K/koo: Kipande cha Sabuni badala ya simu

K/koo: Kipande cha Sabuni badala ya simu

Wanitapeli,yaaan ni historia ndefu sana,mm nakaa kimara,so nikawa nakwenda buguruni,unajua dar mwaka 2011 ikifika saa nne huwa barabara nyingi foleni hamna,sasa wale matapeli wakaniambia wamepata ajari ubungo walikuwa wanatoka dodom wanaleta ng'ombe dar,yaaan kwa ufupi simuliz ndefu sana
 
Ha ha hA kuna ndugu yangu alitapeliwa, kapewa kijiti cha muhogo mwanzo aliona ni almasi mpk leo tangu 1999 jamaa jina lilibadilika anaitwa Almasi.

Mimi kariakoo nilishapigwa elfu 5 tu. Kama sikosei ilikuwa 2003. Jamaa aliniuzia jinzi kwa bei ya tsh 7000 dah nikatoa fasta, ile nampa akasema bro nimesema 17000/= nikamwambia nipe pesa yangu, akanirudishia fasta kumbe juu kanipa elfu 2 ndan kaifungia karatasi la box, ile elfu 5 kachukua, naenda mbele kufungua nakuta nna elf 2 na box basi, tangu siku iyo sijawai ibiwa wala tapeliwa.

same year nilipigwa kama wewe kwa staili hiyo hiyo mtaa wa Kongo... huo mwaka walikua wengi sana pale halafu jeans walizokua wanashika zilikua bomba kiasi kwamba akikuambia buku tano lazima usimame
 
Mi nakumbuka baada ya kumaliza darasa la saba nikaenda Dar kufanya majaribio shule mbalimbali,siku moja nikakuta wale jamaa wanaokunja mkanda alafu ukichoma katikati unakula mara mbili ya fedha uliyoweka.
Wakaniambia kujaribu ni bure, nikajaribu ya kwanza, kuzungusha mkanda peni iko kati,nikajaribu ya pili peni iko kati,nikajua wajinga hawa nikakimbia home fasta, nikachukua elfu mbili( ya enzi izo) ndio nilikuwa nimebaki nayo tuu,nawahi eneo la tukio ili niwakute bado wapo.
Nikatoa 2000 alafu nikachoma peni,jamaa kuzungusha peni iko nje, nikaanza kuyahisi machozi kwa mbaali ila ndio basi tena.

Ha ha ha ha ha nmecheka sana et "nikaanza kuyahisi machozi kwa mbaali ila ndio basi tena" hii kali sana
 
Ha ha hA kuna ndugu yangu alitapeliwa, kapewa kijiti cha muhogo mwanzo aliona ni almasi mpk leo tangu 1999 jamaa jina lilibadilika anaitwa Almasi.

Mimi kariakoo nilishapigwa elfu 5 tu. Kama sikosei ilikuwa 2003. Jamaa aliniuzia jinzi kwa bei ya tsh 7000 dah nikatoa fasta, ile nampa akasema bro nimesema 17000/= nikamwambia nipe pesa yangu, akanirudishia fasta kumbe juu kanipa elfu 2 ndan kaifungia karatasi la box, ile elfu 5 kachukua, naenda mbele kufungua nakuta nna elf 2 na box basi, tangu siku iyo sijawai ibiwa wala tapeliwa.
Ah ah ah ah pole sana
 
Mimi ubungo niko narudi arusha, nikanunua magazeti nikiwa ndani ya basi, muuzaji yuko chini nikacheck headings nikanunua magazeti 3,basi limeondoka nakuja kuyacheki kumbe ya mwaka 2002 hapo ilikua mwaka 2004
Ah ah ah ah uhiii.
 
mwaka 2002 maeneo ya MBAUDA wale wazee wa MKANDA na KALAMU. anasokota mkanda unaweka kalama. Daaaah nilicheza kwa BUKU tu nikaliwa wajamaa niliwapa elfu 10 wakagoma kunirudishia buku 9 na mchezo wakavunja wakasepa.
 
Daah wale watakua na dawa aisee si bure. Mi pia walishanipiga hao. Walilamba 20,000 yangu hivi hivi plus kasim kangu fulan kabovu bovu hivi nikajua hapa nimewabambika. Kufika mbele kufungua sabuni yangu ya kipande safi kabisa nimefungiwa vizuri.....daah sabuni ya 100 nikauziwa 20,000. Belive me toka ijumaa april 20 2012 leo ndo nimekitoa hadharani hiki kitu.....kilibakia kuwa siri siku zote hizo.
kubwa jinga duuuuu walikuweza hivi ulipoenda likizo nyumbani kwenu kijijini na wewe ulijidai mbele za marafiki, jamaa na ndugu zako kwamba unaishi na kufanya kazi Dar kweli? jibu nadhani unaloo ukiingia benki kuna tangazo kwa tela kikisomeka hesabu pesa zako kabla hujaondoka kaunta, sasa wewe elimu hiyo hukuwa nayo miaka hiyo weee mburura lazima wakulize unafikiri kuwa na elimu ya darasani ndo umejua kila kitu hii ndo bongo bhana tumia bongo uishi chezea machinga wa mtaa wa kongo....
 
Mi niliuziwa chandarua ambacho kimetumika na kimechakaa kabisa. Nilikiona ni kizuri kipo kwenye mfuko wake kabisa, kufika nyumbani duuuuh, yani hadi kinanuka! Kutapeliwa au kuibiwa dsm ni jambo la kawaida kabisa.
 
Bure ni ghali! Hiki ndicho kinachotuponza waTanzania. Mchina katuweza, mpaka simu za elfu 10 katutengenezea!!
 
Bure ni ghali! Hiki ndicho kinachotuponza waTanzania. Mchina katuweza, mpaka simu za elfu 10 katutengenezea!!
Sio kwamba bure au bei nafuu, nilinunua kwa bei kawaida kabisa kama ya dukani, The only mistake i dd ni kununua kwa machinga! Mpaka leo sina hamu ya kununua vitu kwa wamachinga bora niingie dukani tu hata nikibambikiziwa naweza kurudi
 
Ilikuwa kitumbini DSM..2004
Tapeli kavaa smart
Gia yake yy ni doctor
Aliniliza 23,000 tena akataka nimwongeze,nikagoma..
Kuanzia hapo..Chale huwa zinànicheza kila nikiona kichaka
 
Kwa maelezo haya inaonyesha wengi wanaotapeliwa wanapenda kununua vitu vya wizi, tamaa ya kupata fedha fasta na shortcut
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom