JWTZ na taarifa ya Mabomu Gongo la Mboto

JWTZ na taarifa ya Mabomu Gongo la Mboto

hebu tuache ujinga.......... amiri jeshi mkuu ni kwasababu ya siasa plus government zaidi kuongoza jeshi la nchi husika

wanajeshi hawana sababu ya kujiuzulu, watakua decommissioned kama hawakidhi viwango na kuna steps zake

ushabiki ukizidi ni ajabu sasa
 
kwa hili naunga mkono wanajeshi... sasa kama kikwete ni amiri jeshi mkuu basi tuone aki-decommission any military officer

kama kweli yeye ni mwanaume wa shoka

nimependa sana jeshi lilivyoweka mambo wazi, haondoki ntu, utaondoka wewe... meaning
 
Sikutegemea la ajabu kutoka kwa hao viongozi mpaka hapo nguvu ya umma itakapotumika. Na hao ndio aina ya viongozi tulionao nchini.
 
Someni National Defence Act kabla ya kulalamikia majenerali.
Labda suala hili la kujiuzulu wanajeshi liingizwe kwenye katiba mpya, vinginevyo sheria ya sasa haitoi mwanya huo.

ungekuwepo usiku ule wa 16 feb katika eneo kati ya tazara traffic lights na gongo la mboto hadi pugu usingetetea kauli hii isiyokuwa na nidhamu.
 
'Kuhusu milipuko ilivyoanza, alisema siku ya tukio askari waliokuwa eneo kambini, walisikia milio midogo midogo ya milipuko na ilipozidi waliondoka eneo hilo kwenda kutoa taarifa kwa viongozi wa kikosi na hatimaye Makao Makuu (Ngome) ilifahamishwa kuhusu tukio hilo.' .......
Kwa hiyo zile taarifa kuwa hakuna mwanajeshi aliyekufa ni za kweli kwani walijua mapema wakasepa na familia zao wakaachwa wenzangu na mie wafilie mbali!

'Alisema katika tukio hilo, maghala 23 ya kuhifadhia mabomu yaliteketea kabisa na mabweni wanayoishi wanajeshi ambao hawajaoa yaliteketea yakiwemo magari manne makubwa ya kijeshi.
"Hili ni janga kubwa la kitaifa ambalo halikutarajiwa, pia chanzo cha milipuko hakijajulikana maana vyanzo vinaweza kuwa vingi, uzembe au hali ya hewa, lakini uchunguzi ukishakamilika tutajua, wananchi tuwe na subira tutakuwa tukiendelea kutoa taarifa kadri tutakavyokuwa tunazipata," alisema.

hapa ndio serikali inapotuchanganya ,wakati wataalamu wa masuala ya kijeshi wanatuambia kuwa hili ni janga kubwa la kitaifa na ambalo halikutarajiwa mheshimiwa spika analiambia bunge kuwa hili sio jambo la dharura.!!! ndugu supika uje watanzania tumechoka kufanywa wajinga nyie endeleeeni kutufanya mazuzu ila ipo siku mtajua kweli wananchi wamechoka!
 
Mengi yatasemwa lakini mwisho wa yote watanzania 2mkimbilie Mungu kwn ye ndo suluhisho la matatz yote yanayo2kabil
 
kama jeshini hakuna kujiuzuru kwa makosa makubwa kama haya basi wanajeshi ni malaika huwa hawakosei,,,, ila amini amini nawaambieni wasipojua kusoma alama za nyakati watashtuka wakati ukiwa umepita,,hata hosn mubaraka aliamini kama wao ila mwisho wa siku akashangaa mwenyewe. hili la gongo la mboto ni deni kwao siku zinakuja watalilipa tu:rain:
 
Hili nalo limeshakuwa Jeshi la Wazembe si Jeshi la Wananchi tena
 
Mabomu yakilipuka wakiambiwa wajiuzulu wanasema JESHI HALINA SIASA.
Mwaka jana wakti wa Kampeni za Uchaguzi(SIASA)Mkuu wa 2011 wanajeshi WALIINGIA KUPIGA KAMPENI. HATUJASAHAU YALE YA SHIMBO amabyo yaliwashangaza Watanzania wote. TUNATAKA LEO JWTZ WATUAMBIE SHIMBO ALIKUWA AKIFANYA NINI MWAKA JANA KAMA SIASA???

MWAMNYANGE NA SHIMBO MJIUZULU AU KIWETE AWATIMUE KAZI. Msitufanye Watannzania hatuna akili. Yaaani KWA UZEMBE WENU WA KILA SIKU TUNAPOTEZA NDUGU ZETU HUKU NYIE MKIDAI HAMWEZI KUJIUZULU KWASABABU NI WANAJESHI KWELI?????

ACHENI LONGOLONGO. RESIGN IMMEDIATELY!!!
 
Haya Majigambo ya Huyu Afande si Bure.
Viongozi wa jeshi wana vijambo viwapavyo jeuri na kuwafanya waseme watakalo.
Inaelekea wameshika sehemu ya Mpini hawaogopi makali.

Hakukua na sababu yeyote ya kublast ujinga wake kwamba hakuna atakaye jihuduru.
Kwanza hajatueleza chanzo cha milipuko hiyo ni nini.
Pili hakutakiwa kumsemea Mkuu wa majeshi kuhusu kujihudhuru.
Tatu Duniani si wanasiasa tu wanao jihudhuru.
Nne wanajeshi Tanzania ni sehemu ya wanasiasa wa CCM ndiyo maana mwaka Jana Afande Shimbo alitoa onyo kwa vyama vya upuinzani kukubali Matokeo No Matter what?? Wakati huo huyu mjinga Brgedia Mella alikuwa wapi kukanusha maneno ya Shimbo??

