe ya mkono yalipopatikana kutoka kwa
wataalam wa nje.
Zana za vita na uwindaji
Mikuki na mishale ya asili ilitengenezwa na miti iliyochongwa mfano wa mkuki wa chuma
unaotumika sasa. Pia walitumia mawe yenye ncha kali na baadaye waligundua zana
zinazotengenezwa kwa kuturnia udongo wa mfinyanzi ambazo zilikaushwa kwa moto mkali
kama tofali.
Hifadhi ya nafaka
Walipovuna walikuwa na utaratibu wa kuweka mazao yao kwenye ghala zao za asili (kuntay)
zilizotengenezwa kwa vinyesi vya ng'ombe. Pia aina ya majani ya miti ya asili na majivu ya
vinyesi vya ng'ombe vilitumika katika kuhifadhi nafaka kutokana na kushambuliwa na
wadudu. Majivu ya majani hayo yalichanganywa na nafaka mithili ya dawa zinazotumika sasa.
http://www.safarilands.org/
Utawala/uongozi
Walikuwa na uongozi toka ngazi ya familia, ukoo, jamii ya kabila zima la Wairaqw
waliotawaliwa na Kahamusmo ambaye ni kiongozi mkuu wao. Kiongozi msaidizi anaitwa
Yaabusmo. Kila mmoja anafanya kazi kwa nafasi yake. Kwa ujumla ni kabila linalopenda
kushirikiana katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa; "Walikuwa na waganga wa kiasili
waliojulikana kwa majina kwa jamii nzima.
Malezi ya mtoto wa kike na kiume wa KIIRAQW
Mtoto wa kike na wa kiume wa Kiiraqw anapozaliwa na kukua hufundishwa maadili mema ya
kuishi na jamii. Mtoto wa kike hufundishwa na akina mama maadili mema ya kuishi na nume
na namna ya kutunza familia anapoolewa na kuzaa. Mtoto wa kiume hufundishwa na akina
baba maadili ya kuishi na jamii, mbinu za kujitegemea katika kutunza familia anapokuwa
ameoa.
Elimu
Wairaqw wa asili hawakupenda kuwasomesha watoto wao wakidai kuwa wakipata elimu
watapotoka au mila zao zingepotea. Pia waliwazuja watoto kwenda shule kwa ajili ya kufanya
kazi za nyumbani kama vile kucunga mifugo hasa kwa watoto wa kiume. Kwa watoto wa kike
waliwazuia kwenda shule ili waolewe na wapate mali (mahari).
Mahakama ya jadi za WAIRAQW
Adhabu zilitolewa kwa taratibu za mila kwa kuzingatia kosa alilotenda mhalifu. Masuala ya
makosa yote yaliyotoka katika jamii hujadiliwa na wazee wa jinsia tofauti yaani wanaume na
wanawake na kutolewa uamuzi. Pia fursa Hitolewa kwa masuala yaliyohusu kesi ya jinsia
moja kujadiiiwa na wazee wa jinsia hiyo kwanza ili hatimaye adhabu itolewe na jamii nzima.
Watuhumiwa waliopatikana na makosa yaliyothibitika walitozwa faini ya kimila iliyoitwa
"Dohho" au waliagizwa kulipa fidia kwa mlalamikaji. Watuhumiwa waliokana mashtaka hata
kama kuna ushahidi walipewa adhabu ya kutengea na jamii nzima. Pia kwa kesi ambazo hazina
ushahidi mlalamikaji na mlalamikiwa waliapishwa kwa yote aliyoeleza ni sahihi na laana
ilitolewa kwa aliyesema uongo fotauti na hali halisi.
Tiba za asili
Wairaqw walitumia mizizi na majani ya miti kama tiba ya magonjwa mbalimbali. Mizizi hiyo
ilichemshwa au kusagwa na kuchanganywa na maji na kupewa wagonjwa.
- mwisho -
historia hh ya wairaq meandaliwa na
kamati ya tamasha ya utamaduniwa jame ya
Wairaqw na Wagorowa - wilaya ya Babati,
 
Hatupotei,tatizo ni kwamba watu mnadharau tamaduni za wenzenu kumbukeni kwamba rev dr j.sulivan once said 'the person of no culture is the person of no belonging'
 
Herufi huwa zinawakilisha sauti. Kwa hiyo hata kama hakuna herufi 'Q' sauti zinazotumia kaakaa laini zinawakilishwa
na herufi zipi kama sio X,Q, /? Jifunza elimu ya fonolojia kabla ya kuanddika.[/QUOTE
Mi naongelea maandishi ya kiswahili hakuna Q,sijaongelea matamshi.

Kama ni maandishi ya Kiswahili ni sawa hakuna konsonanti Q wala X lakini kwa Kiiraqw na lugha ambazo siyo za kiBantu hizo zinatumika.
 
Hii sijui imetoka wapi?

Ifahamike kama ifuatavyo:

Haymu Tipe a.k.a. Irqwatu Bonday ni wa Ukoo wa Hhay-Naman na Moya ni mpwa wake na wala siyo mtumi.

Hakuna ngoma inayoitwa Gilo. Gilo do Nato Awe ni wimbo.

Sibeli ni wimbo wa mahafali wakati wasichana wanapotoka unyagoni (marmo) na hata hivyo baadaye ulitumika kama wimbo wa wasichana wakati wa sherehe zao.
 
Kuna uwezekano mkubwa wa kabila la Kiiraqw lilopo mkoa wa manyara kupotea kabisa au asili ya watu hawa kupotea kabisa siku za mbeleni. na hasa ukizingatia na udogo wa kabila lenyewe. Hii ni kutokana na sheria zao kali za kimila zinazoweka mazingira magumu sana ya wenyewe kwa wenyewe kuoana na kusababisha asilimia kubwa ya watu kulazimika kuoa au kuolewa na makabila mengine, sisemi kama kuna ubaya kuoa au kuolewa na makabila mengine. Katika hili kabila kuna kitu kinaitwa DAWI, maana ya DAWI ni uhusiano wa kikoo au kidamu kati ya watu wawili, hata kama ni kitukuu wa kitukuu ambaye Bibi yake ni ukoo wako basi huwezi kumuoa au kuolewa naye kwasababu atakuwa ni DAWI yako. Sasa kutokana na udogo wa hili kabila vijana wengi walioanzisha uhusiano wamejikuta wameingia kwenye huo mtego na kushindwa kuoana.

hapa ndio utaona umuhimu wa data za makabila na dini katika sensa, otherwise kama sio muhimu tun aweza kusema wacha lipoteee tu kabila hilo watanzania hatujinasib na makabila ama dini!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 
Hakuna mtu mwenye asili ya Tanzania. Wairaqw wanaaminika ndio waliohamia East Africa mapema zaidi kuliko makabila mengine ya Kibantu na nilotes na kwamba waliwakuta Bushmen(Khoisan speaking tribes like Hadza and tsandawe). For your information, Tanzania (mainly Manyara Region) is the only place in the continent where the four major African language families - Bantu, Khoisan, Cushitic, and Nilotic - occur together. Iraqw is the only tribe of Cushitic origin in the region as they grew totally isolated from their original Cushitic cluster who settled in Horn of Africa and southern Kenya. By no means kabila hili itakuja potea if it survived for so long...

Thank you for a nice brief with sound facts. It is indeed an educative script!!!!!!!!
 
wairaq ni wengi sana kwa sasa mku na hiyo hoja yako ya daawi ina mwisho wake generation 3 generation ya 4 inaruhusiwa. Wazee wa kiirak ni makini sana na hilo la close relationship of blood ina matatizo yake ambayo genetic inheritance imesaidia sana kupunguza matatizo mfano ALBINO kule kumpata albino ni ishu waulize je kuna ukweli huo au lahh! wataalamu watatusaidia mana mimi nimeliona ingawa sina uthibitishso sahihi wa kisayansi
 
