Serikali ya Tanzania Yamwaga Ajira 500 Kwa Wanawake wenye Sifa.Kituo Cha kazi ni Saudi Arabia.

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,049
49,733
Vijana wa kike kwenye sekta ya Afya mumemwagiwa Ajira ambazo zitakuwa ni Saudi Arabia.

Chagueni mtaenda Saudia au Israel kwenye vita.?

=====

DAR ES SALAAM: HATI ya makubaliano ya ushirikiano wa masuala ya kazi na ajira yaliyoingiwa kati ya Tanzania na Saudi Arabia imeanza kuzaa matunda baada ya Saudi Arabia kutoa nafasi 500 za ajira kwa wauguzi wa kike nchini.

Akitangaza nafasi hizo Dar es Salaam, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Cyprian Luhemeja alisema kuwa nafasi hizo ni kwa ajili ya wauguzi wa kike wa Kitanzania wenye elimu ya Stashahada na Shahada.


Luhemeja alisema nafasi hizo ni matunda ya hati ya makubaliano ya ushirikiano wa masuala ya kazi na ajira ulioingiwa kati ya Tanzania na Saudi Arabia ambayo yalisimamiwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Alisema Watanzania wenye ujuzi na sifa zilizobainishwa wanatakiwa kuomba kwa kujisajili kupitia NLMIS pamoja na kutuma wasifu binafsi kwa njia ya barua pepe ya esu@taesa.go.tz hadi kufikia Desemba 31, 2023.

Luhemeja alisema mchakato wa kuwapata wauguzi hao unatakiwa kukamilika ifikapo Januari 10, 2024, hivyo waombaji wajitahidi kukimbizana na muda. Alisema kutokana na ufinyu wa muda tayari amekiagiza Kitengo cha huduma za ajira (TaESA) kuhakikisha kuwa hadi kufikia Januari 10 wote wenye sifa wawe wamepatikana kabla ya kukutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako.
Aidha, alisema wamepokea maelekezo kutoka kwa Rais Samia ya kuharakisha mazungumzo yanayoendelea kwa ajili ya uingiaji mikataba na nchi zingine 10 ili kuwapatia Watanzania fursa za ajira nje ya nchi. Alisema kuwa lengo la Ofisi ya Waziri Mkuu ni kuhakikisha kuwa mazungumzo hayo yanakamilika ndani ya Januari 2024 na kuwataka Watanzania wanaotamani kufanya kazi nje ya nchi katika fani mbalimbali.

Imeandaliwa na Mwandishi Wetu

1704704183059.jpeg
1704704203839.jpeg

My Take

Ronaldo Yuko Saudia kula pesa.
 
Yakitokea ya kutokea huko saudi arabia msije kumwaga povu hapa kama wale walioenda kwa mafunzo ya kilimo huko israel.
 
Vijana wa kike kwenye sekta ya Afya mumemwagiwa Ajira ambazo zitakuwa ni Saudi Arabia.

Chagueni mtaenda Saudia au Israel kwenye vita.?

View: https://www.instagram.com/p/C1EA4Lwolli/?igshid=NmJiYWZiY2E0Mg==

My Take
Ronaldo Yuko Saudia kula pesa.

View: https://twitter.com/wizara_afyatz/status/1737381475215974528?t=94gjdbEhowbrf0GmLO4IBg&s=19

Hao wanaitwa MANESI, lakini wanakwenda kufanya kazi za kuwaosha wazee na vibibi visivyojiweza kwenye nyumba za kulelea wazee.

Wawe tayari kukamata mavi, mikojo na makamasi ya vigagula na vijeba
 
Hao wanaitwa MANESI, lakini wanakwenda kufanya kazi za kuwaosha wazee na vibibi visivyojiweza kwenye nyumba za kulelea wazee.

Wawe tayari kukamata mavi, mikojo na makamasi ya vigagula na vijeba
Mbona Ulaya Huwa mnawaosha?
 
Hakuna kazi za unesi huko wanaenda kukinga midomo kunyewa na waarabu midomoni wakirudi huku kama vichaa na wengine wanajitupa kwenye magorofa kwa mateso makali
 
Tunajua saudi arabia ni nchi ya kiislam, tena kinara wa uislam duniani je wakristo nao watapata nafasi za ajira hizo, wakipata vipi watafanya ibada zao za kikristo, kuna makanisa saudi arabia. Mi ni mpentekoste nikiende huko nikute kuna kanisa lenye imani kama yangu msiniletee ukatoliki na usabato siabudu huko, nitasali wapi? Wasaudia wakinikuta nasali ibada yangu nitawapiga injili na kuanzisha kanisa huko, sio mbaya Mungu ni mwema na anapenda watu wote tuheshimiane dini na imani zetu
 
Mi ni mpentekoste nikiende huko nikute kuna kanisa lenye imani kama yangu msiniletee ukatoliki na usabato siabudu huko, nitasali wapi? Wasaudia wakinikuta nasali ibada yangu nitawapiga injili na kuanzisha kanisa huko, sio mbaya Mungu ni mwema na anapenda watu wote tuheshimiane dini na imani zetu
Huko Dunia ya Kiarabu ukiongea Kanisa utakalolikuta ni RC tu. Kwa hiyo utachagua mwenyewe kusali RC au kuishi kama mpagani. Hizi takataka zenu za TAG au EATG au Mwamposa hazipo
 
Mimi nimefafanua tu. Kuwa wasitegemee kufanya kazi kama wanazofanya Manesi wa Muhimbili. Wasije wakashtuka wanapokabidhiwa kuwaosha vikongwe mavi na mikojo na makamasi
Kikubwa maokoto ya zaidi ya mil.2-3
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom