JWTZ, iombeni Serikali isitumie vyeo vyenu wala sare zenu kwa ustawi wa Taifa

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,417
30,927
Naliomba jeshi letu JWTZ liiombe Serikali yetu isitumie sare zake kwa namna yoyote ile kwenye post za kiraia.

Wala nafasi kubwa za kiraia za kuchaguliwa zisivae sare za jeshi letu kamwe.

Sababu.

Tunaànza kuona jeshi linatumika kisiasa kabisa wazi wazi Sasa wananchi wasije kutafsiri under performance ya mwanajeshi mmoja katika capacity ya kiraia haitakuwa sawa.

Jeshi letu ni Safi lisianze kuchukiwa na raia Wala kuwagawa raia !

Raia mwema .

Superbug.
 
Mods tafadhali msifute Uzi huu labda muuboreshe kwasababu hauna majungu uko wazi lengo langu wanajeshi wanaochaguliwa na raia kwa manufaa yao; hao wanajeshi wakivurunda huku wamevaa sare za jeshi haileti sifa nzuri.

Mfano

TAKUKURU wananchi wameshaanza kuinyoshea vidole kwamba inatumika kisiasa kwenye serikali hii ya awamu ya tano na mitano ipo wazi mbaya zaidi under performance ya hicho chombo itatafsiriwa na uniform za jeshi letu tukufu hii itashusha uzalendo wa kweli !! Acha ule uzalendo wa tafsiri ya CCM.
 
Naamini huu Uzi hautafutwa ila kiukweli CCM mnaliumiza Sana taifa mno mno mno na mnavitukanisha vyombo vyetu vya ulinzi na usalama mbele ya taifa na mataifa.
 
Jeshi laweza kuwa ndio kichaka pekee kinachotumika kuhujumu umma wa watz kwa Sasa. Nadhani ni vema kulitazama jeshi kama jeshi la cccm na sio la nchi.
Nyerere aliliita jeshi la wananchi kwa trend ya Sasa linaenda kuwa jeshi la kikundi Cha watu wachache wenye malengo ya KISIASA imeniuma Sana kumuona mnyika anaitwa na TAKUKURU na wabunge wa chadema wakati huohuo Humphrey Polepole anagawa bajaji iringa Sasa najiuliza mstari unaogawa tafsiri ya rushwa kwenye siasa za Tanzania ni upi na una unene gani?
 
Hivi Leo msigwa au chadema akigawa bajaji kwa namna ileile ya Polepole TAKUKURU watakaa kimya? Ndio maana nawashangaa Sana viongozi wetu wa dini wanaoipotosha sheria .
 
Jamiiforums mkifuta huu Uzi kwa Mara ya kwanza nitafikiria kuwasiliana na ikulu ya marekani na EU baada ya kulishtaki kanisa katoliki Vatican na wamenijibu kwa barua na vitendo.
 
Mkuu wa majeshi

Jenerali Mabeyo

Kuna member humu jamiiforums aliwahi kusema akirefer wahamiaji wa CCM toka upinzani. Namnukuu

Ukinunuliwa na CCM utakuwa

Used
Misused then
Abused

Sasa naamini jeshi letu limefikia stage ya pili (misused)

Likifikia stage ya tatu (being abused) naamini halitakubali litajibu !

Tusifike huku wote sisi kwasasa ni watoto wa John Joseph Pombe Magufuli.

Huu ndio ujumbe wangu wa mwisho wa siasa za Tanzania nitarudi Tena mwakani baada ya uchaguzi.

Tukutane jukwaa la mapenzi (MMU)
 
Nyerere aliliita jeshi la wananchi kwa trend ya Sasa linaenda kuwa jeshi la kikundi Cha watu wachache wenye malengo ya KISIASA imeniuma Sana kumuona mnyika anaitwa na TAKUKURU na wabunge wa chadema wakati huohuo Humphrey Polepole anagawa bajaji iringa Sasa najiuliza mstari unaogawa tafsiri ya rushwa kwenye siasa za Tanzania ni upi na una unene gani?
Khaa!
 
Mkuu wa majeshi

Jenerali Mabeyo

Kuna member humu jamiiforums aliwahi kusema akirefer wahamiaji wa CCM toka upinzani. Namnukuu

Ukinunuliwa na CCM utakuwa

Used
Misused then
Abused

Sasa naamini jeshi letu limefikia stage ya pili (misused)

Likifikia stage ya tatu (being abused) naamini halitakubali litajibu !

Tusifike huku wote sisi kwasasa ni watoto wa John Joseph Pombe Magufuli.

Huu ndio ujumbe wangu wa mwisho wa siasa za Tanzania nitarudi Tena mwakani baada ya uchaguzi.

Tukutane jukwaa la mapenzi (MMU)
Bila shaka atakuelewa maans humu atakuwemo tu. Ni kiongozi wetu ni vema akasikiliza hoja hizi.
 
Mkuu wa majeshi

Jenerali Mabeyo

Kuna member humu jamiiforums aliwahi kusema akirefer wahamiaji wa CCM toka upinzani. Namnukuu

Ukinunuliwa na CCM utakuwa

Used
Misused then
Abused

Sasa naamini jeshi letu limefikia stage ya pili (misused)

Likifikia stage ya tatu (being abused) naamini halitakubali litajibu !

Tusifike huku wote sisi kwasasa ni watoto wa John Joseph Pombe Magufuli.

Huu ndio ujumbe wangu wa mwisho wa siasa za Tanzania nitarudi Tena mwakani baada ya uchaguzi.

Tukutane jukwaa la mapenzi (MMU)

Toka siku ile Magufuli amepokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi Arusha, wakati jeshi limetengwa kabisa kikatiba na siasa, toka siku nilipata shaka kubwa na weledi wa jeshi hili. Kwa sasa naona wazi limeamua bila aibu kufanya siasa rahisi.
 
Kuna ukweli fulani,nilikuwa sijaugundua. Huyu boss wa TAKUKURU asitumie uniforms za jeshi akitoka hadharani kwa issues za raia(mf kutoa taarifa fulani,hafla/dhifa za raia nk). Kuna ubadhirifu unatokea serikalini,ila hawashughuliki,lakini tunaona kwa wafanyabiashara/wasounga juhudi wanavyokimbizwa.
Nilikuwa na kawaida ya kuwapa msaada wa usafiri wajeda fulani wakati nawahi kibaruani,ila karibuni niliacha baada ya kumwona boss wa pccb akiwa kapiga uniforms yenye mavyeo mengi,nilidhani wajeda wako nyuma ya haya mateso.
Jeshi letu lisitumike kwenye mambo ya raia
 
No offence. Lakin boss wa takukuru basicaly bado ni askari wa jwtz.
Takukuru ni detachment tu.. lakin haimuondolei uaskar wake
 
Back
Top Bottom