JWTZ na taarifa ya Mabomu Gongo la Mboto

JWTZ na taarifa ya Mabomu Gongo la Mboto

EMT you said it all.

We are on one page Mkuu.

Much respect.

A
 
Mkuu EMT this is how great thinkers think...safi sana..

Tukateni issue huku tukiweka mbali Blah blah tu..tutakuwa hatuna tofauti na wakuu wetu...
 
hivi kutumia power point kuelezea siri za nchi ni sahihi? mi naona hapo anatoa ramani na siri nzito kwa kutumia hiyo power point ..........

na jana jk alisema kuwa g'mboto ndo kambi yenye silaha nzito....

wangefanya hivi na kwa wamiliki wa dowans ingekuwa powa kweli


Edson,
Ni kweli kabisa kusema waziwazi kuwa Gongo-la-Mboto ndipo depot ya kutegemewa na nchi kisilaha na kiulinzi-(Amiri jeshi mkuu kasema live on TV) halafu leo Military inteligence inatoa power-point presentation ya eneo ni sasa na kuwaelezea maadui wetu vichochoro na viambaza vipi wapitie kama hiyo kambi itaendelea kuwepo. HAYA NI MAKOSA MAKUBWA KIJESHI/KIULINZI, commando wa ki-nchi jirani-masikini anaweza kuja kwa mguu na kujua wapi Tanzania ikipigwa itasikia kipigo kitakatifu. Kila balozi ina muambata wa kijeshi Dar-es-Salaam na habari hii wameshaitia kibindoni kwa faida za nchi zao iwe kulipua kambi nyingine watuuzie silaha au kutushinda kijeshi.

Kuna mwan-JF anasema ipo google-map/gps hivyo jeshi limwage siri hadharani kwani hakuna cha kuficha?!! siyo kweli technolojia itakuwezesha kujilinda na kupata ushindi , bali ni busara na uweledi mkubwa wa makamanda ndio unaowezesha jeshi kushinda. Vietnam, Afghanistan majeshi yaliyokuwa na teknolojia ya juu yameshindwa.

Hapa kikubwa kilikuwa jeshi na serikali kusema iki-focus kuwa watafanya nini kuzuia maafa siku zijazo na wale waliohusika kujiuzulu nyadhifa zao serikali na kustaafishwa jeshini.

Pengine serikali inapata wakati mgumu kuwajibisha watu kutokana na kashfa kibao za DeepGreen, Kagoda, DOWANS, RADAR,MIGODi sasa kumvisha paka kengele inahitaji ujasiri ambao haupo hata kabla ya janga hili.

Kilichopo kwa vile JK alisema atafanya 'mageuzi makubwa' kwenye CCM na utendaji wake basi hapa ndipo pa kuonyesha 'Mageuzi' ktk serikali ya CCM juu ya UWAJIBIKAJI na VITENDO vyenye manufaa kwa taifa na usalama wa wa-Tanzania.
 
huyu jamaa anayetabasamu hapo aliyekaa kushoto ni nani?? kwa nini anatabasamu katika hali hii? au ndo system nzima ilivokaa?:spider:
 
Kambi ya Upinzani: Mwinyi, Mwamunyange wajiuzulu


* Yataka maghala ya silaha yahamishwe maeneo ya raia

Na Reuben Kagaruki

KAMBI ya Upinzani Bungeni imeeleza kushtushwa na taarifa za milipuko ya mabomu katika ghala la silaha la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na
imeshauri Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange kuwajibika kwa kujiuzulu nyadhifa zao.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga wa kambi hiyo, Bw. Joseph Selasini alieleza jana katika taarifa ya kambi hiyo kuwa viongozi hao wanatakiwa kuwajibika kutokana na milipuko ya mabomu iliyotokea Gongolamboto, jijini Dar es Salaam, juzi usiku.

Bw. Selasini alisema; "Dkt. Hussein Mwinyi alikuwa Waziri wa Ulinzi wakati wa maafa ya Mbagala na Jenerali Mwamunyange alikuwa Mkuu wa Majeshi. Maafa ya Mbagala yalitokea chini ya dhamana na au usimamizi wao. Na mara baada ya maafa hayo, Waziri Mwinyi na Jenerali Mwamunyange waliahidi taifa kwamba maafa ya aina hii hayatatokea tena. Sasa yametokea," alisema na kuongeza;

"Ahadi yao ilikuwa sio ya kweli, viongozi hawa hawana budi kuwajibika kwa hiari yao wenyewe au kuwajibishwa kama itahitajika."

Bw. Selasini aliongeza kusema kwamba hadi leo hakuna taarifa yoyote rasmi iliyowahi kutolewa hadharani kwa wananchi au kwa wawakilishi wao bungeni juu ya chanzo cha maafa hayo.

Kambi hiyo imewapa pole ndugu, jamaa na wananchi wote wa Tanzania kutokana na maafa yaliyosababishwa na mabomu hayo.

"Mamlaka zote za umma zinazohusika zichukue hatua za haraka kuhakikisha wananchi wote walioathirika na maafa hayo wanapatiwa huduma zote wanazohitaji katika kipindi hiki," alisema Bw. Selasini.

Alisema ni muhimu kwa vyombo vya usalama kuhakikisha ulinzi wa mali za wananchi katika maeneo yote yaliyoathirika ikiwa ni pamoja na kuwapatia matibabu.

Taarifa ya kambi ya upinzani ilieleza kuwa tukio hilo ni la kushtusha na kusikitisha hasa kwa kuzingatia kuwa haijapita miaka miwili tangu tukio la aina hiyo litokee Mbagala, Dar es Salaam.

Tukio hilo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 30 na uharibifu wa mali.

"Milipuko ya Gongo la Mboto inaonesha dhahiri kuwa Serikali ya Awamu Nne ya CCM haijajifunza lolote kutokana na maafa yaliyotokea Mbagala mwaka juzi," alisema Bw. Selasini na kuongeza;

"Kama Serikali ingejifunza kutokana na maafa hayo ingeshachukua hatua za dharura na za haraka kuhakikisha maafa ya aina hiyo hayatokei tena."

Bw.Selasini alishauri maghala yote ya silaha na mabomu yaliyo karibu na maeneo wanayoishi raia nayahamishwe maeneo wanayokaa raia.

Kambi hiyo imependekeza iundwe tume huru ya uchunguzi au kamati teule ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuchunguza kwa kina chanzo cha milipuko ya Gongo la Mboto.

Kaimu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Bw. Tundu Lissu alisisitiza hoja hiyo akihoji kama viongozi hao walijifunza kitu ni hatua gani walizichukua ili kudhibiti hali hiyo.

Hata hivyo alisema ubovu wa masuala ya kisera na kiutawala ndiyo yanayosababisha kuwepo kwa matukio kama hayo hali ambapo alihoji kwa nini maeneo kama hayo ya kutunzia silaha yawekwe katika maeneo ya makazi ya watu.

Kutokana na hali hiyo alisema ni wakati mwafaka sasa kwa Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa Majeshi wajiuzulu au waachie nyadhifa zao kwani inaonesha wazi kuwa katika usimamizi wao wa masuala ya kijeshi kuwa nchi haiko salama.




10 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Nadhani wapinzani hamna subra,badala ya kukaa na kufariji walioumia na kutafakari tayari mnatafuta umaarufu humo,mabomu yametokea jana usiku,hamjajua chanzo chake,tayari mmekurupuka,nadhani mnaomba maafa yatokee ili mlaumu serikali watu wawaone mnafanya kazi, Ningefurahishwa kama mngezikataa Sh 90,000,000/= mlizopewa kununua magari zitumike kuhamisha hayo maghala ya silaha. Saa mnapopewa rushwa na serikali kama hiyo na nyingine mnakaa kimya lakini janga likitokea tu mbio kwenye vyombo vya habari utafikiri mlikaa kuombea litokee
February 17, 2011 11:03 PM
blank.gif

Anonymous said... Ni lazima Mwinyi na Mwamunyange wajihuzuru nyadhifa zao.Tusibabaishe mambo kabisa.Mambo ya siasa juu ya jambo hili hayahusiki hakuna CHADEMA,CCM wala CUF.Cha msingi raia wawe na mshikamano kuwaondoa madarakani Mwinyi pamoja na mwamunyange.
February 17, 2011 11:13 PM
Sung said... Hakuna haja ya subira, watu wamekufa, kuna haja ya subira tena? Baada ya mabomu ya Mbagala kuua watu, tulifanya subira sasa hivi hatudanganyiki. Na wewe unataka subira gani? Unataka mpaka yaripuke mengine kule Kigamboni na kuua tena?
February 17, 2011 11:36 PM
blank.gif

Anonymous said... mtangulizi wa maoni inaonesha huna akili nzuri, na hujui kufikiri kwa kina. msemaji ameshaonesha masikitiko yake na vielelezo vya kwa nini tukio kama hili, linatokea tena mara ya tatu mfululizo bila utekeleza wa kuzuia lisitokee.
anapoieleza serikali na wahusika wajiuzulu haina maana hajali maafa, hata mimi nisiye wa chadema siungi mkono ujinga kama wa mtangulizi wa maoni.
nakubaliana viongozi wahusika wajiuzulu kuonyesha masikitiko ya uzembe wao au watendaji wao kwa sababu, viongozi hao ndio walitakiwa wawe wa kwanza kutafuta mbini mbadala baada ya tukio la maafa ya awali Gongola mboto huko huko, mbagala na tena gongo lamboto.
nadhani msemaji wa awali ni mbumbu wa kufikiri ambaye ni sawa na mzazi ambaye mtoto wake kikojozi anapoharibu godoro, hafikirii wazo la kukomesha tabia itakayomgharimu magodoro, harufu na afya ya mtoto.
nina imani si kila wazo la wapinzani ni baya, yapo mengine mazuri sana, ila kwa uzembe na ujinga, tunayakataa.
Juzi wametuambia (serikali kupitia polisi) tunaua watu tukakataa, baada ya siku moja mungu akathibitisha maneno yao kwa wawili kifo cha mbarali tukakanusha; bado mungu anaendele kuthibitisha kwamba; serikali inaua watu kwa uzembe wake wa kutowajibika na kutoa haki.
wahenga kila siku wanasema mshahara wa dhambi ni mauti, uchakachuaji na wizi wa kura ni mauti ya wananchi.kubalini kosa na kuomba msamaha kwa kuwadharirisha wachungaji na mashehe waliokemea tabia ya mauaji na kuwaomba msamah; hali itakuwa swali.

February 17, 2011 11:55 PM
blank.gif

eng. mwakapango, E.P.A said... kuna mambo ya kusubiri lakini siyo hayo yanayosababisha watanzania kupoteza maisha yao. hata hivyo hiyo ndiyo kazi kubwa ya serikali kivuli. mmechukua hatua stahili ya kuishauri serikali JK apime mwenyewe na atoe uamuzi utaomsaidia yeye ili kuepukana na matukio ya namna hii.
February 18, 2011 4:33 AM
blank.gif

Anonymous said... Mchangiaji wa kwanza unataka subira. saafi saaana.

Maneno yako ya kutaka pawe na subira yangekuwa na maana zaidi kama mmoja wa ndugu zako angekuwa ni mmoja wa waliokufa, ingefaa zaidi yakukute wewe mwenyewe kisha utwambie kuwa tuwe na subira hapo tungekuelewa.

Watu wamekufa kwa uzembe kisha unasema tuwe na subira ya nini? Hili si jambo jipya maana miaka miwili iliyopita yalilipuka Mbagala, sasa hata MAKABURI hatujajengea yanalipuka Gongolamboto, na Viongozi ni walewale, wala hawashtuki!, hawaoni kama ni tatizo, na kama wataendelea kubakia madarakani tutazamie milipuko mingine itakayouwa Watanzania wengine wengi tu, maana kati yao hakuna anayeonesha kujali na kuzuia ajali za namna hii zisitokee. Hata Baba yake Hussein, Mzee Mwinyi alishaonesha mfano kwa kujiuzulu nafasi yake ya Uwaziri wa mambo ya ndani pale yalipotokea mauaji ya watu Mkoani Shinyanga, alionesha ujasiri na kuwajibika kama Kiongozi. Nawe Mwana fuata nyayo za BABAKO,JIUZULU japo ni ngumu kuachia ulaji!

Viongozi wetu wengi leo hawapo tayari kuwajibika kwa makosa yao na au makosa yanayofanywa na wasaidizi wao, Tumemuona Hosea, Mwanyika,Meghji, Idrisa( EPA, IPTL, KAGODA, MWANANCHI, MEREMETA, NEC, IGP, RICHMOND, DOWANS, RTC, NDC, NMC, NASACO, TICTS, BODI YA PAMBA, BODI YA SUKARI, BODI YA KAHAWA, RADA, ATC, TIPPER, TRC, KAMATA, UDA, TAZARA NTC, NK) na wengi wengineo na wakati mwingine hata mamlaka zilizo juu yao zimeshindwa kuwawajibisha maana WANAKULA NAO. MAMBO YA KULINDANA!

February 18, 2011 5:21 AM
blank.gif

Anonymous said... Wote mliotoa maoni kumpinga aliyetoa maoni ya mwanzo inaelekea akili zenu mbovu,huyo jamaa kasema wabunge hao wa upinzani wangekataa mailioni ya mapesa waliogawana juzi,kila mbunge million 90 za kununulia magari ili zihamishe maghala ya silaha mbona hilo hamlisemei.wapumbavu wakubwa nyie,watu wanagawana pesa huko bungeni za kununulia magari,hamlioni hilo,mnalalamikia ajali,kulipuka kwa maghala hata huko Ulaya huwa yanalipuka tu. nyie ni wapumbavu sana hao wabunge wenu wanaishi maisha ya peponi wewe unashindia mlo mmoja unaishia kuandika kwenye mitandao mambo ya hovyo
February 18, 2011 9:19 AM
blank.gif

Anonymous said... Mtu akijamba pia mtamwambia ajiuzulu,mabomu ni ajali kweli,inaweza ikatokea wakati wowote tu,nashangaa wanaowaambia wataalam wa jeshi wekeni air condition,mnashangaza sana kila mtu anajifanya anajua,mngekuwa wajuzi hivyo nchi ingeoza hii?
February 18, 2011 10:16 AM
blank.gif

Anonymous said... Sitegemei kama Tanzani kuna watu uelewa wao ni mdogo kiasi hicho. Hivi mtu unapotetea uzembe kama huu uliogharimu damu za watu ni kitu gani basi utakachosema viongozi wajuzuru. Tunawajeshi wengi wazuri, tunaviongozi wengi wazuri watachukua nyazifa zao, Mkuu wa Majeshi na Waziri wa Ulinzi siyo miungu. Richimondi haikumwaga damu ila viongozi wakubwa kabisa 3 walijiuzuru. Leo tuendelee kucheka na na hawa waliomwaga damu ya Watanzania wenzetu. Tushikamane ili viongozi wawajibike. Wahusika lazima wawajibike. Naomba watu mnaotoa hoja mkitetea yaliyotokea mkumbuke kuwa si mara ya kwanza, yalitokea kwanza mbagara, sasa utaniambie hii ni bahati mbaya basi Duniani hakuna uzembe.
February 18, 2011 10:46 AM
blank.gif

