Jumuia ya wasio na ajira

Sawa kabisa vijana.

Tamasha la wasio na kazi litaiamsha serikali usingizini.

Jipangeni sawa sawa ili muwe na matawi mikoani, wilayani na ngazi ya kijiji.

Hii itakuwa jumuiya yenye nguvu sana Tanzania.

Hata wale walio na ajira isiyo rasmi, pia jiungeni.

Now, how to start and connect yourselves?- a challenge.....

Mkuu najua kuna changamoto nyingi ila nina imani kubwa sana na michango yenu hapa JF. Naamini nitafanikiwa kwa msaada wa michango yenu ya mawazo
 
Sijafaham tunaanza vp.labda kwanza tuanze na kutazama 7bu zinazofanya vijana tusifikie malengo katika soko la ajira. Tena tutazame ajira zote,kuajiriwa ama kujiari.kwa kuanzia tuanze na ajira za kuajiriwa tutamalizia kujiajiri.
 
Kweli ajira ni ishu sana kwa vijana. Tatizo ni kwenda shule kwa malengo ya kuja kuajiriwa badala ya kwenda shule ukitegemea kuja kujiajiri wenyewe!

sio tatizo letu. System ya elimu bongo ndo iko hivyo, tunasoma ili tuajiriwe. Mfumo wote ufumuliwe wote. Na wote hatuwezi kuwa wajasiamali kwa sababu nacho ni kipaji, pili Vijana hatuna dhamana ya kuweka bank tupate mikopo. Elimu yenyewe tumekopeshwa.
 
mwanzo kwa vijana wasio na ajira ila msiwasahau na wale wanaolipwa mafao macdogo kulingana na kazi zao, mkifanikiwa hili basi mtafanya ukombozi wa kweli katika kizazi na taifa la Tanzania
 
popote pale watu wataposhauri kukutana , kulingana na mawazo ya wengi

nimeanza, nashauri iwe mitaa ya kinondoni. nahisi kunafikika kirahisi na hakuathiriwi na mishemishe nyingi za mjini.
 
Kweli ajira ni ishu sana kwa vijana. Tatizo ni kwenda shule kwa malengo ya kuja kuajiriwa badala ya kwenda shule ukitegemea kuja kujiajiri wenyewe!

Lakini kumbuka kujiajiri bila kianzio kuna kazi! kama ungeelewa haya ungeonea huruma watu wasio na ajira. Kuna tofauti sana kati ya mtoto wa maskini na mwenye uwezo wa mali mnapojadili kuhusu kujiajiri. Mtu alie na uwezo anaweza akaanzisha biashra au kilimo na kadhalika. Je yule aliemaliza chuo na baba yake hana hata sehemu nzuri ya kulala na wakati huo kijishamba chake kimechukuliwa na mwekezaji unadhani ataanzia wapi?
 
Kaka umenena watu wengi hatuna ajira tukiunda umoja wetu itasaidia kuwa na sauti moja katika mambo ya kisera, muda mwingine kuwa na sauti moja juu ya serikali katika kuikosoa na kuishauli jinsi ngani inaweza kutoa fursa pana zaidi kwa wasio na ajira.
 
Wazo zuri ila tuwe makini tusigeuzwe mtaji wa kisiasa. Tupoteze muda mrefu kufikiria sisi kwa pamoja ni rasilimali gani tunazoweza kuzitumia ili kujiajiri na inawezekana kwa kuwa utakuwa mtaji ,kubwa wa taaluma mbalimbali. Tunaweza hata kufanya kazi za kijamii kwa kujitolea kwa kuanza mbele ya safari naamini tutakuwa tumepata uzoefu fulani na mtaji wetu ( uzoefu,uaminifu,umoja na mshikamano) utakuwa umeongezeka.Safari ianze mara moja!!!!!!
 
Back
Top Bottom