JWTZ jifunzeni Kupitia clip hii

JWTZ jifunzeni Kupitia clip hii

Hawa wa kwetu,ni kenge kasoro mkia,wenye weredi japo kidogo, ni wale wenye vyeo vikubwa kuanzia kanali, huku chini ni utoporo mtupu, nilipita kambi moja pale Dar karibu na uwanja wa Taifa, kikosi cha usafirishaji, nikawakuta hawa private, baadhi yao wamevaa Kombat kata K, yale mashati yao, hawajachomekea, ni kama vile waimba hip hop, nikaona hapa nimekutana na mandojo na domokaya!
Mi nikikuta hawa wamebananishwa, sehemu, wanatatuliwa malinda, nami naunga foreni.
 
Hawa wa kwetu,ni kenge kasoro mkia,wenye weredi japo kidogo, ni wale wenye vyeo vikubwa kuanzia kanali, huku chini ni utoporo mtupu, nilipita kambi moja pale Dar karibu na uwanja wa Taifa, kikosi cha usafirishaji, nikawakuta hawa private, baadhi yao wamevaa Kombat kata K, yale mashati yao, hawajachomekea, ni kama vile waimba hip hop, nikaona hapa nimekutana na mandojo na domokaya!
Mi nikikuta hawa wamebananishwa, sehemu, wanatatuliwa malinda, nami naunga foreni.
Hahahaaa
 
Nchi ambayo haijawahi kupigana vita wanajeshi wake huwa hawathamini raia,maan hawajawah kushuhudia msaad wa raia wake wakiwa mstari wa mbele..Kizazi cha wanajeshi waliopigana Vita ya Kagera kimeshtoweka kwa kifo au wamestaafu,wanajua thamani ya Raia wao kipindi kile..Watanzania waliwachangia wanajsh wao Damu,fedh,vykula na hata mifugo..Mwanajesh wa leo tena kijana asiye n madili anaingia jeshini ataishia kupiga raia kisa Pombe na kugombania Wanawake Bar
Umenena mkuu
 
Kwani wewe kila kitu unachopewa unakula bila kujiridhisha usalama wake?..mawazo yako yaende mbali zaidi katika mambo mengi yakiusalama kwasababu ushirikiano hauko kwenye kula tu.Majeshi yana vitengo vyake vyakuchakata mambo nakujiridhisha.swala ni jeshi lako linamahusiano gani na wananchi wake au ni maadui.Hiyo ndio hoja.kwasababu kukiwa na uadui adui ni rahis zaidi kujipenyeza kuliko kukiwa na utengamano.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo sawa sana mkuu
 
Swala la kuamini mtu ata wewe hutakiwi kumwamini mtu yoyote ata mkeo.Kwasababu usalama wako nijukum lako wewe mwenyewe sio kwa wanajeshi tu au wakati wa vita.Mada ni ushirikiano wa jamii na vyombo vya ulinzi na usalama,je mahusiano yao yakoje.Adui akiamua kuingia sehem yoyote anaweza kuingia ata ufanyeje kwasababu huyo tayari anakua na lengo fulani ila lazima kuwe na mahusiano mazuri kati ya jamii na hivi vyombo,mahusiano mazuri ya kwenye kila kitu kinachohusu ushirikiano na ulinzi na usalama sio kwenye kula tu.Swala la tahadhari ilo linabaki kwa mtu mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umechukua zote 100% mkuu. Tunachotaka ni mahusiano na ushirikiano mzuri Kwa raia. Jnne natoka shamban na pkpk nikaona nikaongeze mafuta sheli baada ya kuingia barabarani nikapigwa mkono ni simame na mjeda kavaa Kombat nadhan nae alikuwa anatoka kwake ....sikusimama nikajisemea hapa naweza kuyakanyaga muda wowote tu.
 
Anacho zungumzia ni kwamba adui atajichanganya na hao raia wako,akupatie hiyo misosi yenye sumu..maana ni vigumu pia raia wako kutambua kuwa huyu ni raia mwenzake ama adui. Mbona mnashindwa kuelewa jambo dogo kama hili?
Issue sio msosi tu hapa kinacho matter ni ushirikiano wa jeshi na wanaNchi na SI vingine. Ni rahisi sana adui kujipenyeza Kwa raia akijua Kuna udhaifu huo!
 
Kabla hawajajenga kivuko Cha waenda kwamiguu pale kawe bondeni, nilishawahi shuhudia wanajeshi wakimrukisha kichura mtu mzima mwenye miaka kama 45-50 akiwa na watoto wake wawili kisa amekatisha eneo la jeshi,
Hapo walitumia makalio na sio akiri wao wanajua mtu kumwelekeza au kumuonya basi ni kumpa kibano. Amini nakuambia hao Watoto wameshawachukia wanajeshi mazima
 
Hili jeshi tulilo nalo limeshindwa kabisa kuhalalisha uwepo wake kwa kukosa uzalendo.