Anonymous said... Wewe ndugu unayetukana watoa maoni kuwa ni wapumbavu wakubwa basi mungu akusamehe kwa kuwa hujui utendalo. Sitaki kukurudishia matusi yako lakini naomba uwe na nidhamu na pia lugha nzuri unapotoa maoni yako hata kama hayakupendezi tuwe na tabia ya kuvumiliana. Kwa kuwatetea viongozi wa serikali katika hili ni udumavu wa akili na inaonyesha mtu wa namna hiyo ana maslahi ya karibu na Viongozi hao wazembe. Swala la kulinganisha maafa ya Gongo la Mboto na mil, 90 za wabunge ni kukosa mweleko na hoja. Please get informed that pesa hizo wabunge wamekopeshwa na watalipa kupitia mishahara na posho zao. Ni sawa na wanafunzi wanaokopeshwa sasa useme wasikopeshwe eti fedha zihamishe maghala ya silaha kwani hakuna fedha zingine za kufanya kazi hiyo? Mbona juzi pinda ametemba kuwa wanakusanya bil 400 kila mwezi zinakwenda wapi? Wewe jamaa mchangiaji uache kufikiri kifisadi inaonyesha hao mafisadi wa serikali ya Tanzania ni baba zako au mama zako. Ipo siku tutawatafuta na kuvichoma vibenki vyenu mnavyoanzisha kutokana na kuiba fedha za watanzania. Kumbuka Kaka wa Mke wa Rais aliyefukuzwa huko Tunisia alikuwa na benki kubwa iliyotokana na wizi wa dada yake akiwa ikulu na juzi waandamanaji wameichoma moto. Suala la Mwinyi na Mwamunyange kuachia ngazi halina mjadala na wanapaswa wafanye hivyo au Kikwete awafukuze kazi haraka na kuweka wengine watakaolinda watanzania. Nawaunga mkono viongozi wa upinzani kushinikiza hilo na kazi yao nikulishikia bango mpaka wang'oke ama Rais alazimishwe kuwang'oa. Mbona Lowassa alijihudhuru kwa kosa ambalo hakulifanya iweje hawa waliotuahidi katika tukio la awali kuwa halitatokea tena jingine washindwe kujiuzulu. Ili serikali ipate heshima kwa wananchi wake hawa wasisubiri maandamano bali wawahi wenyewe kuchia ngazi. Kuwatetea hawa ni kutetea muaji yaendelee kwani inaonyesha silaha hizo za kivita zimekwisha muda wake na zinastahili kuteketezwa lakini jeshi wataalamu wake hawajui hilo. Mbona jeshi la leo si la akina Mwita Kyaro hili lina wasomi iweje mambo haya yatokee kama sio uzembe wa mkuu wa majeshi.
WAZIRI NA MKUU WA MAJESHI ONYESHENI KUKERWA NA JAMBO HILI KWA KUACHIA NGAZI NYIE WENYEWE MTAPATA HESHIMA

February 18, 2011 11:48 AM
 
Watu 20 wathibitika kufa 184 kujeruhiwa


Na Waandishi Wetu

WATU 20 wamekufa na wengine 184 kujeruhiwa kutokana na milipuko ya mabomu iliyotokea kwenye maghala ya kuhifadhia silaha katika kambi ya
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Gongolamboto jijiji Dar es Salaam juzi siku.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Dar es Salaam nchini, Mrakibu Msaidizi (ASP) Advera Senso aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa miili ya waliokufa imehifadhiwa katika hospitali za Amana, Muhimbili na Temeke.

Awali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema bungeni kuwa idadi ya watu waliokufa ilikuwa 17 na kuwa milipuko ya mabomu hayo ilisababisha madhara makubwa ya majeruhi, watoto wadogo kupotea na uharibifu mkubwa wa mali.

Bi. Senso alisema wahanga wa tukuio hilo wamepewa hifadhi ya muda katika uwanja wa mpira wa Uhuru, Viwanja vya Maonesho ya Sabasaba, Kituo cha Polisi Tazara, Buguruni na Msimbazi.

Aliwataka watu waliopotelewa na ndugu kufika katika vituo hivyo ili kuwatambua.

"Jeshi la polisi linapenda kuwasisitiza wananchi kuwa watulivu na kuendelea na kazi zao kama kawaida kwa sababu hali hiyo tayari imedhibitiwa kwa sasa (jana mchana) na kusingekuwa na milipuko inayoendelea," alisisitiza Bi. Senso.

Alitoa mwito kwa wananchi kutoa taarifa pindi wanapona kitu ambacho si cha kawaida katika maeneo yao kupitia namba 0774-039029, 0782-114515, 0782-60334 na 0755-756410.
 
Wabunge wahofu siasa, hujuma jeshini


Na Waandishi Wetu

BAADHI ya wabunge wameonesha wasiwasi wao kuhusu ulipukaji wa mabomu na kusema kwamba ni uzembe wa serikali hujuma na huenda
siasa zimeingia ndani ya jeshi.

Wabunge hao kwa nyakati tofauti waliyasema hayo wakihojiana na Majira baada ya Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda kuahirisha Kikao cha Bunge akisema kwamba hali inatisha, Watanzania wote wako katika hofu hawajui familia zao ziko wapi, hivyo hawawezi kuendelea na shughuli za bungeni.

Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbles Lema (CHADEMA) akitoa maoni yake kuhusu janga hilo alisema kuwa kutokea kwa milipuko ya mabomu mara kwa mara katika kambi za kijeshi ni uzembe wa serikali na inaonesha kuwa ndani yake kuna masuala ya kisiasa.

Alisema kuwa suala hilo linaonesha kuwa kuna mtu anayetafutwa ndani ya uongozi ili aweze kuangushwa na kubainisha kuwa siasa za nchi hii zimeenda ndani zaidi hadi kufikia jeshini.

"Ukifuatilia zaidi unaweza kukuta walinzi wa maghala hayo ya silaha hawajafa au kujeruhiwa na kama itakuwa hivyo, basi kuna walakini kwa sababu walitakiwa kuwa wa kwanza kufa," alisema Bw. Lema ambaye pia ni waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani.

Alisema kuwa kumekuwa na tatizo kwa nchi hii pindi inapotokea matukio kama haya serikali inakimbilia kuunda tume na kusema kuwa basi tume hiyo itakayoundwa ichunguze kwa makini zaidi na kubaini kilichotokea.

Naye Mbunge wa Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP, Bw. Augstino Mrema kwa upande wake alisema kuwa rais achukue jukumu la kuwawajibisha baadhi ya viongozi wanaosimamia masuala ya kijeshi kwani wameonesha kutowajibika kikamilifu katika kusimamia usalama wa maisha ya wananchi.

Alisema kuwa wananchi walidhani kuwa Serikali ilijifunza kitu kwa tukio la Mbagala la kulipuka kwa mabomu ambayo yaliua watu wengi lakini inaonesha haikujifunza kitu hivyo wahusika lazima wawajibike.

Alisema kuwa Tanzania ijifunze kwa nchi zingine zilizoendelea kuwa ikitokea hali kama hiyo basi wahusika huwajibika kutokana na matukio kama hayo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF), Bw. Rashid Mohamed alisema kuwa inaonesha kuwa Tanzania haina uwezo mzuri wa kudhibiti silaha.

Alisema kuwa ipo haja kwa serikali kuchukua hatua za dharura kuangalia hali hiyo kwani inaonesha kuwa nchi haiko katika hali nzuri.

"Serikali ambayo ina amani kwanini inakuwa na silaha kama hizo ambazo ni nzito, utunzanji wake unaonesha kuwa si mzuri na umekuwa ukihatarisha maisha ya watu, iliangalie hilo na kujifunza kitu kutokana na matukio," alisema.

Hata hivyo, alisema wananchi walijua serikali ilifanya tathmini na utafiti wa kutosha kwa tukio la Mbagala mwaka juzi na kujifunza kitu ili hali hiyo isijitokeze tena lakini inashangaza kuona kuwa tukio kama hilo linajitokeza tena kwa mara nyingine tena na kupoteza maisha.

Awali Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda akitoa taarifa ya maafa hayo alisema mlipuko ulianza saa mbili usiku katika maghala ya Jeshi la Ulinzi ambapo maghala 23 yameteketea yakiwa na silaha pamoja na mchanganyiko wa mabomu.

Alisema juhudi zilifanyika na viongozi wa jeshi baada ya milipuko kupungua na kubaini mabweni mawili ya jeshi hilo yaliharibiwa vibaya, magari mawili yaliteketea na watu zaidi ya 17 walifariki dunia.

Bw. Pinda alisema maiti waliofikishwa Hospitali ya Amana ni 13, Muhimbili wawili na Temeke wawili na kati ya maiti hizo tatu waliyoka Kitunda.

Alisema majeruhi 145 hadi asubuhi lakini upo uwezekano wa kuongezeka marehemu na majeruhi baada ya kufanya ukaguzi katika maeneo ambayo usiku hayakufikika.

Waziri alisema zaidi ya watu 4,000 wamehifadhiwa Uwanja wa Uhuru, wakazi waliojirani na maeneo ya matukio wanatakiwa kupisha ukaguzi kujua hali ilivyo.

Alisema kuna mabomu yaliangukia Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius, walipendekeza uwanja ufungwe kwa muda na ndege zilihadharishwa kutotumia uwanja huo.

"Rais ameitisha kikao cha dharura cha Ulinzi na Usalama wa Taifa na jeshi liunde tume ya kuchunguza tatizo hilo ili kubaini chanzo na hatua stahiki zianze kuchukuliwa," alisema na kuwapa pole wote kutokana na mtikisiko huo.




6 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Ni kweli,Rashid umenena.Kwa nini tukae na mabomu kama nchi yetu ni amani?????
Tunaomba viongozi wenye nafasi hizo wajihuzuru mapema bila kulazimishwa.Nasikia tuna usalama wa taifa lakini mimi naona wanakula tu mshahara lakini hawafanyi kazi yoyote.Tunashuhudia mambo kadhaa ambayo nilidhani usalama watadhibiti kabla hayajatokea lakini wanashindwa.Nchi yetu haina ulinzi,watu wananenepa tu na kufungua biashara mtaani badala ya kuwalinda wananchi.

February 17, 2011 11:21 PM
blank.gif

Anonymous said... jamani tunawataka viongozi wawajibike kwani hii serikali yetu imetushosha kila kitun kinaenda hovyohovyo lakini ndio vijitu vimeng'ang'ania madaraka pamoja na kuwa vimechoka!!!!!!!!!!!!!!!!!!sasa unategemea shimbo ana mpya? unategemea mwinyi ana jipya? au makamba wa ccm ana jipya? au kikwete anaegoma kumtaja rostam kama mmiliki wa dowans ana jipya?

WATANZANIA TUMEKWISHA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!KHANGA NA FULANA INCLUDING KOFIA ZIMETUMALIZA JUZI WAMETOKA KUUA ARUSHA,IKAFATA MBARALI,IKAFATA HIFADHI YA WANYAMA NA LEO GONGOLAMBOTO....WATANZANIA TUSITAFUTE MCHAWI TUKO NAE HAPAHAPA HATA MALOW MWANAMUZIKI ALIHAMASISHA SANA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

February 17, 2011 11:42 PM
blank.gif

Anonymous said... Manenoyanayosemwa ni mengi lakini technically lazima tujiulize kwa nini mabomu yanalipuka!!

1. Je ni kwa sababu muda wake umekwisha hivyo yalihitaji kuharibiwa?

2. Ni kwa sababu hayakutunzwa vizuri kwa maaana ya unfavarorable temperatures, etc?

3. Je aina ya mabomu tuliyotunza hayakuwa na kiwango kizuri cha utengenezaji, na hivyo kulipuka bila wanajeshi wetu kujua ( manufactures default?

4. Au kuna tensions kati ya jeshi na serikali kuhusu kuyateketeza hayo mabovu; kwa maaana ya budget

6. Suala la neighourhood si la msingi sana kwa sasa kwa maana hata kama kambi ingekuwa kilometres elfu ngapi mbali na makazi ya wanaichi; bado mabomu hayatakiwi kulipuka tu kwani kuna wanajeshi wanatakiwa wawepo eneo hilo

Jeshi linatakiwa lijibu maswali haya kikamilifu

February 17, 2011 11:55 PM
blank.gif

Anonymous said... SERIKALI IMECHEMKA. TUME NDIO WIMBO WA KILA SIKU.WATU WANAKULA POSHO.WANAOMBA WAKIMALIZA HICHO WANACHOKIITA UCHUNGUZI , WANAPIGA JALAMBA KUSUBIRI JANGA LINGINE LITOKEE WACHAGULIWE TENA KWENYE TUME NYINGINE. " EWE MWENYEZI MUNGU FUNGUA FAHAMU ZA HAWA VIONGOZI WETU WEKA UPENDO NA UZALENDO WA KWELI NDANI YA MIOYO YAO, ILI MAMBO WANAYOYAPANGA WAYATEKELEZE , YASIISHIE KWELNYE MAFAILI TU, TUNAHITAJI KUONA KUWA WANATUJALI, NA SIYO KUTUUPUZA NA HUKU WAO WAKINEEMEKA, JINSI WALIVYO NI WEWE MUNGU ULIWAJALIA WAWE HIVYO WASIJE WAKAJIVUNA NA KUONA KUWA WAO WAMESOMA SANA. EWE MUNGU , UTUSIKIE, AMANI ULIYOTUJALIA TUIIHIFADHI KWA JINSI INAVYOPASWA, NA VIONGOZI KUSIMAMA KATIKA NAFASI ZAO SAWASAWA.AMINA." VILE WANAPASWA KUFANYA.ZIRI JIUZULU.
February 18, 2011 1:31 AM
blank.gif

Anonymous said... well,
kwa muda watanzania watazungumzia mambo ya mabomu na kusahau mengine.. mi sisemi sana. but i know it is conspiracy

February 18, 2011 3:52 AM
blank.gif

Anonymous said... Mungu kakasirika baada ya Maaskofu kubariki dhambi za Slaa kuchukua mke wa mtu na wao badala ya kukemea wanasema ni masuala binafsi,sasa hii ni adhabu na zingine zinakuja,mnaua maalbino kutafuta pesa,mnadhulumu masikini na mahakama hazitoi haki,ole wenu tubuni kwa Mungu.
February 18, 2011 9:24 AM
 
JK ataka waliokimbia warudi Gongolamboto


Na Waandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete amesikitishwa na mlipuko wa mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Brigedia 511 Gombo la Mboto Dar es salaam na
kuweka wazi kuwa tukio hilo ni maafa makubwa na la kushtua.

Pia Rais Kikwete amewataka wananchi kutulia na kurejea kwenye makazi yao kuendelea na shughuli zao kama kawaida kuwa kipindi cha hatari kimepita na kuwataka kupuuza taarifa za uzushi kuwa mlipuko zaidi utatokea.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutembelea kambi hiyo na kujionea uharibifu mkubwa kambini hapo jana, Rais Kikwete alisema serikali imechukua hatua za haraka juu ya tukio hilo hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi.

"Nilipata taarifa za tukio hilo jana usiku, na nikataka nikutane na Mkuu wa Majeshi lakini akanitaarifu kuwa wanaendelea na harakati za kuangalia tatizo hilo. Baadaye saa tisa usiku nilikutana naye na kunipa taarifa za tukio hilo.


"Ni maafa makubwa, siyo jambo dogo ni la kushtua, lakini kipindi cha hatari kimepita, wananchi wasiwe na wasiwasi, wapuuze taarifa kwamba milipuko zaidi itaendelea hizo ni taarifa za radio mbao, hakuna mabomu yatakayoendelea," alisema Rais Kikwete na kuongeza

"Leo (jana) mchana nitakuwa na kikao cha Kamati ya Usalama na baada ya kumaliza nitatoa taarifa," alisema.

Rais Kikwete ambaye alifika katika kambi hiyo saa 6:00 mchana, alisema kambi ya Gombolamboto ndio ghala kubwa ya kuhifadhia silaha na kwamba kulipuka kwa kambi hiyo ni jambo la kushtua, lakini bado nchi iko salama kwa vifaa vya kutosha.

Waziri wa Ulinzi

Hata hivyo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dkt. Hussein Mwinyi, hakuwa tayari kusema lolote juu ya tukio hilo kwa maelezo kuwa aliyosema Rais Kikwete yanatosha.

"Siwezi kusema lolote aliyokwishasema mheshimiwa Rais yanatosha kwa sasa," alisema Dkt. Mwinyi.

Luteni Generali Abdulrahaman Shimbo

Akijibu maswali ya waandishi Habari Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo, alisema licha ya mlipuko huo hali ya usalama wa Taifa kiulinzi ni nzuri na kwamba wananchi wasifikiri kwamba Jeshi hilo linaweza kuwa na upungufu wa silaha kutokana na tukio hilo.

Alisema tayari Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange ameunda kikosi cha uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo na kwamba taarifa kamili itatolewa baada ya kazi hiyo kukamilika.

Alisema watu 20 walikuwa wamepoteza maisha kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa hadi jana mchana huku zaidi ya 300 wakiwa wamejeruhiwa na kwamba mlipuko wa mabomu yaliyolipuka yanaweza kusafiri hadi umbali wa kilomita 20 lakini yakiwa kwenye mtutu wake.

Alisema kazi ya kukusanya mabaki ya mabomu katika makazi ya wananchi ilitarajiwa kuanza muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuondoka katika kambi hiyo na kuwaomba wananchi wasiwe na wasiwasi kwa kuwa mabaki hayo hayawezi kulipuka tena bila shinikizo mkubwa.

"Nawaomba wananchi wasiwe na wasiwasi, hayo mambomu hayawezi kulipuka tena , hata kama yapo katika makazi yao, lakini wasiyacheze wala kuyagongagonga.

Kazi ni kubwa sana, niwahakikishie, lakini uko wanakoishi watu ndipo tutakapoanzia kukusanya mabomu hayo, tunayo orodha ya wananchi waliotupigia simu," alisema Luteni Jenerali Shimbo.

Alipoulizwa kuhusu chanzo cha tukio hilo kwa kuzingatia kuwa hii ni mara ya pili kwa mabomu kulipuka ndani ya kipindi cha miaka miwili alisema matukio hayo hayalingani wala hayafanani kwa kuwa yana vyanzo tofauti.

Alisema mlipuko wa Aprili mwaka 2009 ulitokea katika kambi ya Mbagala ulitokea wakati wanajeshi wakiwa kazini lakini tukio la juzi usiku ulitokea usiku wakati mabomu hayo yakiwa yametulia.

"Kwanza haya matukio hayafanani, tukio la kwanza ni tofauti na tukio hili, la kwanza lilitokea watu wakifanya kazi ndani ya ghala, hili limetokea usiku ghala likiwa peke yake, msije mkalinganisha matukio haya," alisisiza.

Alipotakiwa kueleza iwapo JWTZ itahitaji msaada kutoka nje wakati wa uchunguzi wa tukio hilo na muda wa uchunguzi na kutoa taarifa hiyo alisema watalamu wa jeshi hilo wanatosha kufanya kazi hiyo lakini akakiri kuwa ni kazi kubwa.

"Uchunguzi wa kitaalamu ni muhimu sana, tunao wataalamu wa kwenda kuchunguza, tunajua ni ghala namba tano ndio lilianza kulipuka, tutachgunguza vitu vilivyokuwa ndani ya gahala hilo na takwimu zake, kutoka hapo tutajua kila kitu, ndio maana tumezuia watu kuingia pale ili kutoharibu ushahidi wakati wa uchunguzi," alisema.

Alipoulizwa iwapo mlipuko wa mabamu hayo umetokana na muda wake kupita, alisema tarifa hizo ni za uzushi kwa kuwa tukio hilo limetokea siku tatu tu baada ya ukaguzi uliobaini kuwa silaha hizo ni salama.

Alisema baadhi ya sialha hizo ni za septemba mwaka jana hivyo hakuna wasiwasi kuhusu ubora wake.

Alipotakiwa kueleza vitu vinavyoweza kusababisha mabomu kulipuyka alisema vipo vyanzo vingi ikiwemo moto na radi na kwamba baada ya uchunguzi wa kina watajua chanzo halisi ya tukio hilo na kwamba ya hewa ulikuwa safi.

Alipoulizwa kuhusu umbali ambao mabomu hayo yanaweza kwenda alisema ni kilomita 22 ikipigwa kwenye mzinga wake na kwa mlipuko kama ulivyotokea inaweza kuwa kilomita tano hadi 11.

Alisisitiza kuwa JWTZ haina mpango wowote kuhamisha kambi hiyo kwa kuwa ni muhimu kwa ulinzi na usalama wa Taifa na kuwaomba wananchi kuheshimu sheria ya kukaa jirani na kambi za jeshi kwa kuwa lipo kwa ajili ya usalama wao wenyewe na kwamba kambi hiyo ilijengwa mwaka 1971.

Alisema wakati kambi hiyo ilipojengwa eneo hilo lilikuwa pori huku kukiwa na Shule ya Sekondari ya Pugu pekee na kwamba wananchi walifuta kambi hiyo lakini si jukumu lao kuwahamisha na kwamba wanalazimika kuishi nao jirani kama Jamii.

Alisema zipo uchunguzi wa aina mbili ikiwemo ya kwao kama JWTZ na ile ya serikali ambayo hata wao watahojiwa kama wahusika.

Awali akitoa taarifa ya tukio hilo kwa Rais Kikwete Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Kanali Aloyce Mwanjile, alisema jumla ya gahala 23 za silaha ziliteketea, magari mawili ya maji, magari mawili mapya kabisa ambayo yalikuwa hayjaanza kufanya kazi pamoja na Ofisi zote za kambi ziliathirika licha ya zile zilizoteketea kabisa.

Alisema pia mabweni ya askari iliteketea na vitu vyote huku mwanajeshi moja akijeruhiwa mkononi.

Alitaja maeneo ambayo mabomu hayo yalisambaa kuwa ni Pugu Kajiungeni, Yombo Vituka, Tabarta, Gombo la Mboto, Kivule na maeneo ya Tazara.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa JWTZ Luteni Kanali Kapambala Mgawe,alisema kati ya watu 20 waliothibitishwa kupoteza maisha katika tukio hilo 13 walikufa kwa mabomu hayo huku saba wakipoteza maisha kutokana na mshtuko.

Alisema hadi jana mchana jumla ya watu 300 waliripotiwa kujeruhiwa na kuwaomba wananchi kupata taarifa sahihi kutoka katika Jeshi hilo au viongozi wa serikali na si za mitaani zinazoweza kuwachanganya.

Majira ilishuhudia umati wa watu wakiendelea kuwatambua watoto na ndugu zao katika uwanja wa Uhuru huku wadau mbalimbali wakiwemo chama cha Msalaba Mwekundu, Kampuni ya Vinnjwaji sayona, Tume ya Taiga ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) zikitoa misaada ya aina mbalimbali.

Serikali iliwaomba wananchi ambao wanatafuta ndugu zao au wale walio na watoto wasiowajua kuwapeleka katika uwanja huo au vituo vya polisi ili waweze kutambuliwa na ndugu zao.

Imeandaliwa na John Daniel, Benjamin Masese na Rabia Bakari

 
Lipumba ataka uchunguzi huru Gongolamboto


Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimetoa taarifa ya kusikitishwa na tukio la milipuko ya mabomu ambalo ni la pili kutokea katika kambi za Jeshi la Wananchi na
kuomba uchunguzi huru wa tukio hilo.

Kimeitaka serikali kuwaomba nchi marafiki wa kijeshi na zile ambako silaha hizo zilinunuliwa kutoa msaada wa watalaamu kufanya uchunguzi ili kubainisha sababu ya kulipuka wakati muda wake wa matumizi haujaisha.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema milipuko hiyo imesababisha mtafaruku mkubwa kwa wakazi wa maeneo ya jirani na kambi hiyo, ambapo mamia ya wakazi hao wamegeuka kuwa wakimbizi wa ndani na kuweka kambi za muda maeneo ya kambi ya kikosi cha kutuliza ghasia, Uwanja wa Taifa, vituo vya polisi kama Buguruni na wengi wao kuhifadhiwa kwa ndugu na jamaa.

"Tukio hili linachukua taswira ya tukio la Jumapili ya Aprili 29 mwaka 2009, ambapo, milipuko ya mabomu ilitokea katika ghala la kuhifadhia mabomu katika kikosi cha 671 KJ, Mbagala na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 20 na wengine wengi kupata ulemavu wa maisha, pamoja na uharibifu mkubwa wa majengo na maeneo ya makazi," alisema Profesa Lpumba.

Alisema pamoja na ahadi mbalimbali kutoka kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi ya kuhakikisha kuwa tukio kama hilo halitatokea, tayari tukio kubwa zaidi ya lile la Mbagala limetokea.

Alisema waziri huyo alionesha ukaidi pale alipotakiwa kujiuzulu kutokana na uzembe uliofanyika ndani ya wizara yake, ya kushindwa kuweka mazingira salama yasiyoweza kuleta madhara kwa wananchi.

"CUF tunahuzunishwa na uzembe huu unaoendelea kujitokeza kwa makusudi na kuonesha dharau ya kutothamini uhai wa raia wa nchi hii ambapo dhamana ya jeshi la Ulinzi ni kulinda mipaka ya nchi na raia wake," alisema Profesa Lipumba.

Alisema chama chake kwa mara nyingine kinamtaka Dkt. Mwinyi na Mkuu wa JWTZ, Jenerali Davis Mwamunyange kuwajibika kwa kujiuzulu mara moja kutokana na ukaidi na kushindwa kudhibiti madhara yaliyojitokeza siku za nyuma.

"Tunamsihi Waziri Mwinyi kulinda heshima yake kwa kufuata nyayo za baba yake Mzee Ali Hassan Mwinyi alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alipojiuzulu kutokana sakata la mauaji mkoani Shinyanga," alisema Profesa Lipumba.

Alisisitiza kuwa matukio hao yanasababisha maafa yakiwemo, kupoteza nguvu kazi ya taifa (ambayo ni vifo), kupoteza uwezo kuzalisha kutokana na ulemavu wanaoupata na kusababisha kuwa tegemezi.

Alisema hali hiyo inaliingizia taifa hasara ya ununuzi wa vifaa vingine mbadala vya kijeshi ya vilivyoangamia pasipo matumizi stahiki, jamii husika iliyoathiriwa kupoteza mali zao na kuchanganyikiwa kisaikolojia hadi kufikia kushindwa kumudu maisha.

"CUF tunaungana na Watanzania wote kwa msiba huu mzito wa kitaifa na kuwapa pole familia, ndugu na jamaa za wananchi waliopoteza maisha yao kutokana na milipuko ya mabomu hayo na kuwataka wawe na subira katika kipindi hiki cha majonzi, na kumuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi," alisema.

Alisma CUF inamtaka Rais Jakaya Kikwete kuwahakikishia wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuishi bila hofu kutokana na matukio yanayoendelea kujitokeza ya milipuko katika kambi za jeshi, ili hali jiji likiwa limezungukwa na kambi mbalimbali za jeshi katika kila upande, Kigamboni, Lugalo, Mgulani, Upanga, Mabibo, Mbweni na kwengineko.




2 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... HUYO KIKWETE MWENYEWE NI MWANAJESHI UNAJUAJE KAMA NDIO KAWATUMA? PIGENI KELELE LAKINI WATANZANIA TUNAISHA NA MABOMU HAPO NDIO BADO MPAKA TUTEKETEE. RAIS HANA UCHUNGU WOWOTE WALA MKUU WA MAJESHI KAMA ANGEKUFA AU KUUMIA RIDHIWANI ANGECHANGAMKIA HARAKA LAKINI NYIE WA GONGOLAMBOTO ETI NDIO MMEKUTA KAMBI ZA JESHI HIVYO VIFO MMEVITAFUTA. EE MUNGU PELEKA MIAKA HII MITANO HARAKA HUYU MKWERE AENDE TUMECHOKA. WENZETU LIBYA LEO WAMEANZA MAMBO
February 18, 2011 12:25 PM
blank.gif

Anonymous said... Kikwete, waziri Mwinyi, Waziri Nahodha na mkuu wa JWTZ wawajibike sasa imetosha. Serikali inauwa watu lakini hakuna haijali wala kujifunza maana haioni makosa. Watu walikufa Mbagala kwa mabomu, Arusha kwa risasi za moto na sasa Gongolamboto kwa mabomu, lakini tunadanganyiwa Tume itaundwa kuchunguza ambayo mwisho wa siku hakuna tutakachosikia. Hivi watanzania tumekuwa watu wa kudanganywa mpaka lini? Raisi wa Tunisia, Misri walikuwa waongo hivihivi mwishowake wananchi walisimamama kidete mitaani kuwakataa. Nawaomba watanzania wenzangu popote mlipo tujipange mitaani kwa amani bila fujo tumkatae Kikwete maana amezidi uongo kwa watanzania. Yote aliyoahidi 2005 kama si machache hakuna alichofanya. Ajila kwa vijana hakuna, umeme hakuna, vitu bei juu, uchaguzi umepita sasa machinga wanasumbuliwa, mapato nao wamekuwa mbogo. atanzania msingojee muujiza, tumkatae Kikwete aondoke madarakani.
February 18, 2011 5:33 PM
 
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema hakuna kiongozi ndani ya Jeshi hilo atakayejiuzulu kufuatia vifo vya watu 21 na majeruhi 300 katika milipuko ya mabomu huko Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, kwa kuwa nafasi hizo si za kisiasa.

Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Usalama na Utambuzi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam, Brigedia Jenerali, Paul Mella, wakati akizungumza na Wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.


Brigedia Jenerali Mella alimwakilisha Mkuu wa Jeshi hilo, Jenerali Davis Mwamunyange, ambaye awali ilitarajiwa kuwa ndiye angezungumza, lakini ilielezwa baadae kuwa ameitwa ghafla kwenye majukumu mengine.


Dhumuni la mkutano huo ilikuwa kueleza mtiririko wa tukio zima la milipuko ya mabomu iliyotokea katika kambi hiyo ya Gongo la Mboto 511 KJ, iliyoko umbali wa kilomita 16 kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam.


Mella alisema wanaomtaka Mkuu wa Jeshi hilo, Jenerali Mwamunyange ajiuzulu hawajui Sheria ya Usalama wa Taifa namba 24 ya mwka 1976 na kueleza kuwa wanapaswa kuisoma kabla ya kutoa maoni yao.


"Sisi sio wafanyakazi na ndiyo maana huwezi kusikia Jeshi limegoma, sisi hatuna vyama vya wafanyakazi kama nyinyi kwa hiyo hizi nafasi za kijeshi si za kisiasa au mashirika ya umma na taratibu za kuingia na kutoka jeshini zinajulikana watu wazisome ziko wazi," alisema Brigedia Jenerali Mella.


Alisema kuna mambo mengi mazuri ambayo Jeshi hilo linafanya lakini hayawekwi wazi kama yanavyoandikwa mambo mabaya inapotokea milipuko ya mabomu.


"Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, hivi jamani Jeshi limefanya mangapi nchi hii, kule Kilosa wakati wa mafuriko ile reli ilijengwa na wanajeshi ndani ya muda mfupi, wanajeshi wakati wote wako kwenye hatari, msidhani tuna raha, kwa hiyo mnapoandika mabaya yetu basi na mazuri msiyasahau mbona yako mengi," alisema

"Fikiria wakati milipuko ikiendelea sisi tuliingia mle ndani lengo ikiwa ni kuangalia namna ya kuzima moto uliokuwa ukiendelea kuwaka lakini nyinyi mngekuwepo tukawaambia tuingie wote wengi wenu msingekubali," alisema na kusababisha kicheko.


Alisema matukio ya ajali kama hizo yamekuwa yakitokea katika mataifa mbalimbali duniani ila tofauti na Tanzania ni kwamba kwenye nchi hizo yamekuwa hayawekwi wazi na inakuwa siri.


Kuhusu milipuko ilivyoanza, alisema siku ya tukio askari waliokuwa eneo kambini, walisikia milio midogo midogo ya milipuko na ilipozidi waliondoka eneo hilo kwenda kutoa taarifa kwa viongozi wa kikosi na hatimaye Makao Makuu (Ngome) ilifahamishwa kuhusu tukio hilo.


Alisema baada ya hapo, maofisa na wapiganaji walikwenda eneo la tukio kwa ajili ya kusaidia kuzima moto ambao wakati huo ulikuwa ukiendelea.


Alisema mlipuko ilitulia majira ya saa 10:30 usiku na wakati huo tayari wananchi wapatao 4,000 walishakimbia maeneo yao na kwenda kwenye maeneo ya wazi.


Alisema ingawa hawana idadi kamili ya nyumba zilizoharibika lakini kuna nyumba nne ambazo zimeteketea kabisa kwa milipuko hiyo.


Alisema katika purukushani za kujiokoa, maofisa na wapiganaji wanne walijeruhiwa lakini hadi ssa hali zao zinaendelea vizuri.


Alisema katika tukio hilo, maghala 23 ya kuhifadhia mabomu yaliteketea kabisa na mabweni wanayoishi wanajeshi ambao hawajaoa yaliteketea yakiwemo magari manne makubwa ya kijeshi.


"Hili ni janga kubwa la kitaifa ambalo halikutarajiwa, pia chanzo cha milipuko hakijajulikana maana vyanzo vinaweza kuwa vingi, uzembe au hali ya hewa, lakini uchunguzi ukishakamilika tutajua, wananchi tuwe na subira tutakuwa tukiendelea kutoa taarifa kadri tutakavyokuwa tunazipata," alisema.


Alipoulizwa kuhusu tume ya Mbagala, alisema majibu ya tume ile ni kwa matumizi ya Jeshi na si rahisi kuwekwa wazi kwa raia.


Naye Mkaguzi Mkuu wa Jeshi, Brigedia Jenerali Leonard Mdeme, alisema iwapo serikali itaamua kambi hiyo ihamishiwe sehemu yoyote hilo litatekelezwa ili mradi litakuwa na maslahi kwa taifa.


"Serikali ikiamua kuwa kambi ihamie kisiwani au wapi, hilo linawezekana lakini kama litazingatia maslahi na usalama wa nchi, maana serikali ikiamua inawezekana," alisema.


Alisema inawezekana pia wananchi nao wakaondolewa karibu na makambi kwa ajili ya usalama wao iwapo itaonekana inafaa kufanya hivyo.

"Wakati naingia jeshini mwaka 1973 Lugalo ilikuwa mbali sana na Kariakoo, Gongo la Mboto kulikuwa hawaishi watu kabisa, unajua kuhamisha vikosi ni rahisi lakini lazima ieleweke kuwa vikosi hivi mkao wake unasababu zake kiulinzi, serikali ikiamua inawezekana ila hatua za namna hiyo zizingatie maslahi ya kiulinzi," alisisitiza.
Akizungumzia historia ya kambi hiyo, Brigedia Jenerali Mella alisema ilihamishiwa eneo hilo mwaka 1976 ikitokea Kunduchi na Lugalo na sababu kubwa ya kulipeleka eneo hilo ni kwamba wakati huo hakukuwa na watu karibu na ilikuwa mbali na katikati ya Jiji.

Alisema ilionekana ni busara kuweka kambi hiyo eneo hilo kwa kuwa ni karibu na reli, barabara na usafiri wa anga mambo ambayo ni muhimu katika suala la usalama.

Alisema kambi hiyo ni ghala kubwa la kuhifadhia zana na vifaa mchanganyiko vya kijeshi na kuvigawa kwa vikosi vingine katika maeneo mbalimbali hapa nchini.


Source: IPP MEDIA
 
Huyo jamaa hajui anaongea nini inaelekea na yeye yupo jeshini kisiasa zaidi, ni mbumbumbu asiye jua mambo yanayo endelea duniani.

Mfahamisheni kuwa wapo majenerali kadhaa wa majeshi ya marekani na Uingereza mbao wamejiuzuru miaka ya hivi karibuni (vita ya Afghanstan na Iraq) katika hali ya kuwajibika. Kama hajawahi kusikia jenerari anajiuzuru basi hiyo inaonyesa jinsi alivo short-sighted na huo ujenerari wake ni feki.

SISI HATUWEZI KUONGEA ZAIDI, KAZI TUNAMWACHIA JK.
 
Huyo jamaa hajui anaongea nini inaelekea na yeye yupo jeshini kisiasa zaidi, ni mbumbumbu asiye jua mambo yanayo endelea duniani.

Mfahamisheni kuwa wapo majenerali kadhaa wa majeshi ya marekani na Uingereza mbao wamejiuzuru miaka ya hivi karibuni (vita ya Afghanstan na Iraq) katika hali ya kuwajibika. Kama hajawahi kusikia jenerari anajiuzuru basi hiyo inaonyesa jinsi alivo short-sighted na huo ujenerari wake ni feki.

SISI HATUWEZI KUONGEA ZAIDI, KAZI TUNAMWACHIA JK.

Soma habari uielewe kabla ya kubwabwaja.

Imeelezwa kuwa sheria zetu zilizoanzisha JWTZ hazitoi mwanya kwa makamanda kujiuzulu.

Hata wewe waweza kuisoma sheria husika.
 
Yaani mara nyingine huwa ninapata taabu sana kuwaelewa viongozi (wawe wa kisiasa au kitaalamu kama huyu jenerali). Wananchi wanadai kuwajibika kwa wote ambao walikuwa na jukumu la kitaifa kuhakikisha haya hayatokei yeye anasema hajiuzulu kwa sababu wao si wanasiasa. Hivi kuna mwongozo upi unaosema kuwa wa kujiuzulu ni mwanasiasa tu? Mrema alipojiuzulu ile miaka ya 70 na mzee Mwinyi alikuwa mwanasiasa? Halafu anasema hatuyatambui mazuri ya jeshi huo ni mkakati wa kukwepesha mada na kuwafanya wahanga wa mabomu wajisikie vibaya. Ukweli wananchi na serikali kwa ujumla wanajali mchango wa wanajeshi. Na hili linathibitishwa na jinsi wananchi wasivyolalamika kwa wanajeshi kuuziwa vitu kwa bei ya chini ikiwemo kupanda daladala bure. Pia serikali inatambua mchango wao ndiyo maana wanapandishwa vyeo. Kutambua mchango haina maana ukifanya uzembe usiadhibiwe. Kitu kingine anasema hafanyi kazi kisiasa hivi anaweza kufafanua hii kauli? Je anaweza kuvamia nchi bila amri ya Amiri Jeshi Mkuu? Hivi hawa makamanda haelewi kwamba wale waathirika wa mabomu inabidi kulipwa na serikali na hiyo pesa ni kodi ya wananchi? Na haoni kuwa walipa kodi wanahaki ya kuuliza nani aliyesababisha hayo matumizi? Na je wanajua kuwa matumizi ya serikali yanasimamiwa na bunge ambalo linaendeshwa na wanasiasa? Jingine hivi hawajui kuwa kuna familia zipoteza watu ambao ndiyo ilikuwa mhimili na hivyo watategemea msaada wa serikali, ndugu na majirani? Ushauri wangu ni kwamba viongozi wetu wawe wanakuwa makini na kauli wanazozitoa maana zinaweza kutafsiriwa kuwa waliozitoa hawajali maisha ya watu?
 
Haya ni makamasi mengine kwenye kauli za wakubwa wetu........no matter what, lazima mtu abebe lawama kwa kilichotokea ikibidi kufukuzwa kazi, kufunguliwa mashtaka akithibitika n.k
Ufisadi na kula nchi kwa pamoja ndiyo kuna leta kauli za kijinga kama hizi! Majenerali wanajua kabisa kuwa kuna mahali kuna makosa ila hawako tayari kusema kwani wanajua na hakuna wa kuwanyooshea kidole....nani Raisi? mbona nae wanajua madudu yake mengi yaliyoitia hasara kubwa nchi hii..... lakini anaendelea kutawala?!
 
Na Mwandishi wetu

19th February 2011



Jeshi%282%29.jpg

Mkuu wa Usalama na Utambuzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Brigedia Jenerali Ignas Mella akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la kulipuka kwa mabomu katika kambi ya jeshi hilo iliyopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkaguzi Mkuu wa JWTZ, Brigedia Jenerali Leonard Mndeme.

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema hakuna kiongozi ndani ya Jeshi hilo atakayejiuzulu kufuatia vifo vya watu 21 na majeruhi 300 katika milipuko ya mabomu huko Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, kwa kuwa nafasi hizo si za kisiasa.
Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Usalama na Utambuzi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam, Brigedia Jenerali, Paul Mella, wakati akizungumza na Wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.