Anasubiri ukuu wa Wilaya huyu.

Matumbo ya maafande hawa yameanza kuwa mazito kwa lishe Haramu ndiyo maana wanaropoka ovyo!
Jeshi letu linazidi kupoteza maadili na nidhamu inashuka kwa kasi sana, sasa hivi liko kwenye kiwango cha JKTpunde kidogo litakuwa kwenye kiwango cha mgambo na hatimaye Sungusungu.
 
Kuwajibika = Hakuna !! Lo mpya hii yaani uzembe uachiwe kuendelea .
 
Kama wakujiuzuru ni wanasiasa mbona Waziri ajaanza mapema ilikuonyesha kuwa maneno yake ni kweli, pia kama hawawezi basi rais amfuke kazi Mwamunyange kama hataki kung'oka
 
hakuna wa kuresign hapa



Chukua tano mwanangu, Mobomu ni ya kichina sasa mnategemea nini wakati hamuyatumii
 
Hiyo ni kwa Tanzania tu ndiko ambako maafisa wa jeshi ni lulu kiasi kuwa hata hawawezi kuwa accountable kwa makosa wafanyayo. Mbona kwa Obama majenerali wengi wamekuwa wakijiuzulu wanapofanya makosa. Gen. Stanley McChrystal aliyekuwa akiongoza vita huko Afghanstan alijiuzulu kufuatia skendo ya kumdhihaki rais Obama kwa mwandishi mmja wa habari, General Ricardo Sanchez aliyekuwa akiongoza vita huko Iraq naye alijiuzulu baada ya skendo za kutesa wafungwa waIraq kwenye gereza Abu Ghraib. Ironically, nafasi zao zilikuwa zinajazwa na mtu yule yule: General David Patreas.

"Fikiria wakati milipuko ikiendelea sisi tuliingia mle ndani lengo ikiwa ni kuangalia namna ya kuzima moto uliokuwa ukiendelea kuwaka lakini nyinyi mngekuwepo tukawaambia tuingie wote wengi wenu msingekubali," alisema na kusababisha kicheko.
Alisema matukio ya ajali kama hizo yamekuwa yakitokea katika mataifa mbalimbali duniani ila tofauti na Tanzania ni kwamba kwenye nchi hizo yamekuwa hayawekwi wazi na inakuwa siri.
Huiyu Afisa ni mwongo. milipuko haina siri; hakuna nchi yoyotye ambayo iliwahi kuwa na milipuko ya aina hiyo ikaua watu halafu eti ikawa ni siri. Dunia ya leo ni ya uwazi sana hasa inapokuwa swala la maisha ya raia. Labda kama inatokea nchi za siri kama Iran, Libya, Cuba na Korea. Hata China ya leo hii siyo nchi ya siri namna hiyo.
 
Tumezidi kuwanyenyekea wanajeshi utafikiri Miungu-watu,hawajui hata maana ya kujiuzuru!!? Hata unaposhindwa kusimamia ueledi inabid kujiuzuru. Je,waziri wa Rwanda kujiuzulu sbb ya ngono ni siasa??
 
Alipoulizwa kuhusu tume ya Mbagala, alisema majibu ya tume ile ni kwa matumizi ya Jeshi na si rahisi kuwekwa wazi kwa raia.[/I]


Sasa nini maaana ya kufanya uchunguzi kama majibu ndio yanakua kama haya?
 
Mi labda nipewe maana ya Kujiuzulu na kuwajibika?

Formally Defn:
A resignation is the formal act of giving up or quitting one's office or position.

Responsibiliy: Answerable for an act performed or for its consequences; accountable; amenable, especially legally or politically; Capable of responding to any reasonable claim; able to answer reasonably for one's conduct and obligations; capable of rational conduct.

Katika hali ya kawaida mtu ambaye ni responsible pia lazma atakuwa tayari kujiuzulu kwa makosa aliyofanya na pia kuruhusu uchunguzi huru kufanyika. Pia kitaalamu sio lazma uache jeshi kama BG. Mdeme anavyotaka kuaminisha umma. Unaweza kuacha cheo ambacho kiko answerable ili wengine washike usukani.. Na wewe kubaki na cheo cha kijeshi tuu na si cha kiuongozi. Pale Jeshini kuna vyeo vingi lakini kushindwa kutimiza wajibu hakumaanishi kama wewe ni General au Brigedia General basi utavuliwa cheo cha kijeshi.. Hapana!! Bali kama wewe sijui ni mkurugenzi wa nini sijui, kiongozi wa kikosi fulani labda basi unatolewa hiko cheo. Na sisi kama wale wakuu walivyotaka kupotosha UMMA.

Mi nadhani wapishe wengine wafanye uchunguzi na watu wapewe adhabu za kijeshi kama zinavyoanishwa endapo utafanya uzembe wa kupindukia jeshi.. Mkuu wa kikosi yule Colonel wa Group 511 ni mnene mzembe aachie ngazi kwa uzembe akifuatiwa na wakubwa zake.

Nawasilisha!!
 
Kuna ambao ulitokea Maputo Mozambique nadhani miaka miwili iliyopita , habari zilikuwa wazi kabisa. Vile vile kama ni siri hivyo anajuaje ilitokea?
 
Back
Top Bottom