Juu ya DOWANS: Mwakyembe ashangaa kutaka kulipa matapeli

Tatu, Ngeleja, Werema na Pinda, wote hawa ni wanasheria na wanajua wanasema nini, achilia furahisha genge!

Pasco hata Sitta, Mwakyembe na some members humu JF ni wanasheria pia hivyo wao pia wanajua wanasema nini!!!!!!
 
Nyambala, mikataba yote inatawaliwa na sheria ya mikataba, 'law of contract' hata ndoa ni mkataba. Ikishafungwa, hata kama ni illegal marriage, ni mahakama tuu ndio yenye mamlaka ya kutamka it is illegal, sio bunge, sio kamati ya bunge na sio mtu yoyote.

Baada ya kamati ya bunge kutambua kuwa richmond was illegal company, serikali ilipaswa kwenda mahakamani fasta na kuuvunja mkataba huku mahakama ikitangaza mkataba ule ni illegal. Kwa vile hakuna chochombo chochote kilichotangaza kuwa mkataba ule kuwa ni illegal,pamoja na illegality yake, umeendeleav kuwa legal mpaka leo tunapolipishwa!.

ICC pia imeponda hoja za usajili na legality ya richmond kwa sababu subject mater hapa sio nani ni nani, wala kampuni ipi imesajiliwa wapi, subject matter ni majereta ya kuzalisha umeme wa dharura, ni majereta ya ukweli na umeme wa ukweli. Msingi wa fidia ndipoo ulipolalia hapo!.

Suala hili limefanywa kisisas sana kulika kihalisia, serikali ilivunja mkataba wa kuilipa dowans capacity charge ya shilingi milioni 150 kwa siku, lakini tukakubali kuilipa IPTL shiling milioni 300 kwa siku na lita za mafuta laki 6 kwa siku!.
 
Duh hii habari haiwezekani ikawa imeandikwa na gazeti la Uhuru tena la CCM ..... duh
 

ICC hata waiweke Dowans kwenye cold list Tanzania itapiga kazi za kimataifa kwanza Dowans haina inchi inapotokea zaidi ya tANZANIA, na pia kama umesikia mitambo ni ya Richmond na sasa Richmond wamefungua kesi Marekani kutaka walipwe wao badala ya Dowans na hapa Tanzania Dowans tANZANIA nao wanataka walipwe wao badala ya Dowans SA
 
Nyerere alishawahi kumwambia Rais Kabila Sr. usilipe madeni ya nje ya hovyohovyo kwa manufaa ya nchi yake ya Kongo. Hilo linashindikanaje hapa kwetu wakati aina ya mikataba ni ile ile? tena nafuu hata ile ya Kongo ilikuwa na kauwazi kidogo kuliko huu uliogubikwa na wizi wa dhahiri? Nadhani shida ni Uthubutu wa viongozi na pengine malipo hayo yanakwenda kwao wenyewe.
 
Mag3, mikataba ni makubaliano huru baina ya watu wawili.
Vpengele vya mikataba ni utekelezaji wa makubaliano hayo.
Kila mkataba lazima uwe na kipengele, cha endapo kutatokea matatizo, mtasuluhishwa vipi.
Wote wawili mkakubaliana sheria za kutumika ni za Tanzania, msuluhisi ni ICC na mkakubaliana atakacho amua ndicho, yeye ndie mwamuzi wa mwisho, uamuzi wake hauhojiwa na jombo chochote, bali utasajiliwa tuu kwa utekelezaji!

Makubaliano hayo ni binding na sealed, wote wakaanguka saini kuyakubali, that is the deal and its done,
hakunas zaidi ya hapo, labda kama ni kujifurahisha tuu, na kila siku iendayo kwa Mungu, deni linazidi kwa milioni 7.5 ILI USIENDEKEZE DILLY DALLIYING. THE SOONER UNALIPA THE BETTER!.
 
Hivi Mwanasheria Mkuu anajisikieje pale ambapo anasoma habari kama hii ya DR. Mwakyembe? Dr. Mwakyembe ni kama amemkashifu AG kwa kumwambia hata mwanafunzi wa sheria wa mwaka wa kwanza hawezi kupoteza kesi kama hii!!
 
Hatukatai kuilipa Dowans,lakini kabla ya kuilipa ni lazima tujue uhalali wa malipo hayo!!
 

Si uliona shida na dhiki tuliokuwa nayo wakati wa Nyerere kwa ubishi wake? Mwisho akasalimu amri, rejea LONRHO wakati wa Nyerere.
 

Pasco toka lini sheria ikawa kama fizikia?????????? Mimi siyo mtaalamu wa sheria lakini huwa tunasikia huko mambo ya circumstantial, intention,good or bad faith etc. Which means kuna uwanja mpana zaidi wa kujenga hoja kadha wa kadha kwenye kila shauri!

Kwenye fizikia mfano Newton's third law of motion inasema "Action and Reaction are equal and opposite" haijalishi ni usiku, au kuna vita, au hujala, umefumaniwa n.k it will remain that way. Nashangaa kuona kwenye hili la Dowans sheria nayo inalinganishwa na fizikia, hii ni toka lini?

How come eti sasa tunaambiwa swala hili liliendeshwa kisiasa, nani alifanya siasa na ni kipi katika awamu hii ya nne hakiendeshwi kisiasa hapo Tanzania?????

Nilitoa mfano huu kwenye thread nyingine kule vipi unaweza kututoa tongotongo as to how sheria goes?

"Una kiwanda cha matofali akaja mtu kuomba kazi ya uhandisi ukampa. Say Katika sheria za Tz mtuu haajiriwi kama mhandisi kama hayuko registered. Ila anakuwa exempted kama ni registered kwenye any of the common wealth countries. Mhandisi wako akakupa vyeti kuthibitisha kwamba yeye yuko registered India. Under similar influence of joy or drugs and even alcohol mkawekeana maandishi kwamba ikitokea mkataba umevunjika kati yenu kwa sababu yeyote ile utatakiwa kumlipa mtu huyo sh milioni 200. Lakini baada ya miezi kama sita unagundua kwamba mhandisi huyo hayuko registered India kama alivyodai unaamua kuvunja nae mkataba. Anakupeleka mahakamani kutaka m 200 zake wewe unagoma. Utaratibu unakuwaje ?"

 
Si uliona shida na dhili tuliokuwa nayo wakati wa Nyerere kwa ubishi wake? Mwisho akasalimu amri, rejea LONRHO wakati wa Nyerere.


Kwani Lonrho nayo ilikuwa kampuni ya kitapeli?
 
Si uliona shida na dhili tuliokuwa nayo wakati wa Nyerere kwa ubishi wake? Mwisho akasalimu amri, rejea LONRHO wakati wa Nyerere.
Pitia tena ujue nimeandika nini kabla kujibu. Una haraka sana katika kujaribu kutetea wizi huu wa mchana.
 
mwakyembe mpaka leo hajaisoma hukumu ya icc. hata jf tumeisoma. naona angeiomba aisome kwanza na baada ya hapo kusema ya kwake.

kuna mtu anajua nini kimemzuia mwakyembe kuisoma hukumu hii. mwanasheria mkuu na hata mawakili binafsi wanasema wameisoma.

mwabie aje jf aisome.
 
Mkuu nadhani ulimaanisha wakilipwa
 

umemsahau pinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…