Jumba la Dharau: Sehemu ya kwanza

Jumba la Dharau: Sehemu ya kwanza

BONGE LA BWANA

Senior Member
Joined
Apr 14, 2015
Posts
199
Reaction score
168
Habari wana JF.... leo nataka kuanza kuwaletea simulizi kali na yenye mafunzo ndani yake. Simulizi hii ni ya ukweli kama ilivosimuliwa na mtunzi wa simulizi hii ndugu Rashid Karume ambae kwa sasa anapatikana Mkoa wa njombe. Kwa ruhusa yake mtunzi ameniruhusu nishare simulizi hii inayokwenda kwa jina la JUMBA LA DHARAU. Twende kazi sasa....

JUMBA LA DHARAU

MTUNZI: RADHID KARUME.


SEHEMU YA KWANZA

SIKU YA KWANZA NDANI YA GEREZA LA RWANDA NZOVWE MBEYA (JUMBA LA DHARAU) -2010

Ilikuwa siku ngumu sana mimi na Rafiki yangu,hakuna aliyeamini kwamba tungekuwa Gerezani, japo sisi tulikuwa wangen lakini sura zetu zilitangulia Gerezan kupitia vyombo vya habar Runinga na magazet. kila mfungwa na mahabusu walikuwa wanatuangalia huku wakivuta picha za kwenye Tv,

wakati hatujui nn cha kufanya mara kundi la watu likatuzunguuka na huku wakiwa na sura za furaha mmoja wao akasema KARIBUNI KWENYE JUMBA LA DHARAU, ni kama tulipigwa na butwaa sisi tulikuwa kimya tuu. Daaaaa siwez kusahau

Mara alikuja Askari magerez aliyechafuka kwa vazi lenye mamlaka kwenye mabega yake, alikuja pale tulipo kisha akasema ninyi embu nifuatane huku, basi sisi tukaanza kumfuta kwa nyuma, kisha yeye akageuka na kutuangalia akiwa na sura iliyojaa tabasamu languvu akatuuliza majina nasi bila hiyana tukamtajia, kisha tukaenda kuakaa jikoni ambako msosi wa jela unaandaliwa.

Maneno yake ndiyo huwa nayakumbuka kila ninapopata wakati mgumu, yule afande alisema "KARIBUNI VIJANA KARIBUNI SANA, HAPA MLIPO NDIO JELA MLIYOKUWA MKIISIKIA TANGU MKIWA WADOGO LEO MMEINGIA HAPA, NAJUA HAMTAKI KUAMINI LAKINI HAPA NDIO JELA NA HAMUWEZI KUROKA KWA SABABU KUNAULINZI WA MKALI, ANGALI ULE UKUTA ULIVYOKUWA MREFU WATAALAMA WANATHIBITISHA HAKUNA BINADAMU ANAEWEZA KURUKA ULE UKUTA, PIA NI MARUFUKU KUUSOGELEA ULE UKUTA KWA SABABU UTAPIGWA RISASI, ANGALIA KULE JUU, KILE NI KIBANDA CHA ASKALI AMBAPO ANAONA NDANI NA NJE YA GEREZA HIYO UKIJARIBU KUTOROKA UTAKUWA MWISHO WA MAISHA YAKO, JAMBO MOJA AMBALO NAWEZA KUWASHAURI LEO NA SIKU ZOTE ZA MAISHA YENU NI KWAMBA IKUBALI HALI, KUBALI UKO JELA NA HUWEZI KUTOKA LABDA WATU WA NJE WAJE KUKUTOA KWA SHERIA LAKINI WEWE HUWEZI KUTOKA, wakati Afande akitiririka mistari yote hiyo sisi tulikwa kimya tukimsikiliza baadae akatuliza niwaletee soda gani wote tukamjibu yoyote akamuita mfungwa mmjoja aliyekuwa na mkanda kiunoni akamwambia WALETEE SODA HAWA VIJANA, baada ya muda kidogo soda zikaja kisha afande akamwambia, Naomba nikukabidhi hawa vijana Hakikisha hawapati usumbufu wowote wakiwa humu ndani mpaka watakapo pata dhamana.
Baada ya hapo ikapigwa filimbi na wafungwaa wote na maabusu tulipanga foleni kuingia vyumbani( SERO) mm nikiuwa sero na 9 na rafiki yangu alikuwa Sero na 8

nilikutana na watu wenye akili nyingi sana waliofanya matukio ya ajabu we acha tuu

........Itaendelea
 

Attachments

  • jumba la dharau.jpg
    jumba la dharau.jpg
    35.2 KB · Views: 124
Born in Pretoria, Musk taught himself computer programming at the age of 12. He moved to Canada when he was 17 to attend Queen's University . He transferred to the University of Pennsylvania two years later, where he received a degree in physics from the College of Arts and Sciences and an economics degree from the
Wharton School . He began a PhD in applied physics and material sciences at Stanford University in 1995 but dropped out within a month to pursue an entrepreneurial career. He subsequently co-founded Zip2 , a web software company, which was acquired by Compaq for $340 million in 1999. Musk then founded X.com , an online payment company. It merged with
Confinity in 2000 and became PayPal , which was bought by eBay for $1.5 billion in October 2002.
 
JUMBA LA DHARAU - SEHEMU YA PILI

MTUNZI: RASHID KARUME

Ikumbukwe kwenye stori hii kinachoelezewa ni stori ya kweli kabisa ambayo imekuta mtunzi wa stori husika.. SASA TUENDELEE NA SEHEMU YA PILI YA SIMULIZI HII


27336570_1441627835947537_4576346012254289600_n.jpg


Baada kupanga foleni kwa ajili ya uhakiki wa Idadi ya wafungwa na mahabusu. baada ya muda kidogo Maafisa wa jeshi la magereza walijiridhisha ya kwamba idadi ipo kama inavyosomeka kwenye nyaraka zao ndipo tulipo ruhusiwa kuingia ndani ya sero kwa mstari .

nilipo ingia tu Sero alikuja mtu mmoja ambae simjui akanishika mkono na kuniambaia njoo kwanza hapa wakati tunakuandalia sehemu ya kulala. nilipata khofu kidogo kutokana na simulizi za Jela nilizokuwa nikisikia kabla lakini nilipiga moyo konde huku nikijiandaa kwa mapambano endapo litatokea jambo lolote la kutweza utu wangu. wakati pilika pilika zikiendelea za watu kutandika magodoro yao na kuweka mambo yao sawa mimi nilitumia dakika hizo chache kuichunguza ile Sero.

kilikuwa ni chumba kikubwa sana naweza kukifananisha na ukubwa vyumba viwili vya madara ya shule ya msingi. pia kilijengwa kwa ukuta mnene sana na mrefu sana urefu ule ni wastani wa mita 6. pamoja ma ukubwa Sero ile lakini ilikuwa na madirisha madogo sana yalikuwa katika kimo kirufu sana miale ya macho pekee ndiyo iliyokuwa na uwezo wa kufika, pia nilitupa macho mlangoni ulikuwa ni mlango wa chuma cha pua, Ghafla nikakumbuka maneno ya yule Afande "IKUBALI HALI NA HUWEZI KUTOROKA"

Ghafla nikaona watu wawili wakija pale nilipo kwa pamoja, kwakweli kwa kipindi hicho nilikuwa na mashaka makubwa mno na kila mmoja aliyekuwa jera. walipofika pale wakaanza kuongea na mwenyeji wangu,

"Oya huyu dogo tumpangie wapi?:" aliuliza mmoja wapo pia akajibiwa itabidi tumuulize maswali ndio tumpangie pa kulala. kwakweli muda wote nilikuwa nawashangaa tu. ndio wakaanza kujimbulisha kwangu . kumbe walikuwa ni viongozi wa SERO kulikuwa na NYAPALA WA SERO, PAMOJA NA ASKARI SERO.hao ni watu wakubwa sana ndani ya Sero.

waliniuliza maswali kadhaa juu ya kesi iliyonileta gerezani, wakaniuliza kama kesi yangu ipo mahakama gani ya wilaya au mahakama ya nwanzo, wakaniuliza kama kesi yangu inawakili baadaya kuwapa majibu walikubaliana kwamba nina hadhi kubwa, hivyo nikapangiwa sehem safi ya kulala na sio chaka ambayo ina kunguni na chawa wa kutosha.

baada ya dakika chache nikasikia muda wa Ibada ndipo watu wakajikusanya na kuanza kufanya ibada walianza Wakristo wakafanya ibada na kuimba nyimbo mbalimbali nilifarijika kuona kumbe hata Mungu anapewa nafasi gerezani kisha nikasikia adhana kumbe hata waislam nao walipewa nafasi ya kufanya ibada basi nimi ikabidi niende kuchukua udhu niungane na wenzangu kufanya ibada baada ya kufanya ibada ikawa ni lazima nijitambulishe kwa wenzangu , nikaanza kujitambulisha kwa kiswahili maskini ya mungu hakuna aliyenielewa, jamaa mmoja alikuwa anajua lugha ya kingereza ndio akaniambia English Pleasa, Daaaaaa nilipo angalia vizuri kumbe wale wote walikuwa ni Raia wa Somalia na wa Ethopia hawajui kiwahili wana jua kisomali na kihabeshi pekee hivyo nilivyokuwa najitambulisha kwa kingereza yeye anatafasiri kwa kisomali na Kihabesh

Baada ya hapo tukatawanyika na watu waka wanipiga stori mbalimbali zikiwemo za uchaguzi maana ulikuwa mwaka wa uchaguzi 2010. huku wengine wakisikiliza habar kupitia radio zao. katika kipindi cha Radio ukasomwa mukhatari wa habari ikiwepo na tukio lililonileta sisi JELA, watu wote walikaa kimya kusikiliza ile habar,

kwakweli niliumia sana kusikiliza ile habari kwani ukwli ulipindishwa sana, watu wengi waliopata kusema waliongea uongo mwingi na ukweli mchache usio kuwa na faida kwetu.

ulipofika muda wa kulala Gereza zima lilikuwa kimya, kwakweli mm sikuweza kupata usingizi nikiwa na muwazia Rafiki yangu huko aliko lala je amepewa hifadh nzuri kama niliyopewa mimi?
nikakumbuka Ahadi yetu kushikamana juu ya jambo hili nikajikuta machozi yananidondoka , sikuweza kupata usingizi mpaka kuna kucha ,,,,,,,,,,,,

ITAENDELEA..............

Moja ya picha ambayo inanijia mara kwa mara ni picha juu ya maisha ya Gerezani



27336570_1441627835947537_4576346012254289600_n.jpg


LikeShow more reactions
Comment
 
JUMBA LA DHARAU –SEHEMU YA TATU

Hata usiku uwe mrefu vip lakini asubuhi itafika, pamoja na usiku wa mashaka mengi uliojaa mang’amng’am lukuki lakini asubuhi ilifika . utaraibu wa kutoka ndani ya Sero ni kama wa kuingia ambapo maafisa wa Geraza ni lazim wahakiki idadi ya wafungwa na mahabusu kama ipo sawasawa
Baada ya kutoka Sero pilikapilika za Gerezani ziliendelea katika ya wafungwa na na Askari magereza, walioliokuwa wanajiandaa kwenda mahakamani kwa ajili kusikiliza kesi zao hao walikuwa ni mahabusu wakati wafungwa wengine wakijianda kwenda mahakamni kwa ajili ya rufaa zao kwani waliamini wapewa adhabu ya kifungo kwa kuonewa.
Mimi nilikuwa na shauku ya kuonana na Rafiki yangu maana usiku ni mrefu sana, hivyo katika pitapita zangu katika viunga ndani ya Gereza nilikutana nae , Daaaaaa ilikuwa ni furaha kabla hatujazungumza lolote ikagonjwa kengele ya kupata uji . Basi nasi tulijongea na tukapanga fole na kupata vikombe vya uji wa Jera. Ndugu yangu Jera ni Jera, uji wa jera sio sawa na nyumbani lakini utafanyaje la muhimu ni “KUIKUBALI HALI”
Baada kupata uji tulikwenda sehem na tukaanza kupiga stori za kufarijiana kwamba , Chea hii habari imetanda nchi nzima, chea akaniambia ndio Sisi sio watu wakawaida ndio maana kila mtu anashangaa hawawezi kuamini kama sisi ndio tumekuwa na misimamo mikali namna hii ., Unajua karume Uoga ni dhambi ni lazima mtu uishi kwa kile unachokiamini na ukipiganie siku zote, Watu wa aina yetu ni wachache sana ndio maana waliowengi wanatuona sisi ni watu wa ajabu sana.
Kabla sijanza kutoa maoni yangu mtu mmoja akatufuata na kutuambia mnaitwa kule na Wazee, ndani jela neno wazee linamaana ni aAskar magereza.
Basi tukaelekea mpaka kwenye jengo la utawala ambako tulikutana askari magereza na askali polisi watatu. Wale askali polisi wakauliza hao vijana wako wap? Akajibiwa na askari magereza ndio hao hapo.
Yule afande alivua kofi hakuamini macho yake, maana alidhani angekuta watu wenye miili mikubwa,
Akasema “Yaan hivi vitoto ndio vinatupa shida sisi mkoa mzima unataharuki , embu waangalie walivyo wadogo kama njiti ya kibitriti, kwakweli lile neno niliona ni dharau kubwa sana, lakini sikuwa na lakufanya zaidi ya kumporomoshea Yule afande matusi ya nguvu kimoyomoyo maana laiti angeyasikia lingekuwa timbuli la Asha ngedele. Baada ya hapo akasema “ Haya bwana nyie nendeni sisi tulita kuwaona tuu, Rafiki yangu Chea akauliza” kwa hiyo lengo la kutuita ni kutuangalia tu” rafiki yangu namjua maana alianza kutabasamu kwa dharau nikajua huyu jamaa ataliamsha dude muda si mrefu basi nikamkatisha kwa kumwambia, Poapoa Afande asante kwa upendo wako.Nikamvuta mkono jamaa na kumuondoa pale,
Hatukupiga hata hatua kumi akatufuata mfungwa mmoja akatuambia “nyie jamaa mnaitwa na Yule Afande kule” huku amkimuonyeshea kidole , daaa kwan tunaitwa itwa hivi kwani tuna kipi cha ajabu? Nilimuuliza chea, chea akaniambia twende tukamsikilize sisi tuko chini yao, basi tukamfuata Yule afande na tulipofika karibu yake tukapiga magoti na kuitikia ndia bwana mkubwa kama ilivyo destuli ya Jera. Yule afande akasema simamane na mnifuate nasi tujka fanya hivyo,
Alitupeleka kwenye jengo mmoja ambalo tuliwakuta watu ambao wamevaa sare za tofauti na wafungwa wengine Yule afande akasema hawa watu wame kuwa na shauku kubwa ya kutaka kuwaona, mmoja wa wale jamaa akaanza kuwaita wengine waliokuwa vyumba vya ndani oyaaaa wale madogo tulio waona jana kwenye tv wamekuja humu ndani basi tukaanza kuona watu wakitoka kuja kutuangalia, huku wakiwa na vicheko vya furaha, hahahhahahahahahahah tulikuwa kama vinyago wa maonyesho. Basi wale jamaa wakatuuliza hizi sare mmewahi kuziona wapi, chea akasema hapana name pia nikawajibu hatujawazi kuziona popote. Basi Yule afande akaanza kutupo somo juu ya kule tulipo ingia
Akasema, “ hii ni sehem maalum wanayowekwa wafungwa walio hukumiwa kunyongwa,wafungwa hao hawachanganyiki na wale walio hukumiwa miaka na walio hukumiwa kifungo cha maisha, hawa wana kaa peke yao” afande akaweka kituo kasha akatuuliza “ mpaka hapo nani anaswali” mimi nikanyoosha mkono kwa kidoe , Yule afande akasema hapa hatuko shule kama unaswali wewe uliza tuu hata bila kunyoosha kidole, nami nikauliza “ je kila mtu anajua tarehe yake ya kunyongwa ?, afande akajibu hapana kwani Raais huyutangu aingingie madarakani hakusani kibali cha kumnyonga mfungwa yeyote Yule.
Wale wafungwa waliohukumiwa kunyongwa walikuwa na furaha kubwa sana mpaka nikashangaa maana nilitegemea watu kama hawa wawe wanahuzuni muda wote lakini ilikuwa tofauti sana.
Mfungwa mmoja akafunua sufulia moja ambalo kasha akachota mchuzi wa nyama na vipande kadhaa vya minofu akaweka kwenye bakuli kubwa kasha akaema karibuni hapa panaitwa “KONDEM” ninyi ni mahabusu tuu mnahuzunika, sisi wenzenu ni wahumuhumu tena mpaka kifo tena ni cha kunyongwa, kuweni na Amani hii ni hatua ambayo mwanaume kamili lazima apitie, alisema mfungwa mmoja. Kwa kweli yalikuwa ni maajabu makubwa, baada ya kumaliza supu Yule afande akasema ninyi mmepata bahati maana wafungwa wengine wanaingi Gerezani mpaka wanamaliza vifungo vyao hawajawahi kuingia huku lakini ninyi mmeingia. Hahahaha Eti ni fahari kuingia Jera jamaniiiiiii
ITAENDELEA………………………………………………………
 
