Kabila la Kiiraqw laweza kupotea kabisa Tanzania

BIG X

JF-Expert Member
Nov 4, 2011
777
212
Kuna uwezekano mkubwa wa kabila la Kiiraqw lilopo mkoa wa Manyara kupotea kabisa au asili ya watu hawa kupotea kabisa siku za mbeleni na hasa ukizingatia na udogo wa kabila lenyewe.

Hii ni kutokana na sheria zao kali za kimila zinazoweka mazingira magumu sana ya wenyewe kwa wenyewe kuoana na kusababisha asilimia kubwa ya watu kulazimika kuoa au kuolewa na makabila mengine, sisemi kama kuna ubaya kuoa au kuolewa na makabila mengine.

Katika hili kabila kuna kitu kinaitwa DAWI, maana ya DAWI ni uhusiano wa kikoo au kidamu kati ya watu wawili, hata kama ni kitukuu wa kitukuu ambaye Bibi yake ni ukoo wako basi huwezi kumuoa au kuolewa naye kwasababu atakuwa ni DAWI yako.

Sasa kutokana na udogo wa hili kabila vijana wengi walioanzisha uhusiano wamejikuta wameingia kwenye huo mtego na kushindwa kuoana.
 
Mkuu, je una uchunguzi au taarifa yoyote ya kisayansi zikiwemo takwimu, kuthibitisha madai yako?
 
Ni kweli kabisa Mkuu DA'AWI inatutafuna vibaya, Ukiacha kabila kupotea, Ukweli ni kwamba Asili au tamaduni zimeshapotea, Maeneo mengi vijana wamechanganyika sana, ni sehemu chache sana ambazo bado wanaheshimu mila na tamaduni. Sehemu kama Iriqwada'au kule milimani maeneo ya Mbulu ni kati ya sehemu chache ambazo bado hazijaharibika. Kuhusu DA'AWI ngoja tuwasubiri akina Afrodenzi, dena Amsi na wengine watueleze vizuri.
 
Issue ya kuchunguza daawi wakati wa mchakato wa ndoa ipo ila cricital follow-up ya family trees za kila upande imepunga nowadays. Pia kuna faini huwa inaweza kulipwa kama kuna kauhusiano baina ya wachumba.
Suala la utunzaji wa mila na tamaduni nzuri ni tatizo kwa kabila la wairaqw.
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na sababu hiyo, kabila la ki-Iraqw ni wengi sidhani kama litapotea. Ukianzia Karatu, Daudi, Masieda, Bargish antsi, Arri, Mbulu mjini, Anslay, Gehandu, Gedamar, Titiwi, Kwermusl, Khaday, Kainamu, Nahasey, Tsaayo-raat, Hayloto, Murray, Qwam, Kuta, Siday, Tlawi, Masqaroda, Diyomati, Bashay, Dongobesh, Tumati, Mongahay, Endoji, Bashnet, Gidhim, Maretadu, Gibdiyo, Gidmadoy, Gidarudadaw, Simhha, Haydrer, Semonyandi, Mewadani, Musru, Endagikot, Endaharghadakt, Endamasaki, Endamilay, Endanachan, Endanyawish, Erboshan, Ngw’andakw, Yarotamburda, Qatabella, Qamatananat, Qambush, Datlaa, Dumanangw, Endagew, Muguruchan, Maghang, Haydom mpaka kule Murkuchida ni wao tu. Pia kule Yaeda chini na Mungowamono kwa Wahadzabe wapo wachache.
 
umetiiiiiiiiiiiishaaa !!
 
its historical fact hizi makabila zetu hazikuwepo 1000 year ago na for sure haztakuwepo just 200 year to come. unajua miaka 500 ilopita hakukua na makabila yafuatao katika aridh inayoitwa tz leo. maasai waarusha taturu sukuma hakua moja, ngoni ilikua sehemu ya zulu ama ndebele, kara kisiwa chao kilikua tupu. nk
 
hawawezi kupotea wairaqw Taifa kubwa labda wewe uliyepost ni mnyatturu au mmasai.Wamasai ndo waka katika hatari ya kutoweka maana wamejazana mijini wakilinda nyumba za watu
 
