Jumuiya ya Mabohora Tanzania wamkabidhi RC Makonda vifaa vya kujikinga na Corona

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,810
11,978
1587999003613.png

Jumuiya ya Dawoodi Bohora Tanzania leo imekabidhi vifaa mbalimbali vya kujikinga na corona vyenye thamani ya Shilingi Milioni 27 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kwa lengo la kuwakinga wananchi wa Mkoa huo.

Akipokea Vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dr. Rashid Mfaume amesema miongoni mwa vitu vilivyotolewa ni pamoja na Vifaa vya kuzuia maambukizi, vifaa vya kinga binafsi, vyakula vya kujenga mwili, sabuni, dawa za kunawa mikono na mashine za kuua mazalia ya bacteria.

Aidha Dr. Mfaume amesema vifaa hivyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona ambapo amewataka wananchi kuendelea kuchukuwa tahadhari na kufuata kanuni na maelekezo yanayotolewa na Wizara ya Afya.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Jumuiya ya Mabohora Bw. Murtaza Adamjee amesema Jumuiya hiyo itaendelea kuunga mkono Juhudi za Serikali ya Mkoa huo katika mapambano dhidi ya Corona ambapo pia wameipongeza Serikali kwa jitiada wanazozifanya kukabiliana na corona.
 
Toa barakoa, toa vitakasa mikono na mfano wa hivyo

Barakoa haziwezi kutumika kwa matumizi tofauti na yaliyokusudiwa na ndio sababu safar hii wengi wanatoa Donation in kind badala ya hard cash
Wengi tunapenda kutoa lakini tukikumbuka tetemeko la Kagera na ajali ya wanafunzi wa Lucky Vincent moyo wa kutoa unakufa kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...
Corona imetusaidia kutambua tatizo la uhaba wa maji tiririka Tanzania
... mimi corona imenisaidia kutambua kinywani mwa mwanadamu kunatoka mauchafu ya ajabu sana including viruses and bacteria sema mengine hayana athari ndio maana.
 
View attachment 1432250
Corona imetusaidia kutambua tatizo la uhaba wa maji tiririka Tanzania
Uhaba wa maji ulikuwepo tangia enzi hizo mkuu na tunalitambua kuhusu hilo usitake kusingizia corona.
Tunatambua ya kuwa hata pale makao makuu ya nchi kuna wananchi walikuwa wanatembea umbali wa zaidi ya kilomita 10 kutafuta huduma ya maji.
NB:Tunaomba msidiriki kutugawa katika kipindi hichi kigumu cha corona kwani tunahitaji kushikamana kwa hali na mali
 
Lilikuwepo na mliahidi mtalitatua katika ilani za CCM. Miaka minne madarakani mmefanya nini?
 
Back
Top Bottom