Watanzania ni kabila la pande gani?

mtanzania in exile

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
1,335
1,183
Habari zenu ndugu wote.

Naomba samahani kwa kuwa nitakuwa natuma nyuzi nyingi fupi fupi kuanzia leo hadi nimalize yaliyo moyoni mwangu.

Moyoni kumejaa uzito juu ya suali zima la "Hadhi maalumu" kwa wana diaspora.

kwa leo naanza kwa kuuliza suali langu la hapo juu, hivi jamani watanzania ni kabila la pande gani? nadhani wengi mtashangaa kwa suali hili, ila mimi nimeamua kuuliza suali hili kwa sababu toka majuzi viongozi wa nchi, vyombo vya habari za serikali na vya binafsi wamekuwa wakirudia rudia neno "Watanzania wa diaspora walioukana uraia wao kuondoshewa visa".

Sasa hapo ndipo panaponitatiza mimi, ikiwa tunaambiwa kuwa wameukana uraia wao (hili nitalijadili wakati mwengine) sasa kwa nini bado vyombo vya habari na viongozi wanaendelea kuwaita Watanzania? Kama wamekana kuwa wao sio Watanzania na bado wanaitwa watanzania hivi hili linaeleweka?

Hivi hawa wanaoitwa watanzania lakini sio raia wa tanzania ni wa kutoka kabila linaloitwa watanzania kama yalivyo makabila mengine kama vile wamakonde, wahaya, wasukuma nk au ndio matatizo ya lugha ya kiswahili?

Asanteni
 
Back
Top Bottom