Hivi jamani Wairaq si ndio hao hao Wambulu? Yaani akina Slaa. Nadhani kuna mambo wanayotofautiana kutokana na upande wanaotoka au imani kalina lugha yao ni moja, hebu nielewesheni!
 
hivi jamani wairaq si ndio hao hao wambulu? Yaani akina slaa. Nadhani kuna mambo wanayotofautiana kutokana na upande wanaotoka au imani kalina lugha yao ni moja, hebu nielewesheni!
kwa taarifa yako wairaq ndo hao wambulu haswaa. Sasabu ya neno wambulu kutumiwa zaidi kumaanisha wairaq ni kwa kuwa kwa asili wairaq wengi walianzia wilaya ya mbulu wakatanauka kwenda karatu ambayo zamani ilikuwa ni pati ya mbulu wengine wakaingia kidogo kateshi na wengine babati!

hivi jamani wairaq si ndio hao hao wambulu? Yaani akina slaa. Nadhani kuna mambo wanayotofautiana kutokana na upande wanaotoka au imani kalina lugha yao ni moja, hebu nielewesheni!

kwa taarifa wambulu ndo wairaq!!! Sababu ya neno wambulu kutumika zaidi ni kwa kuwa zamani ilikuwa mbulu inajumuisha eneo lote la mbulu karatu some parts of babati na some parts of katesh...na kabila lililokuwepo ni wa iraq,sasa kutokana na wairaq kuenea sana eneo lote la mbulu basi watu wakawaita wambulu!!!
 
Kuna uwezekano mkubwa wa kabila la Kiiraqw lilopo mkoa wa manyara kupotea kabisa au asili ya watu hawa kupotea kabisa siku za mbeleni. na hasa ukizingatia na udogo wa kabila lenyewe. Hii ni kutokana na sheria zao kali za kimila zinazoweka mazingira magumu sana ya wenyewe kwa wenyewe kuoana na kusababisha asilimia kubwa ya watu kulazimika kuoa au kuolewa na makabila mengine, sisemi kama kuna ubaya kuoa au kuolewa na makabila mengine. Katika hili kabila kuna kitu kinaitwa DAWI, maana ya DAWI ni uhusiano wa kikoo au kidamu kati ya watu wawili, hata kama ni kitukuu wa kitukuu ambaye Bibi yake ni ukoo wako basi huwezi kumuoa au kuolewa naye kwasababu atakuwa ni DAWI yako. Sasa kutokana na udogo wa hili kabila vijana wengi walioanzisha uhusiano wamejikuta wameingia kwenye huo mtego na kushindwa kuoana.

Inavyoonekana wewe unataka kupuuza hilo sharti la kutokoa DA'AWI (iwe haiwarasu au hatikar qaramba )na unataka kuiingiza jamii kwenye IRINGE (incest). Inabidi uwe mwangalifu kama unataka kumwoa/kujenga urafiki na mtu ambaye una uhusiano naye.
 
Pamoja na sababu hiyo, kabila la ki-Iraqw ni wengi sidhani kama litapotea. Ukianzia Karatu, Daudi, Masieda, Bargish antsi, Arri, Mbulu mjini, Anslay, Gehandu, Gedamar, Titiwi, Kwermusl, Khaday, Kainamu, Nahasey, Tsaayo-raat, Hayloto, Murray, Qwam, Kuta, Siday, Tlawi, Masqaroda, Diyomati, Bashay, Dongobesh, Tumati, Mongahay, Endoji, Bashnet, Gidhim, Maretadu, Gibdiyo, Gidmadoy, Gidarudadaw, Simhha, Haydrer, Semonyandi, Mewadani, Musru, Endagikot, Endaharghadakt, Endamasaki, Endamilay, Endanachan, Endanyawish, Erboshan, Ngw'andakw, Yarotamburda, Qatabella, Qamatananat, Qambush, Datlaa, Dumanangw, Endagew, Muguruchan, Maghang, Haydom mpaka kule Murkuchida ni wao tu. Pia kule Yaeda chini na Mungowamono kwa Wahadzabe wapo wachache.

Uendelee hadi Endalaqanet,Dareda, Maganjwa, Masqaroda, Gudedesh, Endasak, Nangwa, Giting, Sabilo, Basoduqwang, Endagaw,Sigino..............
 
Back
Top Bottom