Watanzania kwa ujumla wetu lazima tuanze kuwalazimisha viongozi wetu kujiuzuru kwa lazima. Hii si nchi ya CHADEMA, ni nchi ya watanzania. Waliokufa, kujeruhiwa na kupoteza makazi Niwatanzania. Pesa zitakazotumika kwa shughuli zote mpaka kulipa fidia Nizawatanzania.Lazima tuhoji, tupewe maelezo ya kutosha na kuwalazimisha wazembe wajiuzuru hata kwa lazima.
Hivi kama hatutawalazimisha viongozi hawa wazembe wajiuzuru kwa suala zito kama hili (tena limetokea mara mbili), ni suala gani ambalo litatusukuma kuwalazimisha hawa wazembe wawajibike. Wamelewa starehe na maisha ya juu kwa gharama ya kodi zetu mpaka hawajui wala kutekeleza wajibu wao.
Watanzania tuamke na tuache kulea upumbavu.