Juni 07: Siku ya Usalama wa Chakula Duniani (World Food Safety Day)

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Chakula salama ni miongoni mwa vichocheo muhimu vya Afya njema. Vyakula visivyo salama ni chanzo cha magonjwa mengi. Kila mmoja wetu wajibu katika kuhakikisha usalama wa Chakula katika hatua zote za mnyororo wa thamani, kuanzia kinapozalishwa hadi kinapomfikia mlaji wa mwisho

Mbali na madhara yake kiafya, Chakula kisicho salama pia huathiri Sekta mbalimbali zikiwemo Biashara na Utalii, hivyo kukwamisha Maendeleo

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), Mtu 1 kati ya 10 duniani huugua kutokana na kula Chakula kisicho salama

=======

Foodborne diseases affect 1 in 10 people worldwide each year. There are over 200 of these diseases - some mild, but others deadly.

The United Nations General Assembly established World Food Safety Day in 2018 to raise awareness of this important issue. WHO and the Food and Agriculture Organization of the United Nations (FAO) jointly facilitate the observance of World Food Safety Day, in collaboration with Member States and other stakeholders.

This year’s theme, “Safer food, better health”, highlights the role that safe, nutritional food plays in ensuring human health and well-being and calls for a set of specific actions to make food safer.

We all have a role to play; whether we grow, process, transport, store, sell, buy, prepare or serve food, food safety is in all our hands. And if we work together, we can all help achieve safer food for better health.
 
Naomba nitoke nje, kumradhi

Taarifa zilizopo kwenye vianzio vya habari Marekani: Taasisi kadhaa za huko zimetoa tahadhari kuhusu uwezekano wa kuongezeka kwa Ukosefu wa chakula duniani. Sababu zikiwa vita vya huko Ulaya(ukraine)na ongezeko la joto duniani kuchochea Ukame ambao tayari umeshaonekana kuathiri nchi jirani kwetu, yaani Kenya, Ethiopia, Somalia...pamoja na nchi zingine Ulaya.

....kwa hiyo "safer food, better health" binafsi naona ni kinzani na Taarifa zilizopo...Vita Ukraine, Ukame, milipuko ya bei n.k n.k

Tuombe Tanzania yetu iweze kujikimu. Tutumie maarifa na sio Siasa.

Hata hivyo ni muhimu tukaitikia wito huo wa kuwa 'chakula salama kwa afya zetu'... na kuipa umuhimu kwa kutoa elimu kwa Wananchi wetu!
 
Watanzania tunakula tusicho kichagua na tunachagua tusichokula.

Yani kimsingi tunakula vyakula vya hovyo sana aseee...hasa kwa watu wa dsm wanaoishi maisha ya chini.

Turudi kwenye misingi ya ulaji bora na sio bora kula.
 
Watanzania tunakula tusicho kichagua na tunachagua tusichokula.

Yani kimsingi tunakula vyakula vya hovyo sana aseee...hasa kwa watu wa dsm wanaoishi maisha ya chini.

Turudi kwenye misingi ya ulaji bora na sio bora kula.
Ntemi:
Ni vyakula gani hivyo vya "hovyo"?

Wadondoshee wasomaji wengine na hata kamfano kamoja ka misingi ya ulaji bora?
 
Back
Top Bottom