JWTZ na taarifa ya Mabomu Gongo la Mboto

Siku hizi wenzio hawaiiti tume, wanasema BARAZA LA UCHUNGUZI!!! teh teh teh
 
ndio anamaliza, sijaona substance aliyoongea...actually discussions za jf ni far educative na ziko juu na mbele ya wakati kuliko anachoongea huyu afande.
 
na mbagala ilikuwa ajali siyo? then itatokea nyingine na nyingine> ni uzembe wanatakiwa watuombe msamaha!! hamna mambo ya bahati mbaya!:spider:
 
JamiiForums,

Jana nimeangalia clip ya mkulu (Amiri Jeshi Mkuu Mh. Rais) akiweka siri za jeshi letu wazi namnukuu '' Gongo-la-Mboto ndiyo kambi yenye silaha zote kali na nyingi kupita zote Tanzania'-source Video clip GlobaPublishers na abbymrisho -gongolamboto video youtube.

Hapa mkuu wa usalama jeshi anatumia power-point presentation tuwaelezea maadui wa Tanzania kwa kina siri zetu za kijeshi ila siri za Kagoda na DeepGreen ndiyo siri za Taifa.
 
Kaka habari kutozipata mapema si kwa sababu ya mgao wa umeme, bali ni mfumo wa utendaji kazi mbaya si kwa vyombo vya serikali bali pia hata kwa vyombo binafsi. Imagine tukio linatokea Dar, Gongolamboto sehemu inayofikika kirahisi maana ni njiani kabisa na barabara ni lami tupu lakini hakuna hata TV station hata moja ilorusha picha za matukio hadi ilipofika saa sita usiku, wakati mchezo umeanza rasmi toka saa moja na nusu usiku???.

Hata kama wasingerusha picha za ndani ya jeshi kutokana na sababu za kiintelejensia, lakini japo tu kuonesha misululu ya watu barabarani wanavyohangaika na watoto ingesaidia saana watu kuweza locate ndugu na jamaa zao. Watanzania wenye vyombo vya habari tuwe wabunifu jamani, tusifurahie tu BBC, Aljazeera, Sky news na CNN wanavyorusha matukio yao, bali tujifunze kutoka kwao.

Mkuu nakuunga mkono. Vyombo vyetu vya habari ni kama havipo. Yaani wao wanasubiri wanaletewa habari na watawalandio watangaze. Maana yake hapo ni kuwa vyombo vya habari ni watawala wenyewe. Watu tumepata habari kwenye redio mbao ambazo Rais amesema tusizisikilize. Sasa tutapata habari wapi wakati vyombo vyetu vya habari havitoi habari? Hili ni janga la taifa but it seems as no body cares.

Ni siku ya tatu sana hakuna hata preliminary investigatory report. Hakuna aliyewajibika. Inasikitisha kwa kweli. Halafu hao watakaonyeshwa TBC nani atawaona na mgao wote huu wa umeme? Kinachosikitisha ni kuwa tunaelekea. Inakera.
 
Hawa jamaa ni wasanii sana, mimi nitahama nchi kama Mwamunyange atajiuzulu!
 
Kumbe mabomu yenyewe yalikuwa mapya, je ni ya kichina au ufisadi ulipita hapo?
 
Huyu jamaa ni Brig Gen kweli au?

It is amazing kuona jinsi alivyo-LOW, anaongea kama "Private Dadu"...

Kama huyu ndiye Mkuu wa Usalama na Utambuzi , basi hatuna JESHI bali MEN in UNIFORM!! It is shame!!!!
 
huyu jamaa ni brig gen kweli au?

It is amazing kuona jinsi alivyo-low, anaongea kama "private dadu"...

Kama huyu ndiye mkuu wa usalama na utambuzi , basi hatuna jeshi bali men in uniform!! It is shame!!!!
big shame
 
Nadhani hawakuja na jipya hao mabwana, nitarudi badae!

Pumzika tu mkuu....... wala hakuna la maana lolote, wamebadilisha tu maneno na kuonyesha michoro, ila ni ngonjera ile ile aliyoitoa jk.
 
Back
Top Bottom