Jumba la Dharau: Sehemu ya kwanza

Jumba la Dharau: Sehemu ya kwanza

JUMBA LA DHARAU- SEHEMU YA SITA

Baada ya kupewa matumaini ya kwamba kesho tunapata dhamana na wote tutatoka katika jumba lile dhalili, furaha ya moyo wangu ilianza kurejea, kwani nilijipa moyo yakwamba nimebakiza usiku mmoja tu wa mateso katika jengo lile. Tulipoingia Sero jamaa mmoja ambae alikuwa karibu yangu alikuwa na anaadika jambo Fulani katika daftari lake mara nikaona amechana karatasi moja hivi kisha akaendelea kuandika.wakati huo wote mimi nilikuwa nimekaa kwenye kagodoro kangu niliko kabidhiwa na Nyapala wa Sero pamoja na Askae sero siku ya kwanza wakati naingia Gerezani. Basi nikamuulize yule jamaa hiyo karatasi uliyo ichana una kazi nayo, akaacha kuandika kidogo na kuniangalia kisha akanijibu hapana sina kazi nayo. Nikamwambia naiomba basi akaniambia ichukue. Basi kwa nikasogea hadi kwenye ukingo wa godoro langu nikanyoosha mkona mpaka kwenye godoro lake ambalo karatasi ilikuwa imedondokea na nikaichukua kisha nikarudi na nikakunja miguu yangu na kukaa mkao wa kuomba Dua, yaani niliikunja miguu yangu yote miwili kwa kuipishanisha kwa mbele. Na kuanza kuingalia ile karatasi yule jamaa alikuwa ananitazama tu muda wote, nadhani alikuwa anatakakujua kwanini nimechukua ile karatasi.
Nikamuona anaendelea kuandika huku akinitazama kwa jichola chini chini wakati huo namI naiangalia ile karatasi huku nikimtazama kwa macho ya wizi. Lengo langu lilikuwa namsubiria amalize ili nimuombe kalamu. Unajua maisha ya kule ni mashaka sana hakuna anaemuamini mwezie hasa kwa mahabusu ambao wanakesi mahakamani. Lakini naona mwenzangu uzalendo ukamshinda ikabidi anigeukie na kuniambia sasa unaomba karatasi bila kalamu au unataka ukachambie? Nikamwambia hapana nilikuwa nasubili umalize kuandika nikuombe na kalamu, jamaa akacheka cheka kisha akasema kwahiyo na karatasi ulikuwa unasubiri niishane ndipo uniombe? Daa maswali ya Gerezani na mahakamani hayapishashani kabisa, nikona hakuna haja ya kumjibu bora nikae kimya. Akaniangalia tena kisha akatikisha kichwa ishara ya kusikitika kisha akafunua mchago wa godoro lake na akatoa kalamu nyingine kisha akanipa. Na yeye akaendelaa kuandika mambo yake.
Unajua mimi napenda sana kuamdika mashairi palepale nikapata hisia ya kuandika shairi ndipo nilipo andika beti hizi za shari
Gereza ni jahanamu, ichomayo waharifu
Waharifu wanadamu, jamii imewakifu
Nami leo nimo humu, moyo una hitilafu
Ipo siku nitatoka kweye JUMBA LA DHARAU

Kwenye Jumba la dharau, kuna siku nitatoka
Japo sinto lisahau, kwa kushindwa kutoroka
Mola unipe nafuu, Mja wako nateseka
Kwenye Jumba la dharau, kunasiku nitatoka

Maisha ya Gerezani, binadamu kama mbuzi
Chakula ni kwa foleni, iwe wali au mchuzi
Nina imani moyoni, itanikwisha simanzi
Kwenye jumba la dharau, kunasiku nitatoka

Nilipo maliza kuandika ubeti huu wa mwisho, nikashangaa tone la maji limedondokea kwenye ile karatasi daaa….. maskini ya Mungu kumbe nilikuwa nalia, mara nyingi sikupenda kuonaneka dhaifu, hata ningepitia gumu gani huwa si ruhusu kutoa machozi lakini siku hii ilikuwa tofauti. Basi ilinibidi niamke na kwenda kwenye bafu iliyoko ndani ya Sero, nikafungua koki na kuanza kunawa uso. Nilipo rudi muda ulikuwa umekimbia sana, hivyo nikafungu lile hotpot langu la chakula kisha nikamkaribisa yule jamaa aliyenipa karatasi kalamu, yule jamaa alikubali mualiko wangu na tukaanza kula pamoja wakati tunakula yule jamaa akaniuliza kwanini ulikuwa uanalia , nikamwambia mbona mimi sijalia yule jamaa kawa anatabasamu huku anatupia mawe pangoni. Baada ya kumaliza kula na kupanga vyombo yule jamaa akaniuliza kwani ulkuwa unaandika nini? Nikamuonyesha ile karatasi nae akaangalia kisha akaanza kusoma nikamuona anabadilika sura na kuwa na sura ya huzuni, kisha akaniambia, shairi lako linanichoma sana. Akaniomba alinakiri kweye Dafari Lake.

Alipo maliza kuanzdika alinirudishia karatasi yangu kisha akafunika daftri lake kisha akaniambia akaniambia” wewe ulikuwa unalia mimi nilikuona lakini sikutaka kukukatisha kilio chako niliona ni nikuache ili umalize kutoa sumu ilikyoka moyoni mwako,najua una maumivu makali sana lakini tambu hizi jela zipo kwa ajili ya binadamu, na hao binadamu ni sisi,mimi na wewe pamoja na wengine ambao wako huko uraini, embu angalia ndugu yangu wakati sisi tuko hapa kuna watu wapo hospitalini hawawezi hata kuongea na wengine wamekata shauri na wanasubiria kifo tuu, lakini mimi na wewe tuko hapa kwa sababu tunatuhumiwa kwa makosa mbalimbali lakini wewe ni tofauti kidogo na mimi kwa sababu wewe dhamana yako ipo wazi lakini mimi dhamana yangu imefungwa, siku yoyote unaweza kutoka ndani ya jumba hili lakini mimi mpaka itolewe hukumu maana kesi yangu ni ya Mada. Na kama nitapatikana na hatia nitahukumiwa kifo au kifungo cha maisha lakini wewe ninauhakika kesi yako ni ndogo sana na haiwezi kukutia hatiani zaid ya kupoteza muda. “ Jikaze wewe ni mototo wa kiume na hii ni hatua ambayo unapitia lakini yataisha . Humu gerezani wapo wataalam mbalimbali wapo aminjinia, wapo madaktari wapo askali ambao nao wamefungwa, maarifa mengi yapo humu gerezani.
Mimi ni msomi nina shada ya teolojia elimu ya dini ya kikristo na nimeifanyia kazi muda mrefu sana hivyo nina uzoefu wa kutosha, kwa nilivyo kuangalia nimegundua kwamba wewe umeonewa “ yule jamaa alikuwa naongea kwa sauti ya chini sana, kwa mtu aliye umbali ha mita moja hasingeweza kusikia, hapo ilibidi nimuulize swali wewe umejuaje kama mimi nimeonewa, akasema katika baadhi ya masomo niliyosomea katika kada yangu ni pamoja na Saikolojia na falsafa, hivyo ninauwezo mkubwa wa kuwatambua watu kwa kuwaangalia tu usoni au kwa matendo yao machache tuu hapo naweza kumjua mtu tabia yake halisi.

Akaniambia ngoja nikuelezee wewe jinsi ulivyo, basi mimi nikawa na shauku kubwa ya kutaka kumsikilza maana nilijiona kama nipo kweye kioo cha kutazama tabia zangu akaniambia, wewe unasifa zifuatazo,
Wewe ni Jeuri, wewe unahasira sana, wewe ni kiburi sana lakini wewe sio mkatili na unahuruma sana maana uko tayari wewe kuteseka lakini watu wengine waishi maisha mazuri kwa mfano wewe upo humu ndani watu unao uliokuwa ukiwapigania wako nje wapo wachache wanaumia kwa kwawewe kuwa ndani lakini ninauhakika waliowengi watakuwa wanakusemea vibaya, pia kitu kikubwa ambacho kitakugharimu sana katika maisha yako wewe huwezi kupuuzia jambo na unapenda kuweka kumbkumbu ya makosa ya watu waliokukosea sio kwa sababu ya kulipa kisasi bali ni kwa sababu ya hupendi kurudia kosa hivyo mara nyingi utakuwa nao mbali,ningekuwa na uwezo ningekwambia ujifunze kusamehe lakini wewe umeubwa hivyo. Mimi nikushauri kitu cha mwisho usipende sana kumwamini mtu yeyote katika maisha yako sababu katika dunia hii wanafki ni wengi sana “ nadhani nimemaliza, na uniache mimi nijiandae kwa ajili ya kesi mahakamani maana kesho ni kesi yangu mbele ya jaji.

Maneno yake yalinipa faraja sana basi nikageuka katika godoro langu, nikaichukua ile karatasi niliyo andika shairi, nikaanza kuisoma tena huku nikwa na matumaini ya kwamba kesho nitatoka Gerazani

Je kesho nilitoka naomba ufuatilie sehemu ya saba ya simulizi hii ya JUMB LADHARAU
 
Back
Top Bottom