LD
JF-Expert Member
- Aug 19, 2010
- 3,014
- 574
Ujue mtu anapoamua kujiunga mara nyingi anakuwa na jambo linalomkuna au kumsukuma. Jambo hilo laweza kuwa shida ya maisha - anaona hapa JF anaweza kusaidiwa. Au pia mtu anajiunga baada yakuvutiwa na mijadala - anaona aingie naye atoe mchango wake. Kwa hiyo mtu anapojiunga mara moja anaweka mbele yetu kitu/ shida iliyomleta hapa. Ndo mana unaona junior wengi wanaanza kutoa shida zao zilizowabana, mf kutafuta wachumba, wake, kutafuta tiba kwa ugonjwa, kuomba ushauri kwa shida za familia, nk. Lakini mtu huyu baada ya kutoa madukuduku yake anakuwa hana zaidi jipya. Anakaa na kutulia jamvini, na kuanza kutoa michango mbalimbali katika uzi zinazoanzishwa. Kumbe sisi wazee wa JF tulishajieleza shida zetu siku nyingi, sasa tumekaa na kutulia jamvini.
Babuyao nakubaliana na mtazamo wako huu!!! Kuna ukweli katika hili. Ingawa kuna wengine wanaamua tu kupost bila kufikiria ni nini cha kupost hata kama anatafuta mchumba kweli.