Kabila la Kiiraqw laweza kupotea kabisa Tanzania

looohhh we Duduwasha wewe.
itabidi tukutane tuongee vizuri kabla hujapandisha BP na mi kumbe dada ako.

PS. Nashukuru kusikia umejifunza kitu kwenye ile web.
Haha your make me Happy... Afrodenzi... Me nipo Tayari kukutana Siku yoyote... wewe tu nimesha jituliza BP isipande.... i hope your well too... Nimejifunza Mengi Kule Ohayoda bado kujifunza Mengi kutoka kwako pia:teeth:
A%20S-rose.gif
 
Kabila la Wairaqw linatokana na mbari (race) ya Caucasoid kama yalivyo mataifa ya Ulaya. Ndiyo maana katika lugha yao kuna maneno yanashabihiana na ya Kiingereza ama Kiyunani. K.m.

Ear - Ia - Sikio
Colour - Kalay - Rangi
Why - Way - Kwa nini?
Alla (Kiyunani) Alla - Lakini
 
Kabila la Wairaqw linatokana na mbari (race) ya Caucasoid kama yalivyo mataifa ya Ulaya. Ndiyo maana katika lugha yao kuna maneno yanashabihiana na ya Kiingereza ama Kiyunani. K.m.

Ear - Ia - Sikio
Colour - Kalay - Rangi
Why - Way - Kwa nini?
Alla (Kiyunani) Alla - Lakini
Mkuu Yaelekea Ni Mjuzi wa Lugha ya Home Vipi historia Zaidi za Wairaqw na Koo Zake Wengine tunahitaji Tujuzwe fresh Sababu kama mimi Nimeona Jina la Ukoo wetu ni la Datooga so nahitaji sana Nijue zaidi Babu yangu alifikaje Lake zone na Kumbe ni Wa Huko Dah! Alitubadilisha Kabila akasahau Jina lol
 
OHAYODA, OHAYODA, OHAYOOOODAAAA!

Friday, June 1, 2012

Wadatooga: Historia, Maisha na Hatma yao......Sehemu ya Kwanza


Baada ya kuwaletea makala kuhusu Historia, Maana na asili ya jina Mbulu na pia Taratibu za kufuata kama unataka kuoa Mwiraqw, kuanzia leo nitakuwa nawaletea kuhusu jamii au kabila la Wadatooga.
Nikiwa katika harakati za kutengeneza filamu kuhusu Historia, Maisha na Hatma yao kama jamii ambayo imepewa jina la Datooga:Geeleabu yeenu ak ghamneawa geendi yeenu? Ak geegalli yeenu? nimeona niwaletee wasomaji wangu waweze kujifunza mambo mawili matatu kuhusu Wadatoda.
Je Wadatooga ni watu gani?
Wadatooga au watatooga kama wanavyoitwa ni jamii ya kinailotiki wa nyanda za juu ambao wanapatikana Kaskazini mwa Tanzania hasa katika wilaya za Mbulu na Hanang mkoani Manyara japo katika miaka ya hivi karibuni wamesambaa nchi nzima ya Tanzania kusaka malisho ya mifugo yao. Kuna aina mbili za Wanailotiki ambazo ni Wanailotiki wa Nyanda za juu yaani Highland(Southern) Nilotics ambao ni jamii za Wadatooga wa Tanzania, Dorobo na Kalenjin wa Kenya na Wanailotiki wa nyanda tambarare yaani Plains Nilotics kama Wamasai na Luo wa Kenya. Kama wanailotiki wengine, wadatooga asili yao ni Sudan na Magharibi mwa Ethiopia na walifuata bonge la mto Nile (ndio maana wanaitwa Nilotes) kuelekea Kusini

Makundi ya Wadatooga (Dialects)
Kuna lahaja (Dialects) ambazo ndizo zinazounda makundi mbalimbali ya Wadatooga. Makundi haya hutofautina katika mambo kadha wa kadha. Makundi haya ni

  1. Barbayiga (Barbayiiga)
  2. Gisamajanga
  3. Bajuta
  4. Rotigenga
  5. Burediga
  6. Hojabooga
  7. Isimijeega
  8. Gidang`odiga
  9. Bisiyega
  10. Darorajega
  11. Daregwajega
  12. Damarga
  13. Utatu (taturu, Biyenjida)
Wadatooga wote hutambulishwa kwa wanawake wao wanapoolewa kuvalishwa sketi ya ngozi ``Hanang`wenda`` na hujiita ``Geda hanang`wenda`` yaani wavaa ngozi.
Barbayiga (au Barbaig kama wanavyofahamika na wengi) yaani wapiga fimbo au wapenda fimbo kutokana na kupiga fimbo wakati wanacheza ngoma na pia kupenda kukata fimbo kila wanapoona mti unaofaa kwa fimbo ndilo kundi kubwa kuliko yote kwa wadatooga na hivyo kupelekea watu wengi kuwaita wadatooga wote kuwa ni Wabarbayiga.