JUMBA LA DHARAU -SEHEMU YA NNE

Watu walio hukumiwa kunyongwa ni wenye ushauri mzuri na wanabusara sana, nitofauti kabisa na simulizi zilizoko mitaani juu ya wafungwa mbalimbali. Tena leo nataka nikwambia jambo moja, maisha ya gerezani hayatofautiani saba na maisha ya Uraiani kitu pekee kunachotutofautisha ni UHURU. Wafungwa hawana uhuru kama tulionao sisi.huwezi kuaona thamani ya uhuru mpaka huo uhuru utakapo chukuliwa na mamlaka nyingine, ndipo utakapo udai kwa Gharama ya jasho na ikibidi Damu.
Baada ya kupiga michapo na na wafungwa wa KONDEM, tuliagana nao kwa kupeana mikono na kila mmoja kwani huwenda ikawa ndio mwisho wa sisi kuingi katika jengo lile tena katika historia ya maisha yetu labda kama tutahukumiwa kifo. Yule askari akatutoa mpaka nje ya lile jengo, kisha akasema , “MUWE WAANGALIFU VIJANA” ni kweli kabisa maisha ya Jera ni maisha yenye tahadhali kubwa sana kwa kila dakika inayo kufika.
Rafiki yangu Dickson maarufu kama CHEA akaniuliza twende tukapumzike wapi? Nikawaza nikamwambi twende kwenye kibanda cha TV tukaoshe macho. Tulipofika pale tuu. Akaja Askari mmoja akamuita Dickson na kuondoka nae. Nilipata mashaka kidogo hivyo iliniradhamu kuwaangalia muda wote bila kupepesa jicho langu pembeni. Wakafika karibu na maeneo ya utawala wakaa kwenye kingo za kuta ambazo kwa nyuma yake kumepandwa maua. Ni kama watu wanaofahamiana kwani nilimuona Dick akiongea nae kwa furaha bila kuwa na sura ya hofu na mashaka. Lakin bado haikutosha kuamini kwamba amani ilitawala pale walipo. Ilinibidi niondoke kwenye kibanda cha Tv na kutafuta pembe nzuri ambayo itanipa nafasi ya kuwaona bila kukingwa na mtu au kitu chochote ndipo nikaenda kukaa karibu na jengo la Zahanati ya wafungwa.
Pale nilikuwa nimekaa peke yangu lakini baada kama ya dakika kumi alikuja mtu aliyekuwa amevaa mavazi ya mfungwa lakini mtu Yule alikuwa wa tofauti sana na wafungwa wengine, Sare zake ilikuwa ni safi sana, kuanzi kofia, shati mpaka viatu na usoni alikuwa na amevaa miwani nadhani itakuwa ni ya macho, na mikono alikuwa na kamkoba wa nailoni juu umeandikwa my clear bag, ni mikoba maarufu sana uraiani.ndani ya mkoba ule kulikuwa na nyaraka mbalimbali pamoja na kalamu ya wino na kalamu ya risasi. Huyu mfungwa alikuja kukaa karibu na mimi, na akanisalimia kwa salamu hii,” we mhalifu haujambo “ nikamjibu sijambo lakini mimi sio mharifu, akaniangalia kisha akatabasamu akaniambia kila aliyeingia humu ndani ni mharifu wa makosa mbalimbali kama vile jinai, Mada, uhaini, na ufisadi, akaniuliza kesi yako ni jinai namba ngapi nikamtajia, akaniambia unakataa nini sasa wakati wewe ni mharifu wa kosa la jinai. Hapo niliishiia pozi. Nikamwambia haya bwana nimekusoma vizur
Pamoja nilikuwa na ongea nae lakini nilikuwa na muangalia kwa makini sana kwa sababu sikutaka kumuamini mtu yyote ndani ya jera ile.nilichokigundua kwake ni kwamba kwenye sare yake hakukuwa na namba ya kutoka gerezani kama kwenye sare za wafungwa wengine. Ikanibidi nimuulize “mbona sare yako haina namba ? Yule jamaa akaniangalia tena usoni kisha akanikazia macho na kuniambia “mimi natumikia kifungo cha maisha” hivyo sinto toka gerezani nikiwa hai labda nikiwa maiti, hata nikifa sintaishi uraiani bali nitaenda kuishi maisha mbinguni nako sijui peponi au motoni , akatabasamu tena , hapo nikapata shauku ya kutaka kujua kosa lililomfanya yeye kufungwa maisha hivyo nikamuuliza ulifanya kosa gani, akanijibu niliua watu wawili na hata leo wangekuwa hai ningewaua tena na hata kama siku yamwisho ya hukum mbele ya Mungu nitaonana nao basi Nitawaua kwa mara nyingine, huyu alikwa mfungwa wa ajabu sana ,nikamuuliza kwanini unasema hayo, akaniambia unajua bwana mdogo mimi nilipo maliza chuo kikuu nilikuwa ni wakili wa kujitegeamea , kuna mwanamke mmoja ambae nilikuwa nasoma nae pale chuo kikuu ya Dareslaam mimi nikiwa