Nadhani ni wakati wa serikali kutoa elimu kwa vijana juu ya ujasiliamali
ni wajibu wa serikali ndio maana watu wanalipa kodi, pia kuelimisha vijana ni bora kuliko unavyodhani , katika wasio na ajira wanatofautiana malengo na kiwango cha mahitaji, kuna mwingine hana ajira lakini ni mtu mwenye ngazi ya elimu ya juu na mwingine Hana ajira na pia ajui kusoma wala kuandika, hivyo unavyoliangalia tatizo ili lazima uliangalie kwa undaniKila kitu lawama kwa serikali, hivi huu muda wanaokaa kwenye internet si wangeutumia kusoma 'enterpreneurial skills'? siku elimu ni kama bure labda kama unataka vyeti ndio inabidi uende chuo lakini kama unajua kusoma na kuandika kuna fursa nyingi sana za kujielimisha. Sasa mtu kutwa anashinda kusoma magazeti ya udaku halafu unadai serikali ikuelimishe, tena wengine wana elimu ya chuo kikuu ambayo siku hizi pamoja na mambo mengine wanafundisha pia somo la enterpreneurship.
Hili ni wazo au kichekesho? Nikiwa mwanachama wa jumuiya hii leo wakati sina kazi, vipi kesho nikipata ajira! Itakuwa jumuiya ya kwanza na ya aina yake. Wakati katibu na mwenyekiti wanaandaa mkakati fulani, unakuta katibu kapata kazi kwa hiyo mipango yoote inabidi ianze upya, tehe tehe tehe!
Nadhani ni wakati wa serikali kutoa elimu kwa vijana juu ya ujasiliamali
wakuu jmosi kikao cha kwanza
Kwa kwenda hapo kinondoni ndio mtapata kazi?wakuu jumamosi ijayo kikao wamependekeza kifanyike biafra kinondoni
wakuu jumamosi ijayo kikao wamependekeza kifanyike biafra kinondoni
Ingawa sijui ni jumamosi ya tarehe gani!!
Binafsi nadhani kuna mambo yamsingi yanatakiwa kufanyiwa kazi na kuwekwa sawa kabla ya mkutano huo.
Kwanza, ilitakiwa kuwasiliana na taasisi hizo ulizozitaja zitakazo husishwa na uundwaji wa bodi hiyo juu ya jumuia hiyo na malengo yake. Hii itasaidia kujua kama hakuna jumuia au taasisi inayofanya kazi zinafanana na hizo ambazo jumuhia hii mpya inataka kufanya(Kupunguza duplication ya jumuia/taasisi).
Pili , Ajenda za mkutano hazipo wazi, hajulikani nini kitazungumzwa huko mkutanoni ili washiriki waweze kuandaa hoja za msingi vinginevyo mkutano huo utakuwa kama "kijiwe" cha watu wasio na ajira jambo ambalo nadhani hukusudii liwe.