Kabila la Kiiraqw laweza kupotea kabisa Tanzania

Kuna uwezekano mkubwa wa kabila la Kiiraqw lilopo mkoa wa Manyara kupotea kabisa au asili ya watu hawa kupotea kabisa siku za mbeleni na hasa ukizingatia na udogo wa kabila lenyewe.

Hii ni kutokana na sheria zao kali za kimila zinazoweka mazingira magumu sana ya wenyewe kwa wenyewe kuoana na kusababisha asilimia kubwa ya watu kulazimika kuoa au kuolewa na makabila mengine, sisemi kama kuna ubaya kuoa au kuolewa na makabila mengine.

Katika hili kabila kuna kitu kinaitwa DAWI, maana ya DAWI ni uhusiano wa kikoo au kidamu kati ya watu wawili, hata kama ni kitukuu wa kitukuu ambaye Bibi yake ni ukoo wako basi huwezi kumuoa au kuolewa naye kwasababu atakuwa ni DAWI yako.

Sasa kutokana na udogo wa hili kabila vijana wengi walioanzisha uhusiano wamejikuta wameingia kwenye huo mtego na kushindwa kuoana.
mbona nasikia walitoa masepotamia au iraq ya leo mkuu
 
Sawa,lakini kama ni Nilotic,wametoka Egypt,basi labda pia wametoka Iraq. Na ni nani huyo anatoa majina ambayo hayafanani na hali ilivyo? Indeed,hata mimi nina asili ya kijaluo,nilo hamite[great,great grandfahter wangu ni mjaluo,greatgreatgrandmother wangu ni mjaluo] ,kwa hiyo labda ancestors wangu waliishi Misri zamani.
wajaluo ni wa afrika magharibi kwa mansa musah tajiri wa karne
 
Wairaqw ni wengi mno. Idadi yao inakadiriwa kuwa zidi ya millioni mmoja.Wengi sasa wamehamia Loliondo, Iramba, Kondoa, Dodoma, Kiteto, Kilindi n.k., huko hakuna DAA"WI
Mbona mijini awavumi kama wachaga ,wanyakyusa ,wahaa ,wangoni , wasukuma nk
 
Back
Top Bottom