mwaka wa ne yeye alikuwa mwaka wa kwanza, Yule mwanamke alikuwa anaitwa Joice, nilitokea kumpenda sana, siku mmoja nikakutana nae katika viunga vya chuo, na nikamtongoza kwakweli hakunisumbua sana mwisho tukawa wapenzi baadae nikagundua Yule binti anatoka familia maskini sana hivyo nikajipa jukumu la kumuhudumia kwa kila kitu ikiwemo kumlipia ada ya chuo kwasababu wazazi wangu walikuwa na uwezo kidogo. Hata baada ya mimi kumaliza chuo tuliendea na mahusiano mpaka nikafunga nae pingu za maisha , lakini huwezi kuamini kwamba huyu mwanamke ndio chanzo cha mimi kuwa ndani ya JUMBA hili la DHARAU, Hadithi yake ilinivutia sana na kutaka kujua nni kiliendea,nikamuuliza sasa ikawaje akaniangalia tena kisha akatikisha kichwa ishara ya kusikitika akasema nilizaa na Joyce watoto wawili nilkuwa na furaha na amani, ndipo likanijia wazo la kwenda kuongeza elimu katia ngazi ya shahada ya uzamili chuo kikuu cha Dar eslaam. Ndoa yetu ilidumu kwa muda wa miaka tisa hivi nikawa najipanga kufanya sherehe ya kutimiza miaka kumi ya ndoa yetu ananisimulia Yule mfungwa anaetumikia kifungo cha maisha. Akaendelea.... siku moja nilikuwa natoka mahakamanikuwatetea wateja wangu waliokuwa na kesi mbalimbali, nilipofika nyumbani nikakuta nyumba ipo kimya sana, ambapo si kawaida, na kwa bahati nzuri au mbaya siku hiyo nilikuwa nimeacha gari yangu ofisini sijui ni kitu gani kilinifanya nitembee kwa mguu siku ile. Baada ya kukuta nyumba ipo kimya lakini milango iko wazi nikaingia hadi sebuleni sikukuta mtu nikaenda jikoni pia sikukuta mtu, nikapata wasiwasi maaa nilipo ona mlango wa chumba changu uko wazi kwani chumba changu kilikuwa karibu na jikoni. Basi ikabidi nijisogeze huku nikwa na hofu kwani leo nyumban pako kimya mno , nilipofika mlangoni nilianza kusikia miguno na kelele za mahaba ndipo nilipo ingia chumbani sikuamini macho yangu, nilimkuta Mke wangu akifanya mapenzi na rafiki yangu nilipata hasira sana , Yule jamaa alikuwa amemkunja mke wangu kama kifurushi cha maindi mabichi lakini kwa bahati mbaya hawakuniona maana walizama kwenye adimbwi kubwa la mahaba. Kwanza nikaufunga mlango taratibu bila wao kustuka kisha Nilikwenda kwenye droo la kabti langu, nilipovuta ile droo ndipo wakastuka kwamba ndani kuna mtu lakini tayari nilisha chukua BASTORA yangu kwakweli sikutaka kusikiliza maneno ya mtu ya mtu yeyote wote niliwapiga risasi na wote walikufa palepale mimi nikatoka na kwenda kujisalimisha kituo cha polisi. Baada ya hapo nikahukumiwa kifungo cha maisha. Daa niliumia sana kuona elimu ya Shahada ya Uzamili (Masters ) inatumikia kifungi cha maisha, hivyo ndivyo ilikuwa bwana mdogo , huku akitabasamu nikamuuliza kwa hiyo elimu yako haina kazi tena akasema hapana huwa naitumia nikiwa humu gerezani, huwa nawapa ushauri wa kisheria watu mahabusu na wafungwa walioko humu. Nimeandika rufaa nyingi nikiwa humu na zimewasaidia watu wengi na wengine wameshinda rufaa zao na kuniacha mimi gerezani. Akafungua mkoba wake na akanionyesha vyeti vyake kumbe muda wote anatembea na vyeti vyakekila utakapo muona gerezani.
Pia nae alitaka kujua vp kuhusu mmi kwa nn nimeletwa gerezani kama mahabusu, nikamuelezea kwa kirefu sana. Kwani mkuu wa chuo chenu ana elimu gani nikamjibu ni Profesa, Yule jamaa akasema hakuna profesa mwenye maaamuzi ya kijinga kama hayo., hapo ninyi watawapotezea muda hilo sio kosa la kimfunga mwanachuo kokote duniani hapo watawapotezea muda kisha watasema hawana maslahi na kesi. Dickson akaja nilipo nae akaketi jirani name pia nikamuliza Yule afande alikuwa anakwambia nini akasema Yule afande ni mtu wa Nyumbani bukoba alikuwa anataka nimpatie namba ya baba iliwafanye mpango tupae dhamana si unajua huku atuna ndugu. Hapo matumaini ya kutoka Gerezani yakaaza kuereje, sasa je tulifanikiwa kutoka Gerezana? Endelea kufuatilia simulizi hii ya JUMBA LA DHARAU