Kwa hatua hii tuliyofikia laiti kama lingekuwa ni jeshi la kizalendo ccm wasingekuwa madarakani leo lakini kwa kuwa ni jeshi la kisiasa basi ccm wanaendelea kung'ang'ania madarakani kwa kuhujumu uchaguzi kila mara bila hofu.

Tunaona kule Afrika Magharibi jinsi wananchi wanavyowaunga mkono wanajeshi wao kwa vile wanavyoona majeshi yao yanavyopigania maslahi yao wakati sisi hapa tunaona ccm na jeshi lao wanavyonyanyasa raia completely with impunity.
Inasikitisha mnoo mkuu
 
Kwamba hata hao wanajeshi wanaopokea zawadi/vyakula/ vinywaji hivyo hawajui kwamba vinaweza kuwekwa sumu na adui? Ni wazi kwamba na wao wanajua wanachokifanya. Point muhimu kwenye clip ni ushirikiano uliopo kati ya raia na wanajeshi ambapo kwa mazingira ya TZ tayari kuna doa kubwa. Mbaya zaidi hata viongozì wa serikali na jeshi lenyewe hawatoki hadharani na kukemea uonevu wa hao wanajeshi na ikitokea kukemea inakuwa ni geresha tu na kesho yake matukio ya uonevu yanaendelea kama kawaida.
Ushirikiano JWTZ na raia ni zero kabisa raia huwaombea wafe kama ulifatilia comment kwenye Uzi wa Gent utaona wazi raia Hana hamu kabisa na wajeda
 
Halafu jamaa anataka jeshi letu liige.
Waige 100% kwani faida ni kubwa kuliko wanavoishi na raia saivi hata huko kawe Kwa Sasa mjeda hawezi kaa akastarahe na kunywa au kula bila tahadhar Kwa sababu wanajua walichofanya linaweza mwondoa mjeshi muda wowote.
 
Kinachowaponza wanajeshi wa Tz ni tamaa na kutaka umaarufu wa kipumbavu, kuna jirani yangu alikuwa anajenga nyumba yake, akaweka materials za ujenzi kwa mwanajeshi, huwezi kuamini yule mwanajeshi alitumia mifuko kadhaa ya saruji na nondo kukamilishia shimo lake la choo akimuahidi kumrejeshea, miaka ikapita hakumrejeshea, mbaya zaidi baadaye akawaambia majirani amejilipa pango la kutunza vifaa
Duu tuseme alitumia ubabe
 
Hakuna siku itafika kuwa binadamu au raia wa kawaida hatokuwa chanzo cha taarifa za kipelelezi. Hakuna katika Dunia hii. Pamoja na technology kukua kiasi cha kufika mawinguni. Bado binadamu ni chanzo kikuu cha taarifa za kipelelezi. Nakuambia hivi nipo field. Yaani ni moja ya shughuli zangu nikiwa nimesoma Cuba, Russia, Israel, China na Marekani. Watalaamu wanatufundisha hivyo. Miezi kadhaa ago nlikuwa Russia.
Na huo ndio ukweli
 
Nilikuwa natafuta comment ya hivi. Hakika wewe ni mfano halisi wa JF great thinker!!
Kwa kipi hapo kilichoandikwa mkuu? Mtu uishi vibaya utegemee kulipwa mema? Kwa jinsi wanavyoishi na raia wategemee mema? La hasha kitawaramba
 
You gotta a point, ila hao wanajeshi nao si wapumbavu eti wanachopewa wale tu. Raia amekupa pokea weka kando. Mpe mbwa kwanza akipona nawe unakula. Unadhani wao hawajui madhara ya kupokea kitú toka kwa mtu usiyemfahamu?a

Point yamleta mada ni kuwa, sisi wanajeshi wetu hatuwezi kushirikiana nao namna hiyo.
"sisi na wanajeshi wetu watuwezi shirikiana nao" [emoji419][emoji375]
 
Kitendo kinachofanyika ktk video ni chema na hakika kinapendeza na kuleta fundisho.

Ila sidhani kama ni salama sana hasa kwa vikosi ambavyo vipo vitani. Adui anaweza kujipenyeza ktk aina nyingi hatari hasa vyakula kama hivyo tunavyoona hapo.

Sidhani kama kuna la kujifunza hapo, labda ingekuwa video ya mwanajeshi aliyejeruhiwa akipatiwa matibabu na raia au vinginevyo.
Njia ya chakula & maji sio ya kujifunzia, ni hatari zaidi.
Siku ntaleta video jinsi traffic wa bongo wanavopewa samaki na dhabibu na gari za Mwanza dar, yaani Huwa wametengewa kabisaa
 
Back
Top Bottom