Historia ya chimbuko, mila na desturi za kabila la WAIRAQWUtanguliziWairaqw ni miongoni mwa rnakabila yanayoishi katika Mkoa wa Manyara Wilaya zaMbulu, Babati, Hanang na Mkoa wa Arusha Wiiaya ya Karatu.Asili ya kabila la WAIRAQWKwa asili Wairaqw walitokea Mesopotamia Iraq. Uhamiaji wao ulianza katika karne ya 4 - 6baada ya kuzaliwa kwa Kristo. Wairaqw ni jamii ya Wakushi ambao Walivuka bahari yaSham kwa mashua na kutua Ethiopia, waliishi hapo kwa muda kutokana na vita vya mara kwamara, waiiendelea kuhama kuelekea kusini magharibi waiipitia bonde la ufa kando yaziwa Victoria. Katika kuhama hama huko na kukaa mahali kwa muda vitavikaanza wakakimbilia na waiiendelea hivyo hivyo kupitia njia ya kati kupitia Singida Irambahadi mpakani mwa Dodoma na Iringa. Kwa upande wa kusini kuiikuwa namapambano ya Wahehe, Wangoni na Wazimba wakarejea kuelekea kaskazini hadisehemu ya Kondoa mahali panapoitwa Guser Tuwalay. Waliishi hapo wakiwa wafugajina kilimo kidogo. Ndipo walipoanza mapambano kati yao na Wabarbaig. Waliposhindwavita walikirnbilia karibu na mlima Hanang. Wakagawanyika wengine wakaelekea,Gallapo (Tsea Daaw). Hawa waliitwa Wagorowa na Wairaqw walipandisha mlima Dabilhadi Guser, Gangaru ambapo walifanya maskani.Baada ya muda Kiongozi wao aiiyeitwa Haymu Now wa ukoo wa Haytipe aliwaongoza hadiNou na walifanya rnaskani yao katika maeneo ya Mama Isara. Aidha inasemakana kuwa eneolote la Mama Isara lilikuwa ni ziwa wakati ule, hivyo Haymu na watu wake walifanya maskanikatika maeneo ya milima.Kiongozi huyo alikuwa na mtumishi wake aiiyeitwa MOYA. Hi kuongeza maeneo ya kilimokiongozi huyo alitumia uganga wake kuhamisha ziwa katika eneo la Mama Isara kwakumwagiza mtumishi wake kurusha mshale katikati ya ziwa hilo. mtumishi alipofanya hivyoziwa lilihama pamoja naye hadi katika bonde la ufa ambalo linajulikana kwa jina la ziwamanyara kwa sasa na Kiiraqw hujulikana kama "Tlawta Moya".Baada ya ziwa kuhama kiongozi huyo aliendelea kuishi hapo na watu wake na kuendeleakutawanyika katika maeneo ya Muray, Kuta, Amoa, Kainam, Suum, Datlaa, Tsaayo Wilaya yaMbulu.Baadaye Wairaqw wakatawanyika taratibu sehemu za Karatu, Babati na Hanang kama makaomakuu yao mpaka leo. Baadhi ya miia na desturi za Wairaqw zinafanana na za Wayahudikama matumizi ya kondoo katika jamii.Chakula cha asili cha WAIRAQWChakula chao kikuu kilikuwa nyama ya wanyamapori na ya mifugo waliyofuga. Walichunanyama kwa kutumia mawe yenye ncha kali mithili ya kisu. Mapishi yao yalitokana na motounaopatikana kwa njia ya kupekecha mti hadi moto unatokea, chombo hicho kiliitwa (Bui naDaha). Baadaye waligundua mazao aina ya mtama, ulezi, uwele na mboga yao ilikuwa kunde.Nafaka hiyo ilisagwa kwa kutumia jiwe la mkono na unga uliopatikana ulitumika kupikiaugali mlaini (Xwante) unaofanana na uji uliopoa. Nafaka hiyo pia hutumika kutengenezeapombe ya asili ambayo ilinyweka kama viburudisho wakati wa sherehe mbalimbali za kimila.http://www.safarilands.org/Michezo ya asiliWairaqw walikuwa na ngoma aina mbili:-1. Ngoma ya ndani yaani ya harusi. Ngoma hii huchezwa siku mtoto wakike anapoolewa au wa kiume anapooa.2. ngoma ya nje ya mwaka wakati wa mavuno huitwa "Gilo". Ngoma hii huchezwa wakati wamavuno kama ishara ya furaha na shukrani kwa Mungu.Nyimbo ya "Mudeli" huimbwa wakati wa harusi kwa kumpongeza bwana harusi na bibi harusi,na nyimbo hizp huimbwa na akina mama.Wakati wa kuweka sherehe ya shukrani kwa mwaka, Wairaqw wana utaratibu wa maombiyaani inaitwa "slufay" pamoja na "Giriyda". Giriyda hi nyimbo maalum ya kuomba mambornazuri na kuepusha mambo mabaya.Nyimbo maarufu kwa akina mama inaitwa "sibeli" ni nyimbo ya shukrani kwaMungu.MavaziMavazi ya asili ya Wairaqw ni ngozi. Ngozi hizo zililainishwa vizuri na kushonwa mithili yashuka, sketi au kanga. Vazi la kiume lilikuwa moja ambalo lilifunikwa kama shuka. Vazi lakike lilikuwa sketi na shuka ndogo iliyofanana na kanga. Pia wanaume na wanawake walivaaviatu vilivyotengenezwa na ngozi.Uchumi wa jadi ya WAIRAQWUchurni wa jadi wa Wairaqw ulikuwa ufugaji, kilimo, na utengenezaji wa zana