na
Rashid Karume
Njombe Imagination of Progressive Technology
S L P 1093
Njombe
0754913924
 
JUMBA LA DHARAU- SEHEMU YA TANO

Maisha ya jera yaliendelea ikwa usiku ikawa asubuhi ikawa siku ya pili, katika viunga vya jera watu waliendelea na pilika pilika zao waliokuwa wanakwenda mahakamani walikwenda, waliokuwa wanamepangiwa kufanya usafi walifanya. Basi ikawa ni pilika pilika na shughuli za kawaida.
Siku hiyo Diksoni aliniambia kwamba anajisikia Joto sana na anafikilia kwenda kuoga, ilikuwa majira ya s saa sita mchana nikamwambiwa we nenda kaoge bana hiko ni kipaji ambacho we mwanzangu umejaliwa mimi sina kipaji cha kuoga bali ninakipaji cha kula. Dickson akacheka Sana akaniambia ingekuwa mtu ananenepa kwa kula basi wewe ungekuwa mnene kama pipa. Pamoja na kupenda kula bado ni mwembamba kama mimi. Tena afadhali ningekuwa Kama wewe, unakumbuka Yule afande alituambia tuna miili midogo kama njiti ya kibiriti?Dick akasema” Tena umenikumbusha kwanini ulinikatisha pale nilitaka nimpemakavu Yule Afande”, nikamuuliza halafu mwisho wake ungekuwa nini, akanijibu “ tungeuona hapohapo” nikamwambia wakati mwingine inabidi tuepuke matatizo yasiyokuwa ya lazima. Nikamwambiwa nenda kaoge mimi utanikuta pale karibu na zahanati ya wafungwa ulinipo nikuta jana wakati unaongea na Yule afande wa kwenu, maana ni wahaya mnapenda ukabila sana, haaa wewe sio ukabila ule sisi watu wa bukoba huwa tunapendana sana tunasaidiana mno kuliko makabila yote hapa nchini. Alinijibu hivyo ,Nikamwambie haya nenda kaoge maana unataka kuanzisha mdahalo hapa, yeye akaelekea kwenye bafu za nje nilizoko ndani ya gereza. Mimi nikaenda kukaa pale karibu na Zahanati ya wafungwa nikipigwa na jua la saa sita mchana maana Jiji la Mbeya linabaridi kali hata saa sita bado baridi yake ni kama saa mbili asubuhi ukiwa kwetu Turiani. Pale niliwakuta watu wenge wengi wamekaa kwa kujipanga mstari , wengine walikuwa wanasoma magazeti wengine walikuwa wanasikiliza radio , mimi nilienda kukaa mbali kidogo ingwa masikio yangu hayakushinda njaa maana nilikuwa nasikia story mbalimbali zilizokuwa zikipigwa pale, kulikuwa na vijana wawili waliokuwa wamekaa umbali wa mita kama mbili kutoka nilipokuwa mimi mmoja wa alikuwa amevaa sare za wafungwa na na mwingine alikuwa amevaa nguo za kiraia , alikuwa amevaa suruali ya jinsi na T-sheti nyeusi , stori zao zilinifanya nivutike kuwasikiliza kwa hamu. Maskio yangu yalinasa maneno kadhaa waliyokuwa wanazungumza nikagundua hawa jamaa walikuwa wanatokea wilaya ya Mbozi. Yule jamaa alikuwa na guo za nyumbani kwa maana MAHABUSU, alikuwa anamueleza mwenzake sababu iliyofanya ashtakiwe, yeye alikuwa anashtakiwa kosa la ubakaji ambapo akipatikana na hatia hukummu yake ni MIaka 30 jela, Yule mfungwa , akamwambia mwenzake kwamba wala hasi isumbue mahakama ni bora akubali tu mapema ili afungwe na aje jela kama mfungwa ili apate kampani maana yuko peke yake. Daa nilishangaa kwa ule ushauri aliyetoa Yule mfungwa kwa mwenzake ambaye wanatoka sehemu moja . yaani mwenza akubali kufungwa kwa t miaka 30 kwa sababu tu ya kumpa kampani. Nikatupo jicho kwa yule mahabusu nikaona chozi linamdondoka kwa kweli hata ungekuwa wewe ungepata hasira kwa ushauri ule wa kijinga eti ukubali kufungwa kisha uje jela kwa lengo kampani jamaa yako.
Zilipita Kama Dakika ishirini hivi baada Chea alikuja alipokuwa ametoka kuoga na akaja pale nilipo kuwa nimekaa. Hapa sasa mwili uko poa sana maana naona mwili umekuwa mwepesi sana alisema chea nikamuuliza kwani mwanzo mwili ulikuwa mzito ulifungwa mawe au ? wakati tuko pale akaja jamaa mmoja na kipande cha gazeti ambacho kilikuwa na stori yetu. Akatuambia oyaaa stori yenu hii hapa, chea akachukua na akaanza kusoma kwa sauti nikamwambia soma kimya kimya mimi sitaki kusikia hizo habari za uzushi, mara tukasikia majina yetu yanaitwa na tukaenda eneo lile kumbe kulikuwa na watu waliokuja kutuona, basi kukaingia kwenye chumba cha mazungumzo kile chumba kilikuwa na dirisha lililotenganishwa na Nondo pamoja na wavu, hivyo ulikuwa unaweza kumuona unaeongea nae lakini hawezi hata kukupa mkona wa salamu, tulitaka kujua ni nani aliyekuja kutuona kumbe walikuwa ni WAJUMBE wanafunzi wetu, walikuwa na sura za huzuni na mashaka makubwa, neno la kwanza kulisikia toka kwao lilikuwa POLENI SANA WAJUMBE ,poleni sana washkaji, mdada mmoja aliyekuja kutuona aliniita kwa jina ...Karume pole sana ...., Jamani Dick ....pole sana sisi tunaumia sana, nikamuona yule dada ambae sitaki kumtaja jina lake kwa sababu mbalimbali alichukua kitambaa akawa anafuta machozi, kwa kweli sisi tulijua wenzetu watakuwa na huzuni sana hivyo tuliwafariji kwa kuwaonyesha sura ya furaha muda wote ili kuwapa matumaini wenzetu. basi tulipo maliza tukatoka kwenye kile chumba, kisha afande akasema msiondoke hawa jamaa zenu wamewaletea chakula, wajumbe walileta chakula kwenye Hotpot tatu mbili zikiwa zimjaa wali mwingi mno na hotpot jingine ilikuwa na vipande vya kuku, pia kulikuwa na bakuli la plastiki lilikuwa na samaki . Baada ya mmoja wa wale wajumbe kuonja chakula vyote mbele ya usimamizi wa askari magereza, ndipo sisi tukakabidhiwa yale ma hotpot ya chakula na tukaondoka pale. Kwakweli sura za wajumbe zilitupa mashaka juu ya Taharuki iliyoko nje ya kwa wajumbe nje ya Gereza. Lakini hatukuwa na namna.
Muda wa chakula ulipofika sisi hatukwenda kupanga foleni ya chakula kwa sababu tulikuwa tumeletewa chaku. Pia niwashukuru watu mbalimbali ambao walikuja kutuona na kutuletea chakula ziku zote tulizo kuwa tumekaa jela. Hakuna hata siku moja ambayo tuliyokosa chakula kwakweli
na kwa sababu ya chakula tuu tulipata marafiki wengi sana, maana thamani ya mtu aliyeko jela au mahahusu hata yule aliyeko kolokoloni kweye vituo vya polisi inajulikana kwa watu wanaokuja kumuona na kumletea chakula. Kama kuna ndugu yako au Rafiki yako yuko gerezani au kituo cha polisi nakusihi mpelekee chakula kizurikule aliko atapata heshima kwa kila mtu. Lakini kama watu hawaji kukuona, hawakuletei chakula inamaanisha wewe ndugu zako na jamaa zako wamekususa hivyo huna thamani yoyote kwa jamii.
Tuliendele kupata chakula cha mchana huku Dick akiwa na uhakika kwa muda si mrefu tutakuwa nje ya gereza kwa dhamana, tulikula chakula cha kwenye hotpot moja na nyamaa ya kuku. Baada ya kumaliza kula basi nikachuku lile hotpot na kwenda bombani kuosha kisha nikarudi tukaanza kugawana kile chakula kilicho baki kwa ajili ya jioni kwa sababu hatukai sero mmoja mimi nilikuwa sero namba Tisa na mwenzangu alikuwa sero namba kumi ambako alihamishiawa kutoka Sero namba nane.
Wakati tukijiandaa kuingie Sero yule askari ambaye wanatoka sehemu moja na Dikson alimuita kisha wakaenda kuongea kwa muda kama wa dakika tano baadae Chea alirudi kisha nikamuulize yule Nsomile mwenzako alikuwa anakambia nini? Akiwa na sura ya furaha iliyojaa matumaini akaniambia kwamba yule afande alikuwa anaongea na baba na sasa wanafanya mmpango wa kututo kwa dhamana hivyo wanashughulikia dhamana yetu huko nje. Hivyo inawezekana kesho tukatoka humu ndani, basi ilikuwa ni taarifa nzuri sana kwetu. Ilipo fika saa tisa kama na nusu hivi alasiri tukapata ujumbe wa kwenda kulala, hivyo tukabeba mahotpot yetu huku tukiwa na matumaini ya kwamba kesho tutakuwa nje ya Gereza.
Je kesho yake tulifanikiwa kutoka gerezani, fuatilia sehemu ya sita ya simulizi hii?
 
Back
Top Bottom