Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema hakuna kiongozi ndani ya Jeshi hilo atakayejiuzulu kufuatia vifo vya watu 21 na majeruhi 300 katika milipuko ya mabomu huko Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, kwa kuwa nafasi hizo si za kisiasa..[/I]
Hiki kipande cha picha toka kwenye hiyo picha hapo juu. Huyu ni kiongozi wa ngazi ya juu kabisa wa jeshi anakwenda kuongea na waandishi wa habari baada ya janga kubwa lililosababisha vifo (janga ambalo imesababishwa na jeshi analoongoza) akiwa umevaa kiraia kama vile anaenda dukani! Anajua fikra habari hiyo itarushwa kitaifa na kimataifa lakini hajali! Cha zaidi anakupa tabasamu namna hii kama vile kuashiria "....mnaolalamika hamuwezi kutufanya chochote, sisi ndio sisi...hii ni issue simple to...!" Kama wanajeshi hawachukulii hili suala serious, hivi Tanzania wanajeshi wana issue gani nyingine ya kushughulikia na kuwajibishana? Maana hatuna vita sisi! Hivi huyu bwana kama ingekuwa ndugu yake kapoteza maisha kwenye hili janga na kwa sasa anakabiliwa na mambo ya mazishi angetoa tabasamu ya kebehi namna hii...?