mbalimbali zakilimo na ulinzi. Hapakuwa na biashara ya fedha taslimu ila ilikuwa kubadilishana mali aumifugo kwa vifaa au zana.Zana za kilimoMajembe ya asili yalitengenezwa kwa kutumia miti iliyochongwa kama mithili ya jembe.Majembe hayo yalitumika kulimia na kushindilia udongo juu ya nyumba ya Tembe. Jembe hiloliliitwa "Taqhwani", pia kwa ajili ya kutindua shamba jipya walitumia chimbuolililotengenezwa na miti migumu na ilichongwa upande mmoja mithili ya chimbuo. Jembe hiloliliitwa 'Dughsay". Baadaye waligundua zana zilizotengenezwa kwa udongo wa mfmyanziuliotoka Mbugwe. Zana hizo zilitumika hadi majembe ya mkono yalipopatikana kutoka kwawataalam wa nje.Zana za vita na uwindajiMikuki na mishale ya asili ilitengenezwa na miti iliyochongwa mfano wa mkuki wa chumaunaotumika sasa. Pia walitumia mawe yenye ncha kali na baadaye waligundua zanazinazotengenezwa kwa kuturnia udongo wa mfinyanzi ambazo zilikaushwa kwa moto mkalikama tofali.Hifadhi ya nafakaWalipovuna walikuwa na utaratibu wa kuweka mazao yao kwenye ghala zao za asili (kuntay)zilizotengenezwa kwa vinyesi vya ng'ombe. Pia aina ya majani ya miti ya asili na majivu yavinyesi vya ng'ombe vilitumika katika kuhifadhi nafaka kutokana na kushambuliwa nawadudu. Majivu ya majani hayo yalichanganywa na nafaka mithili ya dawa zinazotumika sasa.http://www.safarilands.org/Utawala/uongoziWalikuwa na uongozi toka ngazi ya familia, ukoo, jamii ya kabila zima la Wairaqwwaliotawaliwa na Kahamusmo ambaye ni kiongozi mkuu wao. Kiongozi msaidizi anaitwaYaabusmo. Kila mmoja anafanya kazi kwa nafasi yake. Kwa ujumla ni kabila linalopendakushirikiana katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa; "Walikuwa na waganga wa kiasiliwaliojulikana kwa majina kwa jamii nzima.Malezi ya mtoto wa kike na kiume wa KIIRAQWMtoto wa kike na wa kiume wa Kiiraqw anapozaliwa na kukua hufundishwa maadili mema yakuishi na jamii. Mtoto wa kike hufundishwa na akina mama maadili mema ya kuishi na numena namna ya kutunza familia anapoolewa na kuzaa. Mtoto wa kiume hufundishwa na akinababa maadili ya kuishi na jamii, mbinu za kujitegemea katika kutunza familia anapokuwaameoa.ElimuWairaqw wa asili hawakupenda kuwasomesha watoto wao wakidai kuwa wakipata elimuwatapotoka au mila zao zingepotea. Pia waliwazuja watoto kwenda shule kwa ajili ya kufanyakazi za nyumbani kama vile kucunga mifugo hasa kwa watoto wa kiume. Kwa watoto wa kikewaliwazuia kwenda shule ili waolewe na wapate mali (mahari).Mahakama ya jadi za WAIRAQWAdhabu zilitolewa kwa taratibu za mila kwa kuzingatia kosa alilotenda mhalifu. Masuala yamakosa yote yaliyotoka katika jamii hujadiliwa na wazee wa jinsia tofauti yaani wanaume nawanawake na kutolewa uamuzi. Pia fursa Hitolewa kwa masuala yaliyohusu kesi ya jinsiamoja kujadiiiwa na wazee wa jinsia hiyo kwanza ili hatimaye adhabu itolewe na jamii nzima.Watuhumiwa waliopatikana na makosa yaliyothibitika walitozwa faini ya kimila iliyoitwa"Dohho" au waliagizwa kulipa fidia kwa mlalamikaji. Watuhumiwa waliokana mashtaka hatakama kuna ushahidi walipewa adhabu ya kutengea na jamii nzima. Pia kwa kesi ambazo hazinaushahidi mlalamikaji na mlalamikiwa waliapishwa kwa yote aliyoeleza ni sahihi na laanailitolewa kwa aliyesema uongo fotauti na hali halisi.Tiba za asiliWairaqw walitumia mizizi na majani ya miti kama tiba ya magonjwa mbalimbali. Mizizi hiyoilichemshwa au kusagwa na kuchanganywa na maji na kupewa wagonjwa.- mwisho -historia hh ya wairaq meandaliwa nakamati ya tamasha ya utamaduniwa jame yaWairaqw na Wagorowa - wilaya ya Babati,
kuhusu elimu sio kweli ila mwirak kitu ambayo hapendi ni kule mtoto amefeli amlazimishe kusoma.
 
By malema 1989 tuache kudanganyana, taifa kubwa mtakuwa wairaqw? labda kwa uvivu, umalaya, na ushamba. Kila mahali nyumba ya wageni kwanini ? hafu guest house zenyewe za chap chap! du mnatisha. Wew unaongea upuuzii sana nenda mbulu , babati ujue shule za kata zilianza lini na kilimo cha kutumia wanyama imeanza lini.Watu hawa huwajui kabisa wewe hakuna wachapa kazi kama wairaq na hawapendi longolongo.
 
Back
Top Bottom