Brigedia Jenerali Mella alimwakilisha Mkuu wa Jeshi hilo, Jenerali Davis Mwamunyange, ambaye awali ilitarajiwa kuwa ndiye angezungumza, lakini ilielezwa baadae kuwa ameitwa ghafla kwenye majukumu mengine.

Dhumuni la mkutano huo ilikuwa kueleza mtiririko wa tukio zima la milipuko ya mabomu iliyotokea katika kambi hiyo ya Gongo la Mboto 511 KJ, iliyoko umbali wa kilomita 16 kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Mella alisema wanaomtaka Mkuu wa Jeshi hilo, Jenerali Mwamunyange ajiuzulu hawajui Sheria ya Usalama wa Taifa namba 24 ya mwka 1976 na kueleza kuwa wanapaswa kuisoma kabla ya kutoa maoni yao.

"Sisi sio wafanyakazi na ndiyo maana huwezi kusikia Jeshi limegoma, sisi hatuna vyama vya wafanyakazi kama nyinyi kwa hiyo hizi nafasi za kijeshi si za kisiasa au mashirika ya umma na taratibu za kuingia na kutoka jeshini zinajulikana watu wazisome ziko wazi," alisema Brigedia Jenerali Mella.

Alisema kuna mambo mengi mazuri ambayo Jeshi hilo linafanya lakini hayawekwi wazi kama yanavyoandikwa mambo mabaya inapotokea milipuko ya mabomu.

"Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, hivi jamani Jeshi limefanya mangapi nchi hii, kule Kilosa wakati wa mafuriko ile reli ilijengwa na wanajeshi ndani ya muda mfupi, wanajeshi wakati wote wako kwenye hatari, msidhani tuna raha, kwa hiyo mnapoandika mabaya yetu basi na mazuri msiyasahau mbona yako mengi," alisema

"Fikiria wakati milipuko ikiendelea sisi tuliingia mle ndani lengo ikiwa ni kuangalia namna ya kuzima moto uliokuwa ukiendelea kuwaka lakini nyinyi mngekuwepo tukawaambia tuingie wote wengi wenu msingekubali," alisema na kusababisha kicheko.
Alisema matukio ya ajali kama hizo yamekuwa yakitokea katika mataifa mbalimbali duniani ila tofauti na Tanzania ni kwamba kwenye nchi hizo yamekuwa hayawekwi wazi na inakuwa siri.

Kuhusu milipuko ilivyoanza, alisema siku ya tukio askari waliokuwa eneo kambini, walisikia milio midogo midogo ya milipuko na ilipozidi waliondoka eneo hilo kwenda kutoa taarifa kwa viongozi wa kikosi na hatimaye Makao Makuu (Ngome) ilifahamishwa kuhusu tukio hilo.

Alisema baada ya hapo, maofisa na wapiganaji walikwenda eneo la tukio kwa ajili ya kusaidia kuzima moto ambao wakati huo ulikuwa ukiendelea.

Alisema mlipuko ilitulia majira ya saa 10:30 usiku na wakati huo tayari wananchi wapatao 4,000 walishakimbia maeneo yao na kwenda kwenye maeneo ya wazi.

Alisema ingawa hawana idadi kamili ya nyumba zilizoharibika lakini kuna nyumba nne ambazo zimeteketea kabisa kwa milipuko hiyo.
Alisema katika purukushani za kujiokoa, maofisa na wapiganaji wanne walijeruhiwa lakini hadi ssa hali zao zinaendelea vizuri.
Alisema katika tukio hilo, maghala 23 ya kuhifadhia mabomu yaliteketea kabisa na mabweni wanayoishi wanajeshi ambao hawajaoa yaliteketea yakiwemo magari manne makubwa ya kijeshi.

"Hili ni janga kubwa la kitaifa ambalo halikutarajiwa, pia chanzo cha milipuko hakijajulikana maana vyanzo vinaweza kuwa vingi, uzembe au hali ya hewa, lakini uchunguzi ukishakamilika tutajua, wananchi tuwe na subira tutakuwa tukiendelea kutoa taarifa kadri tutakavyokuwa tunazipata," alisema.

Alipoulizwa kuhusu tume ya Mbagala, alisema majibu ya tume ile ni kwa matumizi ya Jeshi na si rahisi kuwekwa wazi kwa raia.
Naye Mkaguzi Mkuu wa Jeshi, Brigedia Jenerali Leonard Mdeme, alisema iwapo serikali itaamua kambi hiyo ihamishiwe sehemu yoyote hilo litatekelezwa ili mradi litakuwa na maslahi kwa taifa.
"Serikali ikiamua kuwa kambi ihamie kisiwani au wapi, hilo linawezekana lakini kama litazingatia maslahi na usalama wa nchi, maana serikali ikiamua inawezekana," alisema.
Alisema inawezekana pia wananchi nao wakaondolewa karibu na makambi kwa ajili ya usalama wao iwapo itaonekana inafaa kufanya hivyo.

"Wakati naingia jeshini mwaka 1973 Lugalo ilikuwa mbali sana na Kariakoo, Gongo la Mboto kulikuwa hawaishi watu kabisa, unajua kuhamisha vikosi ni rahisi lakini lazima ieleweke kuwa vikosi hivi mkao wake unasababu zake kiulinzi, serikali ikiamua inawezekana ila hatua za namna hiyo zizingatie maslahi ya kiulinzi," alisisitiza.
Akizungumzia historia ya kambi hiyo, Brigedia Jenerali Mella alisema ilihamishiwa eneo hilo mwaka 1976 ikitokea Kunduchi na Lugalo na sababu kubwa ya kulipeleka eneo hilo ni kwamba wakati huo hakukuwa na watu karibu na ilikuwa mbali na katikati ya Jiji.

Alisema ilionekana ni busara kuweka kambi hiyo eneo hilo kwa kuwa ni karibu na reli, barabara na usafiri wa anga mambo ambayo ni muhimu katika suala la usalama.
Alisema kambi hiyo ni ghala kubwa la kuhifadhia zana na vifaa mchanganyiko vya kijeshi na kuvigawa kwa vikosi vingine katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

CHANZO: NIPASHE

Nashangaa sasa jeshi linajiweka mbali na siasa wakati si muda mrefu uliopita wakati wa uchaguzi mkuu walijiingiza katika siasa. Hata hivyo si nafasi ya huyo msemaji kusema kuwa hakuna atakeyejiuzulu. Kujiuzulu au kutojiuzulu kunatokana na uamuzi wa Amiri Jeshi Mkuu ambaye ni raisi wa Tanzania na amewekwa pale kutumikia wananchi. Tumeona hata nchi zingine kama Marekani wakati viongozi wa juu wa jeshi walipojiuzulu nyadhfa zao kutokana na kutowajibika vyema. Usemi wa msemaji huu ni kuonyesha jinsi gani baadhi ya watu katika jamii wanavyofikiria kuwa wanaweza kufanya lolote watakalo.
 
kwani wanaojiuzulu na wanasiasa pekee? Hivi kiongozi wa jeshi anakuwa mtu mwenye upeo mdogo kama huyu? I wonder..

Hebu tuone kama kweli tuna amiri jeshi mkuu ama kituko! Hawa wanapaswa kuwajibishwa.

Ila kwasababu wote wanajuana uchafu wao,wanachekeana tu..hata kwa issue nzito na hatari kama hizi! Anayeumia n mwananchi wa chini
 
Someni National Defence Act kabla ya kulalamikia majenerali.
Labda suala hili la kujiuzulu wanajeshi liingizwe kwenye katiba mpya, vinginevyo sheria ya sasa haitoi mwanya huo.
 
Kama wao hawajiuzulu basi wamshauri Amiri Jeshi mkuu maana yeye ni mwanasiasa. Wasitubabaishe na sheria zao za usalama. Kama watu wanakufa kwa sababu ya mabomu yao huku wahusika wanajitetea kubaki kwenye nafasi zao bora kusiwepo sheria hiyo.
 
Back
Top Bottom