Kwanini ngumbaro na wa elimu ya kawaida ndio wanatoa ajira zaidi kuliko wasomi?

mlinzi mlalafofofo

JF-Expert Member
Apr 20, 2008
277
548
Katika hali ya kawaida ilitegemewa wasomi wasaidie kuongeza nafasi za ajira mpya kwa kuanzisha biashara na makampuni yatakayotoa nafasi mpya za ajira, hasa kwa vijana.

Lakini cha ajabu kwa bongo, wasomi wameendelea kujipambania wao wenyewe kwa kukesha na bahasha za kaki wakisaka ajira kwenye siasa na wengine kung'ang'ania ajira za kuajiliwa kiasi unashangaa elimu waliyoipata inaisaidia vipi jamii.

Maana saivi kuna wimbi kubwa la vijana wasio na ajira. Kama kungekuwa na ongezeko la makampuni mapya si yangesaidia kupunguza vijana wasio na ajira uko kitaani.

Badala yake ngumbaro na wenzao wenye elimu za kawaida tu za shule ndo mara nyingi unaskia wakianzisha biashara na kuajiri. Hii haijakaa sawa. Wasomi kamateni nafasi yenu mlisaidie taifa linawategemea.

Hii sauti inatosha wakuu?
 
Hii inatokana na tendence ya kusoma ili uajiriwe tena uajiriwe serikalini. Mzazi anajua mtoto wake akihitimu tu ataajiriwa. Hakuna mtoto anayepeleka mtoto shule akapate ujuzi wa kujiajiri. Wapi mtu anasoma mpaka chuo kikuu aje ajiajiri? Kama wapo ni kidogo sana tena wana wafadhili katika miradi yao. Hawa wenye elimu ndogo kuajiri wasomi walithubutu kufanya miradi kwa kuwa hawakuona kuwa na sifa za kuajirika ikabidi wa struggle ili waishi
 
Back
Top Bottom