Historia
Rotigenga wagawanyikia Mlima Elgon
Utafiti unaonesha kuwa walifika mpaka Mlima Elgon uliopo mpakani mwa Kenya na Uganda katika karne ya 18 waligawanyika ambapo Rotigenga waliendelea kuelekea kusini hadi pwani ya mashariki ya ziwa Victoria (wadatooga wanaliita Lahu) na kuishi hapo, mpaka leo hii wapo huko Mara.
Kundi kubwa lililobaki lilielekea kusini mashariki hadi magharibi mwa mlima Kilimantaro (West Kilimanjaro). Mlima ambao wadatooga wanauita Gijedamar yaani ``mtu mwenye kipara, au mlima uliokama shujaa aliyeua Simba`` kutokana na barafu iliyopo juu ya mlima huo kwani wadatooga wanapompongeza mtu kwa ushujaa wake humwekea mafuta ya siagi ya ng`ombe kichwani kama barafu ya Mlima Kilimanjaro ilivyo"
Hapo wakakuta na Wamasai ambao walipigana sana na kuelekea magharibi wakipita Mlima Oldonyo Lengai wanaouita Gijeda Sakuraraig yaani mlima unaotapika moto hadi kreta ya Ngorongoro wanayoiita Fued ambako walikaa kwa miongo mingi sana kabla ya kuondoka hapo baada ya vita na mahasimu wao wakubwa yaani wamasai.
Kutoka Ngorongoro walizidi kusonga kuelekea magharibi hadi bonde la ziwa Eyasi (Mang`ola) ambako wakagawanyika tena ambako kundi moja liliamua kuendelea kuelekea magharibi na kundi lingine likapanda kwenye uwanda wa juu wa bonde la ufa wakielekea kusini magharibi.

Kundi lililoelekea Magharibi
Hili kundi lililoelekea Magharibi lilipofika magharibi mwa ziwa Eyasi maeneo ya Maswa ya sasa, Buradiga wakaamua kubaki pale na ndipo wanapopatikana mpaka leo huku Barbayiga wakiendelea kuelekea Magharibi wakisaka malisho na maji kwa ajili ya mifugo inasemekana wakafika hadi Tabora. Wadattoga wanadai kuwa hata jina la Tabora linaasili yao kwani huko kuna kaburi la mtu moja tajiri sana wa ng`ombe aliyeitwa Bora na kufanyiwa Bung`eda na hivyo kulirefer kama ``Bung`eda Bora) na hatimaye jina hilo kubadilika kuwa Tabora. Hili laweza kuwa kweli kwani majina ya maeneo karibu yote katika maeneo walikopita ni ya Kidatooga hasa katika wilaya za Mbulu na Hanang. (Nitaeleza kuhusu Bung`eda katika sehemu nyingine)
Kutoka Tabora wakaamua kuelekea kusini mashariki hadi Singida na wanadai pia kuwa Singida alikuwa tajiri moja wa Kidatooga aliyekuwa na ng`ombe wengi sana na Bung`eda yake ipo hapo hata sasa. Wakiwa hapo Singida bado waliandamwa na tatizo lile lile la maji kwa ajili ya mifugo yao.
Huko nyuma nako kwa Buradiga, kundi lingine likaamua kuondoka hapo likafika hadi maeneo ya Itigi na kuishi hapo mpaka sasa na hawa ndio Utatu au Biyenjida au Taturu

Kundi lililopanda kwenye uwanda wa juu wa Bonde la Ufa
Kuna waliobaki maeneo ya Mang`ola na maeneo ya ziwa Eyasi wanaloliita Balang`ida Mwamba mfano Isimjega na Daregwajega huku wengine wakipanda hadi maeneo ya Mbulu na kukaa hapo. Gisamjenga walifika Mbulu, Gehandu hadi Dongobesh na wakaishi katika hayo maeneo huku Damarga wakikaa maeneo ya Tlawi ambapo ziwa Tlawi huitwa Basso damarga hata leo.
Dararajega walieendelea hadi wakafika ziwa Bassotu kaskazini magaribi mwa mlima Hanang wakakaa hapo na nyuma yao wakaja Hojabooga ambao walipowakuta Darerajega wanafaidi maji fresh ya ziwa Bassotu ikaibuka vita na Darerajega wengi waliuliwa na Hojabooga kutawala ziwa Bassotu.
Gidang`odiga ambao tofauti na wadatooga wengine, wao si wafugaji bali ni wahunzi wakitengeneza zana mbalimbali na silaha kwa ajili ya makundi mengine. Gidang`odiga maarufu kama Karera wanavyoitwa na Wairaqw wao wapo na wanaishi katikati ya makundi mengine lakini cha ajabu hawaoani na jamii nyingine hasa Barbayiga na Gisamjanga na wapo kwa wingi maeneo ya Dawr, Mewadan na Dongobesh

Barbaig wafika Bassotu
Baada ya kuishi Singida kwa miaka mingi na bado maji yakiwa bado tatizo kubwa kwao, inasemekana kuwa vijana wa Kibarbayiga waligundua uwepo wa ziwa Bassotu wakiwa katika harakati za kumtafuta ng`ombe dume aliyepotea. Uwepo wa maji fresh uliwahamasisha Barbayiga kuhamia Bassotu na ndipo yakatokea mapigano baina yao na Hojabooga na hatimaye Barbayiga kushinda na kutawala maeneo ya Bassotu, kisha kusambaa hadi mlima Hanang upande wa magharibi na kusini.

Bajuta watoka kwa Rotigenga Musoma
Ikumbukwe kuwa Rotigenga walijitenga karne nyingi sana na hawakuwa na mwingiliano wowote na wadatoga wengine bado walikuwa wanajitambulisha kama wadatooga. Baada ya karne nyingi, kundi moja liliondoka huko Musoma kutoka kwa Rotigenga na kupita katikati ya uwanda wa Serengeti hadi Mang`ola. Kundi hili ambalo ndilo Bajuta, ndilo kundi mashuhuri miongoni mwa wadatoga wote kama waganga mashuhuri na hata Nabii ambaye wadatooga wote wanamheshimu na kumuenzi yaani Saigilo Magena (Niteleza kuhusu Saigilo katika mada nyingine) alitokea kwa Bajuta. Bajuta wakaenda mpaka maswa, wakazunguka hadi singida na kisha kuingia Mbulu na kujichanganya na wadatooga wengine.

Hawa ndio Wadatooga, usikose sehemu ya pili tutakapozungumzia Ndoa na miiko ya Wadatooga
You might also like:

Wadatooga: Historia, Maisha na Hatma yao......Sehemu ya Pili


Je Wairaqw ni Wambulu? Fahamu Historia yao na asili ya jina ...


Usiyoyafahamu Kuhusu Wadatooga: Ni mwiko kwa mwanamke ...


Je Wairaqw ni Wambulu? Fahamu Historia yao na asili ya jina ...







Nimeipenda hii Nimeona Movement Ya Babu Yangu... Kudadeki... Back to My Roots
 
Huu upuuzi mie house gal wangu mu Iraq mshamba kweli kweli Kabila limejaa kichwani la kutosha!


UOTE=BIG X;3831651]Kuna uwezekano mkubwa wa kabila la Kiiraqw lilopo mkoa wa manyara kupotea kabisa au asili ya watu hawa kupotea kabisa siku za mbeleni. na hasa ukizingatia na udogo wa kabila lenyewe. Hii ni kutokana na sheria zao kali za kimila zinazoweka mazingira magumu sana ya wenyewe kwa wenyewe kuoana na kusababisha asilimia kubwa ya watu kulazimika kuoa au kuolewa na makabila mengine, sisemi kama kuna ubaya kuoa au kuolewa na makabila mengine. Katika hili kabila kuna kitu kinaitwa DAWI, maana ya DAWI ni uhusiano wa kikoo au kidamu kati ya watu wawili, hata kama ni kitukuu wa kitukuu ambaye Bibi yake ni ukoo wako basi huwezi kumuoa au kuolewa naye kwasababu atakuwa ni DAWI yako. Sasa kutokana na udogo wa hili kabila vijana wengi walioanzisha uhusiano wamejikuta wameingia kwenye huo mtego na kushindwa kuoana.[/QUOTE]
 
Kutokana na hii thread nimeamua kuwauliza wenyeji wangu (nipo maeneo ya Babati/Dareda) nanunua mazao..

Nimewauliza tofauti za kitabia kati "WAFYOMI/GOROWA na Iraqw/Mbulu

Wanasema wafyomi ni wasemaji (wachangamfu kwa wageni), wakweli, wenye haraka,(wanfanya maamuzi yao kwa haraka), wengi wao ni wacha Mungu, hawapendi kudhulumu na pia ni waungwana sana..

Kwa upande wa Wairqw/Mbulu wanasema ni wapole, (si wepesi kuchangamka), hawana haraka (kufanya uamuzi), wanafiki (always kuna kitu wameficha moyoni hawakwambii yote), hawapendi kudhulum na pia ni wacha Mungu na waungwana sana..

Wadau nisaidie kama wamesema ukweli ..nimejifunza mengi sana kwani naenda kila mwaka huku..
 
Mkuu Yaelekea Ni Mjuzi wa Lugha ya Home Vipi historia Zaidi za Wairaqw na Koo Zake Wengine tunahitaji Tujuzwe fresh Sababu kama mimi Nimeona Jina la Ukoo wetu ni la Datooga so nahitaji sana Nijue zaidi Babu yangu alifikaje Lake zone na Kumbe ni Wa Huko Dah! Alitubadilisha Kabila akasahau Jina lol

Soma Vitabu vifuatavyo:

(a) Mapokeo ya Historia ya Wairaqw - Ramadhani Hemedi MBE
(b) The Way of Tribe - Gervas Tatah Mlola
(c) Pia upate masimulizi ya wazee wanaofahamu desturi, mila na historia
 
Soma Vitabu vifuatavyo:

(a) Mapokeo ya Historia ya Wairaqw - Ramadhani Hemedi MBE
(b) The Way of Tribe - Gervas Tatah Mlola
(c) Pia upate masimulizi ya wazee wanaofahamu desturi, mila na historia
Duh Ok Thanks manake hu ni Mtihani tena...Nilidhania unanipa Link... Nitafuatilia Ohayoda...

Kuna Link nimeona Wadatooga ndio Walikuwa Wa Kwanza kufika Serengeti na Ngorongoro Creater lakini walikuja fukuzwa na Masai baada ya Kutomsikiliza Nabii wao ... So hii ndio maana Wakasambaa zaidi...
 
I want to shock you guys now, Jee Mnajua ya kuwa WaiiRAQw, claim they come from IRAQ originaly, But the TRue fact is that they come from ERITREA during the great Miigration, Lugha zao zinafanana sana Baadhi ya waeritrryans hawatetiwi wakija kwa waiiraqwi.

Na WAMANGATI wametoka Somalia, proof niliyokuwa nayo Kuna kabila la huko Somaliland ( Kina RAGE wa Simba) wanaitwa HABR MAGAT watoto wa mama wa kimangati. Maneno yanayofana ni kama:

KIMANGATI ---- KISOMALI
1. Shillingi Bokol (SH 100) ------BOKOL SHILLIN
2. ROBUKA (MVUA)------------ ROOBKA
3. ANOGA (MAZIWA) ----------ANOO
4. AFAA (MDOMO)------------- AF

Do you see the similarity, and the only First people in Tanzania kuweza kuweza kuiishi peacefully na Wabarbeg (Wamangati) ni Wasomali, Ambapo hat Muingereza aliwatumia to venture in to MAASAI na Barbeig Teritories, while kila mtu alikuwa hakubaliki. hata in the early 1960s wakati wa vita za kikabila za Wabarbeig Nyerere aliwahi kuwatumia Wasomali kuwatuliza Wabarbeig.

The WORLD IS SMALL ALL ARE BROTHERS DESPITE OUR POLITICAL AFFILATIONS
 
Kutokana na hii thread nimeamua kuwauliza wenyeji wangu (nipo maeneo ya Babati/Dareda) nanunua mazao..

Nimewauliza tofauti za kitabia kati "WAFYOMI/GOROWA na Iraqw/Mbulu

Wanasema wafyomi ni wasemaji (wachangamfu kwa wageni), wakweli, wenye haraka,(wanfanya maamuzi yao kwa haraka), wengi wao ni wacha Mungu, hawapendi kudhulumu na pia ni waungwana sana..

Kwa upande wa Wairqw/Mbulu wanasema ni wapole, (si wepesi kuchangamka), hawana haraka (kufanya uamuzi), wanafiki (always kuna kitu wameficha moyoni hawakwambii yote), hawapendi kudhulum na pia ni wacha Mungu na waungwana sana..

Wadau nisaidie kama wamesema ukweli ..nimejifunza mengi sana kwani naenda kila mwaka huku..

Kuna rafiki yangu anyeishi Babati aliniambia hayohayo kuhusu wagorowa na wairaqw
 
Hey My Dear Me Sijambo na Mzima wa Buheri... Wajionaje ha hali bibie... Nimekumiss...

hata mi nilikumiss sana tu nikaona nirudi kukusalimu my dear ..
sasa umesha "investigate" ile issue ?? nasubiri jibu kwa hamu :) Duduwasha
 
Last edited by a moderator:
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom