K/koo: Kipande cha Sabuni badala ya simu

zegamba180

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
818
536
Binafsi niliingizwa chaka kariakoo kwa kununua kipande cha sabuni badala ya simu mwaka 2006.

Akaniambia ameiba mtaa wa pili hivyo nimpoze kidogo anipe, tena nifanye fasta atakutwa. nikamwambia sikuwa nimejiandaa kununua simu kwa siku hiyo. hivyo ntampa sh 20,000.

Akadai nimuongeze kidogo nikaona niokoe muda nikamuongezea sh 10000, zikawa sh 30,000.

Ile simu dukani ilikuwa inauzwa 80,000. Sijuhi ilikuwaje nikageuka upande wa pili, ndo likawa kosa kubwa nikakuta jamaa ameshaniwekea katika box na mfuko akaniambia nikafungulie mbele.

Nifanye fasta niondoke nikikutwa nitajijua. Kwa spidi ya 4G nikaingia katika bus siti ya nyuma niliyokaa.

Nikasubiri bus lianze kuondoka nikafungua kuona simu yangu.

Looohooooo ni kipande cha sabuni(mbuni). Niliona giza!
Nawe tuambie uliingizwaje chaka town?
 
Umenikumbusha jamaa mmoja walimliza kwa kumuuzia sabuni badala ya simu. yeye akakomaa kwamba wale jamaa ni wachawi maana haiwezekani kaondoka na simu nzima kabisa kufika home anakuta kipande cha sabuni.
 
Ha ha hA kuna ndugu yangu alitapeliwa, kapewa kijiti cha muhogo mwanzo aliona ni almasi mpk leo tangu 1999 jamaa jina lilibadilika anaitwa Almasi.

Mimi kariakoo nilishapigwa elfu 5 tu. Kama sikosei ilikuwa 2003. Jamaa aliniuzia jinzi kwa bei ya tsh 7000 dah nikatoa fasta, ile nampa akasema bro nimesema 17000/= nikamwambia nipe pesa yangu, akanirudishia fasta kumbe juu kanipa elfu 2 ndan kaifungia karatasi la box, ile elfu 5 kachukua, naenda mbele kufungua nakuta nna elf 2 na box basi, tangu siku iyo sijawai ibiwa wala tapeliwa.
 
Daah wale watakua na dawa aisee si bure. Mi pia walishanipiga hao. Walilamba 20,000 yangu hivi hivi plus kasim kangu fulan kabovu bovu hivi nikajua hapa nimewabambika. Kufika mbele kufungua sabuni yangu ya kipande safi kabisa nimefungiwa vizuri.....daah sabuni ya 100 nikauziwa 20,000. Belive me toka ijumaa april 20 2012 leo ndo nimekitoa hadharani hiki kitu.....kilibakia kuwa siri siku zote hizo.
 
dumelang nami kama hiyo yako pia ilinikuta. mimi nilitaka kununua sandoz. hawa jamaa wana dawa c bure
 
Daah wale watakua na dawa aisee si bure. Mi pia walishanipiga hao. Walilamba 20,000 yangu hivi hivi plus kasim kangu fulan kabovu bovu hivi nikajua hapa nimewabambika. Kufika mbele kufungua sabuni yangu ya kipande safi kabisa nimefungiwa vizuri.....daah sabuni ya 100 nikauziwa 20,000. Belive me toka ijumaa april 20 2012 leo ndo nimekitoa hadharani hiki kitu.....kilibakia kuwa siri siku zote hizo.
ahaaaa aaaa jamani tupo wengi sana. wanadawa
 
kabla ya kutoa pesa chukua kagua kwanza kikiwa chenyewe husimrudishie ili akuwekee katika mfuko. mwambie mfuko utanunua mwenyewe, ukipugi ukampa akuwekee yeye umepigwa. Wakikuona unawakazia wanajifanya hawauzi tena. wale wa karata tatu husicheze kamwe utaliwa tu. wanaojifanya wanacheza nao ni wenzao. Ntakuja na uzi mwingine kuonesha namna wanvyotuibia
 
Haaahaaaaahaaaa. Hii bila shaka inatokeaga sana katika online dating. Ukituma tuu imekula kwako.

Sana tu, ingawa hata kawaida inatokea lakini ni kwa nadra sana ukilinganisha na online dating.
 
Mimi hivyohivyo ubungo pale. Kuna dawa wanatumiaga walahi. Me nilikodoa macho kwa tahadhari sana, lazima kuna mchezo pale macho yanachezewa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom