JWTZ na taarifa ya Mabomu Gongo la Mboto

Ingependeza kama mgetoa updates kwenye bandiko la kwanza, kutueleza wamesema nini?? Maana nimepitia kurasa zote sioni mbona chochote??
 
Duuh mi naona wakati umefika wa kuajiri watu wenye Elimu huko Jeshini tena wawe vijana wadogo wasio zidi umri wa 18-24. Brig Gen Mzima hajui kujibu maswali isitoshe basi ujeuri na ubabe juu utafikiri hii nchi ni yao Pekee yao. Na anajibu kwa kejeli maswali mengine.

Hii nchi kila sehemu kuna vilaza nafikiri ndio Mkubwa wa Majeshi ameingia mitini kuogopa kupata aibu.

:wink2:
 
Waliongea ni brigedia generali Meena na Mdeme,Jamaa wapo juu juu sana,vitu viwili walivyosema ambavyo ninavitafakari ni mosi hakuna kujiuzuru,na pili milipuko ya mbagala na G/mboto ni tofauti hivyo tukio la mbagala halikujirudia?

Suala la kuondoa milipuko katika maeneo ya makazi lilihusu mbagala na imekwishaondolewa pia kuwapo kwa kambi za jeshi sehemu fulani ni kwa ajili ya usalama wa taifa.

Nchi hii kila kitu kinachukuliwa kawaida sana vifo,ulemavu na kupoteza mali za watanzania masikini ni jambo la kawaida kwa viongozi,tufanyejeeeeeeeeeeeeeee?
 
Hatuna wataalam wa milipuko nje ya JWTZ wenyewe. Hivyo watajichunguza wenyewe na kutupatia kile wanachoona ni sahihi! Tusahau tu tusonge mbele. Mbona Mbagala tulishasahau.

Ndugu yangu hii Tanzania yetu inatia huruma kutokana na matukio ambayo ni hatari lakini wahusika wanafanya mzaha.Ni matarajio ya kila mtu kwamba yaliyotokea mbagala yasingelize kutokea tena hata kwa muda mfupi kiasi hiki.

Ina maana kwamba nguvu kubwa ya kuwa na tahadhari ingefanywa na wataalam wa jeshi ili jambo hilo la mbagala lisirudie tena. Sasa LEO hii gongo la mboto! Je kesho wapi? Maneno kwetu ndio amri ya kila siku kule jeshini! utaalam nyuma--------

Je tutafika?
 
There are currently 309 users browsing this thread. (97 members and 212 guests)

Duh leo mko wengi !!!.
 
Kukopi current user's names browsing the thread sioni kama ni Ugreat thinker.....kama huna cha kuchangia, unahaki zote kusoma michango ya wengine!
 
meela-paul.jpg

Brig. Gen. Meela Mkuu wa Usalama na Utambuzi Jeshini

Huyo Aliyevaa Combati sio Meela!!
 
Jamani katika mambo ambayo hayana siasa ni Vyombo vya ulinzi na usalama. Alafu kingine ni kucheza na akili za watu kwa kuwafikirisha mambo yasiyo ya kweli au tusiyokuwa na uhakika nayo.

Ni makosa makubwa kuunganisha maswala ya usalama na vyama vya sias au kufanya yaliyotokea kama sehemu ya kujipatia ujiko wa kisiasa maana utakua huna tofauti na vibaka waliofurahia tukio hilo na kwenda kuiba na kuwakaba wahanga au wale wauza mahitaji pale uwanja wa taifa waliopandisha bei ya vitu bila kujali anayemuuzia katoka katika hali gani.

Ushauri wangu wanasiasa wote tuache kutafuta umaarufu maana sikuona mmbunge yeyote wa chama chochote au mwanaharakati yoyote aliyetoa pendekezo au mswada wa uhufidha wa silaha zetu baada ya tukio la mbagala. Nafikiri cha muhimu ni kushauri namna ya kuhifadhi silaha zetu maana usitake kuniambia hamfahamu mahali JF kenedy military Base iko kwenye makazi ya watu, hakumbuki gesi ya nyuklia iliyotokea nchi za sweden, norway na scotland ambyo tena milipuko ilitokea nje ya nchi hizo, je kama mabomu yatahifadhiwa maeneo kama katikati ya ya msata huko alafu mzinga ulipuke hautafika dar? jamani lets think twice "kama vipi silaha zetu tukazihifadhi nchi nyingine siku tukiyahitaji tukayachukue".

Ndiyo Waziri katika level ya siasa he has to resign maana alisha ahidi kuwa likitokea kama mbagala atawajibika maana alitamka kwa maslahi ya kisias but he was no scientifically right huwezi ukadetermine ustahimilivu wa umeme hasa wenye mlipuko. Ni hivi majuzi India walitaka kurusha rocket anga za mbali lakini ikalipuka na kuunguza kituo cha kurushia kabla ya kuruka.

Mkuu wa jeshi asijiuzulu maana alionyesha jitihada za kijeshi kuhangaika usiku ule na kuaihirisha programme zote na hata alipokutana na rais usiku na kukubaliana baraza la usalama wa taifa likae kujadili ni juhudi kubwa. Kwanza watu walishaambiwa muda mrefu tu kuwa hayo maeneo hayafai wakaingia tu tena kwa kuvamia wakipewa kichapo mnasema wanawadhulumu, kumbuka yaliyotokea kunduchi 2005/2006 mpaka wanajeshi wakaamua kuwapiga wananchi walokua wanajenga ndani ya kambi lakini watu wakaenda mahakamani tena wakisaidiwa na mwanasias machachari yakijalipuka madude oh jeshi lihamishe silaha. Kipindi hizo kambi za jeshi zilipojengwa kulikua ni nyika na misimba tu sasa hivi kwa raia.

watu wanalalamika kwanini mabomu yasihamishwe, ni kuvute yuma kidogo kuwa watati mabomu yanahamishiwa gongo lamboto miaka hiyo kulitokea milipuko mikubwa lakini hakukuwa na madhara makubwa maana idadi ya watu dar ilikua ndogo sana tofauti na sasa je yakihamishwa sasaivi alafu litokee la kutokea maana ajali haikwambii sasa natokea mtaanza kusema ohh fulani kafanya hivi mara vile wajiuzulu nk. Mwanasiasa anaweza kumwambia mpinzani wake ajiuzulu hata kama ni mafuriko au drought na kumwambia alisababisha yeye.

Milipuko imetokea yes je ni mara ya ngapi? ya pili au tatu au nne je ingekua ni mara ya kumi si tungefanya mapinduzi ya kijeshi sasa!!! Tuombe Mwenyezi Mungu atusaidie isitokee tena na wataalamu badala ya kupiga makelele tu watoe ushauri wa kisayansi siyo siasa tu ya namna au nini cha kufanya kusaidia walioathirika na kuangalia namna ya kukabiliana na majanga ya aina hiyo hapa nchini.

Nikumbushe wanaosema kuwa CDF anaongea wakati amiri jeshi mkuu ameshaongea - kumbuka Rais alkua anajibu maswali ya waandishi wa habari hakuitisha mkutano na waandishi wa habari na ndiyo maana hakukua na written statement. Pili rais hakuzungumzia military technical issues kwa mujibu wa sheria na taratibu alizungumzia hali ilivyokuwa na nini kinafanyika na mwisho kiutaratibu mkuu wa kitengo cha ulinzi jeshinindiye aliyetoa taarifa ya tukio kitaalamu akiwa na wataalamu wengine wa mabomu.

Kama wanasiasa wanataka CDF ajiuzulu basi nishauri kuwa akijiuzulu na jeshi zima lijiuzulu maana they all fall to him scientifically.

Tuache politic tujenge nchi, tutatue matatizo yetu kitaalamu, tufuatilie mambo kitaalamu na tufanye investigation kitaalamu na siyo kuropoka au kukurupuka na kujibu au kshabikia mambo kisias.
 
Hapo Kwenye Red Nenda kamwambie Kikwete sio sisi walalahoi tunaolalamika kila kukicha na hatusikilizwi Kama umetumwa kawaambie waanze wao Kutuonyesha jinsi ya kujenga nchi kwa kuwa sisi tumeshaanza zamani wao ndio wanavunja na wafujaji wa Kodi zetu, Kutuingiza kwenye mikataba Feki, kutotujali na kutudharau kwa kuwa wao ndio wameshika dola na kukwapua kodi zetu kwa ubinafsi wao.

Hospitalini hakuna dawa. Halafu la mwisho waonyeshe uzalendo wao kwa kuwapa huduma ndugu zetu walio umia G'Mboto kwa kuwaonyesha kuwa wanawajali kwa kuwapelekea mahitaji muhimu sio kuwaambia wakalale uwanjani halafu Serikali haitoi msaada wowote zaidi ya kutudanganya kwenye maluninda na viredio vyao mbao. MNAFI MKUBWA INAELEKEA UNATETEA SANA UFISADI😡

Kukopi current user's names browsing the thread sioni kama ni Ugreat thinker.....kama huna cha kuchangia, unahaki zote kusoma michango ya wengine!

Thanks rev ..it wasnt inteded... hope you have seen the exact post !!!
 
Lazima tukubali ukweli, mtazamo wangu ni kuwa hawa maafande wetu wamejibu vizuri kutokana na maelekezo ya waliyopewa na wakubwa wao, tukubali tu, the guys are good, wanauwezo hilo halina ubishi.

Wasiwasi wangu ni uwezo wa wanahabari wetu, to be sincely I am shocked na maswali yaliyokuwa yana ulizwa ni majungungu majungu tu, pengine na ushabiki au maslahi binafsi, kunammoja alikuwa anauliza swali elekezi kutaka kumlazimisha afande Mndeme amukubalie kuwa umeme unaweza kuwa tatizo (ana agenda ya tununue dowans), hii ni ngumu kwelikweli.

Tufike mahali waandishi wa habari wasifanye kazi zao kiholela holelaa tu, wawe na specilization. Kama wewe ni muandishi wa habari wa masuala yanayo husu Jeshi, afya, sheria, uchumi, n.k iwe hivyo, otherwise jamii itakuwa inapotoshwa kweli na hawa waandishi wa habari. Leo nimeshuhudia maafande wamepata kazi yepesi kabisa katika kujibu maswali ya hawa waandishi wa habari. Infact karibu kila baada ya jibu kujibiwa mapungufu ya uwezo wa muulizwa swali yalijidhihirisha waziwazi kabisa
 
Jamani katika mambo ambayo hayana siasa ni Vyombo vya ulinzi na usalama. Alafu kingine ni kucheza na akili za watu kwa kuwafikirisha mambo yasiyo ya kweli au tusiyokuwa na uhakika nayo.

Ni makosa makubwa kuunganisha maswala ya usalama na vyama vya sias au kufanya yaliyotokea kama sehemu ya kujipatia ujiko wa kisiasa maana utakua huna tofauti na vibaka waliofurahia tukio hilo na kwenda kuiba na kuwakaba wahanga au wale wauza mahitaji pale uwanja wa taifa waliopandisha bei ya vitu bila kujali anayemuuzia katoka katika hali gani.

Ushauri wangu wanasiasa wote tuache kutafuta umaarufu maana sikuona mmbunge yeyote wa chama chochote au mwanaharakati yoyote aliyetoa pendekezo au mswada wa uhufidha wa silaha zetu baada ya tukio la mbagala. Nafikiri cha muhimu ni kushauri namna ya kuhifadhi silaha zetu maana usitake kuniambia hamfahamu mahali JF kenedy military Base iko kwenye makazi ya watu, hakumbuki gesi ya nyuklia iliyotokea nchi za sweden, norway na scotland ambyo tena milipuko ilitokea nje ya nchi hizo, je kama mabomu yatahifadhiwa maeneo kama katikati ya ya msata huko alafu mzinga ulipuke hautafika dar? jamani lets think twice "kama vipi silaha zetu tukazihifadhi nchi nyingine siku tukiyahitaji tukayachukue".

Ndiyo Waziri katika level ya siasa he has to resign maana alisha ahidi kuwa likitokea kama mbagala atawajibika maana alitamka kwa maslahi ya kisias but he was no scientifically right huwezi ukadetermine ustahimilivu wa umeme hasa wenye mlipuko. Ni hivi majuzi India walitaka kurusha rocket anga za mbali lakini ikalipuka na kuunguza kituo cha kurushia kabla ya kuruka.

Mkuu wa jeshi asijiuzulu maana alionyesha jitihada za kijeshi kuhangaika usiku ule na kuaihirisha programme zote na hata alipokutana na rais usiku na kukubaliana baraza la usalama wa taifa likae kujadili ni juhudi kubwa. Kwanza watu walishaambiwa muda mrefu tu kuwa hayo maeneo hayafai wakaingia tu tena kwa kuvamia wakipewa kichapo mnasema wanawadhulumu, kumbuka yaliyotokea kunduchi 2005/2006 mpaka wanajeshi wakaamua kuwapiga wananchi walokua wanajenga ndani ya kambi lakini watu wakaenda mahakamani tena wakisaidiwa na mwanasias machachari yakijalipuka madude oh jeshi lihamishe silaha. Kipindi hizo kambi za jeshi zilipojengwa kulikua ni nyika na misimba tu sasa hivi kwa raia.

watu wanalalamika kwanini mabomu yasihamishwe, ni kuvute yuma kidogo kuwa watati mabomu yanahamishiwa gongo lamboto miaka hiyo kulitokea milipuko mikubwa lakini hakukuwa na madhara makubwa maana idadi ya watu dar ilikua ndogo sana tofauti na sasa je yakihamishwa sasaivi alafu litokee la kutokea maana ajali haikwambii sasa natokea mtaanza kusema ohh fulani kafanya hivi mara vile wajiuzulu nk. Mwanasiasa anaweza kumwambia mpinzani wake ajiuzulu hata kama ni mafuriko au drought na kumwambia alisababisha yeye.

Milipuko imetokea yes je ni mara ya ngapi? ya pili au tatu au nne je ingekua ni mara ya kumi si tungefanya mapinduzi ya kijeshi sasa!!! Tuombe Mwenyezi Mungu atusaidie isitokee tena na wataalamu badala ya kupiga makelele tu watoe ushauri wa kisayansi siyo siasa tu ya namna au nini cha kufanya kusaidia walioathirika na kuangalia namna ya kukabiliana na majanga ya aina hiyo hapa nchini.

Nikumbushe wanaosema kuwa CDF anaongea wakati amiri jeshi mkuu ameshaongea - kumbuka Rais alkua anajibu maswali ya waandishi wa habari hakuitisha mkutano na waandishi wa habari na ndiyo maana hakukua na written statement. Pili rais hakuzungumzia military technical issues kwa mujibu wa sheria na taratibu alizungumzia hali ilivyokuwa na nini kinafanyika na mwisho kiutaratibu mkuu wa kitengo cha ulinzi jeshinindiye aliyetoa taarifa ya tukio kitaalamu akiwa na wataalamu wengine wa mabomu.

Kama wanasiasa wanataka CDF ajiuzulu basi nishauri kuwa akijiuzulu na jeshi zima lijiuzulu maana they all fall to him scientifically.

Tuache politic tujenge nchi, tutatue matatizo yetu kitaalamu, tufuatilie mambo kitaalamu na tufanye investigation kitaalamu na siyo kuropoka au kukurupuka na kujibu au kshabikia mambo kisias.

Mabula; nasikitika sana kwamba baadhi yetu ambao inawezekana ni Wasomi na Wanataaluma wanatetea uozo kwa sababu ambazo hazijulikani. katika jamii ya kistaarabu kuwajibika ni jambo la kawaida na wala halihitaji mtu akushikie bango.

As professionals kila Engineering Device au Equipment, Chemiclas nk mfano mabomu vina namna ya kuwa handled. Kuna watu wanasomea na kuhitimu na kukabidhiwa majukumu na dhamana.

Then kuna swala zima la uwajibikaji ambalo linaendana na professional ya mtu, maadili ya kazi. Leo hii huwezi ukatuambia kuwa Mabomu yaliyolipuka Mbagala hadi leo hakuna mtu anajua ni nini kilitokea na bado baadhi mnaona vyema tukubali tu yaishe. I wonder.

Yametokea tena juzi, Gongo la Mboto; Raia wasio na hatia wamekatizwa uhai wao na wengine kuachwa vilema, acha kukosa makazi na kuathirika kiafya na kisaikolojia. Mabomu ni mengi yamelipuka kutoka katika ghala tofauti, then kama kawaida wenye madaraka wanasema uchunguzi ufanyike . . . na hakuna nayetaka kuchukua responsibility. What a shame! Oooh please give me a break . . .

- Tunao wakaguzi wa maboumu wa mara kwa mara
- Tunao watu wa security
- Tunao watu wa kiutawala
- Tunao watu wenye information kuhusu hayo mabomu, muundo wake, expiry date, mazingira gani yahifadhiwe nk.

Leo hii janga limetokea na hakuna mtu anakubali kuchukua responsibility.

Mbali na hasara kwa raia, ni hasara kwa taifa kwani bei ya mabomu si ndogo hata kidogo, kutatunza nk vyote ni cost kwa taifa.

Kwa nini wakati mwingine tunapenda kutetea hata yaliyo dhahiri?

Let us think Uzalendo sometimes kabla hatujapost.

Respect.

Allien
 
Jamani katika mambo ambayo hayana siasa ni Vyombo vya ulinzi na usalama. Alafu kingine ni kucheza na akili za watu kwa kuwafikirisha mambo yasiyo ya kweli au tusiyokuwa na uhakika nayo. Ni makosa makubwa kuunganisha maswala ya usalama na vyama vya sias au kufanya yaliyotokea kama sehemu ya kujipatia ujiko wa kisiasa maana utakua huna tofauti na vibaka waliofurahia tukio hilo na kwenda kuiba na kuwakaba wahanga au wale wauza mahitaji pale uwanja wa taifa waliopandisha bei ya vitu bila kujali anayemuuzia katoka katika hali gani.

Mkuu nakubaliana na wewe sio vizuri kuunganisha siasa na vyombo vya usalama. Lakini hi tatizo lilianza kwa serikali yenyewe. Kama ilivyo sasa hivi ni vigumu kutofautisha vyombo vya ulinzi na usalama na vipi na viongozi wa kisiasa ni wapi. Angalia kwa mfano hao wakuu waliokutana na wanahabaro leo. Mwanajeshi anaulizwa vipi mbona mlisema kuwa yaliyotokea Mbagala hayatatokea tena, yeye anajibu ya Mbagala ni tofauti na ya Gongo Mboto. Kama hii sio politics ni nini? Tuna tatizo kubwa Tanzania. Vyombo vyetu vya ulinzi vinatumika kukidhi haja za kisiasa.

Mkuu wa jeshi asijiuzulu maana alionyesha jitihada za kijeshi kuhangaika usiku ule na kuaihirisha programme zote na hata alipokutana na rais usiku na kukubaliana baraza la usalama wa taifa likae kujadili ni juhudi kubwa.

Ulikuwa nae wakati huo akihangaika? Au na wewe unacheza na akili za watu kwa kuwafikirisha mambo yasiyo ya kweli au uusiyokuwa na uhakika nayo?

Kwanza watu walishaambiwa muda mrefu tu kuwa hayo maeneo hayafai wakaingia tu tena kwa kuvamia wakipewa kichapo mnasema wanawadhulumu, kumbuka yaliyotokea kunduchi 2005/2006 mpaka wanajeshi wakaamua kuwapiga wananchi walokua wanajenga ndani ya kambi lakini watu wakaenda mahakamani tena wakisaidiwa na mwanasias machachari yakijalipuka madude oh jeshi lihamishe silaha. Kipindi hizo kambi za jeshi zilipojengwa kulikua ni nyika na misimba tu sasa hivi kwa raia.

Kweli wananchi nao inabidi wachukue part ya lawama. lakini so far kwenye majanga yote mawili ya Mbagala na Gongo la mboto, jeshi halijasema sababu za kulipuka mabomu ni wananchi kuishi karibu. Pia kumbuka kwenye hizi kambi huwa wanaishi wanajeshi ambao pia nao ni binadamu. Hata kama yangekuwa mbali na kulipuka hao wanajeshi nao si wangeadhirika?

watu wanalalamika kwanini mabomu yasihamishwe, ni kuvute yuma kidogo kuwa watati mabomu yanahamishiwa gongo lamboto miaka hiyo kulitokea milipuko mikubwa lakini hakukuwa na madhara makubwa maana idadi ya watu dar ilikua ndogo sana tofauti na sasa je yakihamishwa sasaivi alafu litokee la kutokea maana ajali haikwambii sasa natokea mtaanza kusema ohh fulani kafanya hivi mara vile wajiuzulu nk. Mwanasiasa anaweza kumwambia mpinzani wake ajiuzulu hata kama ni mafuriko au drought na kumwambia alisababisha yeye.

Hapo mimi nafikiri zaidi ni uzima wa hayo mabomu yenyewe. Kama ni mazima yanaweza kuhamishika tuu bila kulipuka. Kama huwa yanalipuka hovyo hovyo itakuwaje kama tuna vita na tunataka kuyapeka eneo la vita? Yatafika kweli? Tunahitaji details zaidi za hayo mabomu. Hata kama ni mapya kuna umuhimu wa kujua yalinunuliwa lini, wapi, and for what purpose.

Milipuko imetokea yes je ni mara ya ngapi? ya pili au tatu au nne je ingekua ni mara ya kumi si tungefanya mapinduzi ya kijeshi sasa!!! Tuombe Mwenyezi Mungu atusaidie isitokee tena na wataalamu badala ya kupiga makelele tu watoe ushauri wa kisayansi siyo siasa tu ya namna au nini cha kufanya kusaidia walioathirika na kuangalia namna ya kukabiliana na majanga ya aina hiyo hapa nchini.

This what Tanzania will be dying for. Kila kitu tunamwachia Mungu. Nakubali Mumgu ni mkubwa wa vyote and HE can do anything. Lakini kama sisi wenyewe hatutachukua efforts za kuzui haya majanga yataendelea kutokea. Kuhusu wataalamu, sidhani kama huwa wanapewa nafasi ya kutumia taakuma yao. ndio maana wanaishia kupiga makelele. Chukulia issue kama ya umeme, unafikiri hatuna wataalamu wanaoweza kuja na idea nzuri za kudeal na hili tatizo? Wapo wengi tuu but issue yenyewe imebebwa na wanasiasa. They think they are the best to deal with the issue. Juzi tuu Mh. Makamba na Mh Mnyika walitaka Tanesco umeme tena toka Dowans utafikiri is just simple like that. Too much politics kwenye issue nyeti. Wataalamu wetu hawapewi nafasi kutatatua matatizo yetu. As a result, nao wameamua kuwa wanasiasa.

Nikumbushe wanaosema kuwa CDF anaongea wakati amiri jeshi mkuu ameshaongea - kumbuka Rais alkua anajibu maswali ya waandishi wa habari hakuitisha mkutano na waandishi wa habari na ndiyo maana hakukua na written statement. Pili rais hakuzungumzia military technical issues kwa mujibu wa sheria na taratibu alizungumzia hali ilivyokuwa na nini kinafanyika na mwisho kiutaratibu mkuu wa kitengo cha ulinzi jeshinindiye aliyetoa taarifa ya tukio kitaalamu akiwa na wataalamu wengine wa mabomu.

This just support the argument how our president is. Yaani mpaka sasa hivi bado hakuna official statement toka sio tuu kwa mkuu wa nchi bali pia amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Tanzania. Alishia tuu kujibu maswali aliyoulizwa na waandishi wa habari mitaani. Surely He need to act as a President. Kama ulikuwa unamfuatilia Obama kwenye issue ya Misri whenever there was any develpement alikuwa anatoa official statement from the While House. Hadi sasa hatuna official official statement toka Ikulu.

Kama wanasiasa wanataka CDF ajiuzulu basi nishauri kuwa akijiuzulu na jeshi zima lijiuzulu maana they all fall to him scientifically.

Kama vile unasema waziri wa ulinzi akijiuzulu basi na wale wote wanaofanya kazi kwenye wizara hiyo nao wajiuzulu. Does that make sense to you?

Tuache politic tujenge nchi, tutatue matatizo yetu kitaalamu, tufuatilie mambo kitaalamu na tufanye investigation kitaalamu na siyo kuropoka au kukurupuka na kujibu au kshabikia mambo kisias.

Una point nzuri hapa ila sijui mlengwa hapa ni nani. Ndio tufuatilie mambo kitaalamu na tufanye investigation kitaalamu na siyo kuropoka au kukurupuka but do you know anything kuhusiana na uchunguzi wa mabomu ya Mbagala? What did the investigation found out and why that report has never been realeased to the public? Au ni kwa sababu za kiteligensia? Huoni kama hii ndio inasababisha watu kuropoka?
 
Back
Top Bottom