Moshe Dayan
JF-Expert Member
- Feb 10, 2008
- 815
- 698
Moshe Dayan najua when it comes to mambo ya JWTZ uko very deep.
Swali langu kwako ni hili, kama kweli jeshi linafanya reform na kuanza kuajiri wasomi wengi lakini kwa utaratibu wa jeshi hao wasomi lazima wafaulu shughuli ya monduli, na huko monduli ndiko kunatuhumiwa kuwa na matrainer wanoko hasa wale wa vteo vya chini.
JWTZ inafanya juhudi gani kuondoa huo unoko/uonevu ili wataalamu/waomi hao watumie taaluma zao kwa manufaa ya jeshi na nchi kwa ujumla.
Na kwa nchi zilizoendelea wasomi wanaojiunga na majeshi wanakuwa treated ''kinyaninyani'' kama mnavyowafanyia monduli?
Mkuu mambo ya jeshi yako hivyo hivyo matrainer wengi elimu zao ni za chini, tafuta hata record za WESTPOINT kwa jeshi la AMERICA au Loyal College UK kupitia cadet school lazima uwe harassed ili apatikane soldier mzuri especially officer ambaye ni commander wa unity!!! Mkuu tafuta training program ya majeshi mbali mbali hasa western armies!! Huwezi kupata best officers kama hujawatoa uraia ingawa mara nyingi wanapewa short courses badala ya long program!! Wataalamu wanapewa special treatment wanapomaliza course, hivyo vijana wavumilie tuu undava ili baadae wafaidi!!
Sawa kabisa Mkuu SANHURST walipitia makamanda wengi kama Gen Sarakikya naona yuko fit hata leo hii!!!mtumishi UK ulimaanisha SANDHURST sio?
mtumishi UK ulimaanisha SANDHURST sio?
hahhaaha umenikumbusha mbali nilipeleka cv pale ngome upanga nika kosea geti jama alie ni pokea nikamwambia naleta barua yakuomba kazi akani jibu hili ni jeshi lina taratibu zake sio unaleta barua kama unaenda kwenye shamba la mkongeUnaonekana unalazimisha kuajiliwa ....Jeshi si kampuni kama ya mkonge!
hahhaaha umenikumbusha mbali nilipeleka cv pale ngome upanga nika kosea geti jama alie ni pokea nikamwambia naleta barua yakuomba kazi akani jibu hili ni jeshi lina taratibu zake sio unaleta barua kama unaenda kwenye shamba la mkonge
Ukiangalia mfumo mzima wa ajira utabaini yafuatayo
1. Waalimu waliopo vyuoni 90% ni kikwazo kwa wasomi wengi wanaojiunga na jeshi hilo, akitokea mwanafunzi mwenye elimu kubwa hata Phd watafanya kila mbinu wamfukuze kwa kisingizio cha utovu wa nidhamu au watacomment kuwa kafeli.
2. Trainning zao hazija base kutafuta vipaji vya kweli katika nyanja muhimu kitaifa, kama vile madaktari, Eng, nk. Mfano Nyumbu mpaka leo wameshindwa kuifanya iwe ya kizalishaji toka enzi za mwalimu. Lugalo mpaka leo hawana hata blood bank sababu wanasayansi tiba hawapo ndio maana wanashindwa kukabiliana na migomo ya MH, sababu huko wengi 80% ni AMO na CO.
3. TMA ni kikwazo kikubwa sana katika kuwapata wasomi wazuri ndani ya jeshi hilo, elimu ya rasilimali watu kwa waalimu inawezekana ikawa ni issue. So they are trying to reduce the number of students kwa visingizio vya nidhamu ambayo ukifuatilia kiundani sio nidhamu as such but ni kutojua ubaya wakumfundisha mtu at certain level na kumwachisha mafunzo. HILO N BOMU BAADAYE.
4. Mazingira dhaifu kuwawezesha wenye vipaji kubuni kwa uhuru na kutumia taaluma zao, kufanya tafiti chanya maeneo yao ya kazi, mpaka leo hatujaziona.
5. Officer aliyetokea uraiani moja kwa moja I mean those who have got a little knowledge kuwa mkufunzi, atafundisha nini kama sio kupika majungu na kukosa comfidence?
Hayo machache yaliyobainishwa hapo juu ni chanzo kikubwa cha jeshi letu kuwa kama lilivyo hivi leo.
yani toka nimeanza kusoma huu uzi na michango ya wadau humu ndani nahisi harufu za "viroba" tu.
Comrade, nidhamu haijengwi kwa kumbembeleza mtu..., hata kama wewe ni msomi wa kiwango cha juu, kama umeamua kuingia jeshi, kwanza we train you to be a commander.., lazma kwanza uwe mjeshi mzuri umeiva na mwenye nidhamu then ukifaulu,, unapewa sasa kitengo chako kufatana na elimu ulonayo,
Nasisitiza, monduli unafundishwa kwanza kuwa commander then ukifaulu, MMJ wanakupangia kazi,, kazi ya wakufunzi monduli ni moja tu, kukupika uive.na pale ndio unakutana na watu wana roho mbaya shetani mwenyewe anawaogopa, tena anayekutesa ni corporal ambae siku chache mbeleni atakusalute,,
pale unajengwa utimamu wa akili na mwili na pia wanaitoa ile roho flani ya kahuruma ka asili.., huwezi kwenda kwny battle unamuona adui unaanza kufkiria nikimuua familia yake itapata tabu! Au unaanza kufkiria amri ya mungu usiue,, ww unakua kamanda ambae hujaiva,,
Nakubaliana na ww kuna mazoezi huwa yanazidi kipimo lakn pia yana faida kwa utimamu wa mwili kwa mfano monduli kuna "exercise chomoka" hii ni kukimbia 48kms,,, je, majeshi ya kisasa bado yanafanya haya mambo? Lakn jiulize wht if ulitekwa umefanikiwa kutoroka, kama hukupewa stamina ya namna hii utafika mbali??
Na ukitaka kujua kwamba wanajeshi wana stamina pamoja na wengine kua na vitambi.., kila wiki kila kikosi kina siku ya mazoezi na utaona watu wazima na vitambi vyao lakn wanakimbia na wanafanya mazoezi mengine vzr tu, nadhani wengi wenu mnaoishi near barracks hua mnaona
Mwisho wa siku hata tuki-modernize jeshi kinachohitajika ni nidhamu, utimamu wa mwili na akili, comrade, katika hayo mazoezi ya kinyaninyani kuna faida zake pia..., look at things from a positive side!
yani toka nimeanza kusoma huu uzi na michango ya wadau humu ndani nahisi harufu za "viroba" tu.
Mkuu hilo ndilo jeshi, usiende pale Monduli kutafuta nyota ukatanguliza shahada zako, hizo zitakuja fanya kazi baadae!! Kwanza uwe discipline upate harassment ili uwe askari mzuri, mambo ya jeshi yanahitaji utii, fikiria bomu limetupwa hapo chini unaambiwa down, wewe unajishauri kwa nini si tutakuokota vipande vya nyama???? Kamanda mzuri lazima awe na discipline, hapo tutapata best soldier !!!! Pole kama ulikwenda ukashindwa kupaform, tekeleza amri maswali baadae!!!
Nimependa jinsi watu walivyoeleza mambo kwa kweli imenikumbusha jamiiforums ya wakati ule...
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums