Just for curiosity: Wasanii wanalipwa Shilingi ngapi Youtube?

Just for curiosity: Wasanii wanalipwa Shilingi ngapi Youtube?

Angalau wewe umeuliza. Inashangaza hadi sasa hivi kuna watu wengi sana ambao hawaamini kuwa mtu anaweza akatengeneza mkwanja kwa internet tu... Japokuwa stori na shuhuda ni nyingi ila bado watu wabishi.

YouTube ni njia moja wapo tu. Kama una kismati na ngekewa unatengeneza mamilioni ya pesa kabisa. Cha msingi ni content ambazo zitashika watu.

> Ilivyo ni kwamba, Google inalipa asilimia 68% za mapato yake ya matangazo kwa chaneli husika ambayo imesajiliwa kulipwa. Kwa hivyo kwa kila shilingi 100 za kitanzania, kwa mfano, Google inawalipa wamiliki wa content husika shilingi 68.

Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa niliyoipata Google.

> kama YouTube channel inao uwezo wa kutengeneza hadi shilingi 41,500/= za kitanzania kwa view 1,000. Hiyo ni asilimia 100% ya mauzo. Je asilimia 68% ya hiyo 41,500/= ni shilingi ngapi? 41,500 × 68 ÷ 100 = 28,220. Hivyo kwa kila views elfu moja, mtu anatengeneza 28,220 za kibongo.

Turejee kwenye swali lako: Views milioni 1 ni sawa na shilingi ngapi? 1,000,000 × 28,220 ÷ 1,000 = 28, 220,000.
Big up kiongozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana watu wanazua scandle halafu inatupiwa YouTube,akijua kabisa ataokota idaidi kubwa ya viewers......
 
Affiliate marketing au advertising ni mfumo ambao unatangaza biashara au bidhaa ya mtu, na unalipwa kwa commissions ya mauzo yanayo tokana na tangazo lako.

Mfano: mtandao kama www.ajiras.com una mfumo huo, ukijiunga na kuchukua link yako au link ya huduma yoyote inayo uzwa mule, na kupost labda kwenye facebook groups, jamii forums au hata kwenye blogs na whatsapp

Mtu Akiibonyeza link yako, system ina gundua na kukumbuka Kuwa kaona tangazo kwako, akinunua huduma yoyote unapata % ya mauzo.

Sent using Jamii Forums mobile app
got you.ila sidhani kama huyu jamaa wa jf anapiga mkwanja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom