Jumapili iliyopita mke wangu ameniadhirisha mno kanisani

Mkulungwa01

JF-Expert Member
Jul 14, 2021
3,979
5,295
Nina muda mrefu sijaonekana jamvini, majukumu ni mengi sana. Kwa sasa mimi ni baba Gebbie, nastahili pongezi. Jumapili iliyopita baada ya ibada nilikuwa nasikiliza earphone.

Mke wangu alinifanyia hujuma, kati kati ya waumini wengine alichomoa waya kwa siri na hivyo kufanya wengine wasikie wimbo wangu. Nilikuwa nasikilza wimbo wa J Moe, 'pesa ya madafu', wote wa pembeni akiwemo mke wangu walikuwa wanacheka mno, baadaye nikagundua walikuwa wakinicheka.

Nimehisi kumchukia mpaka leo hii, na niliondoka muda ule ule. Amenibembeleza lakini wapiii! Nina hasira naye sana. Amenidhalilisha, ameishusha heshima yangu. Na hivi kulikuwa na watu wachache, je wangekuwa wengi?

Hovyo kabisa!
 
Nina muda mrefu sijaonekana jamvini, majukumu ni mengi sana. Kwa sasa mimi ni baba Gebbie, nastahili pongezi. Jumapili iliyopita baada ya ibada nilikuwa nasikiliza earphone.

Mke wangu alinifanyia hujuma, kati kati ya waumini wengine alichomoa waya kwa siri na hivyo kufanya wengine wasikie wimbo wangu. Nilikuwa nasikilza wimbo wa J Moe, 'pesa ya madafu', wote wa pembeni akiwemo mke wangu walikuwa wanacheka mno, baadaye nikagundua walikuwa wakinicheka.

Nimehisi kumchukia mpaka leo hii, na niliondoka muda ule ule. Amenibembeleza lakini wapiii! Nina hasira naye sana. Amenidhalilisha, ameishusha heshima yangu. Na hivi kulikuwa na watu wachache, je wangekuwa wengi? Hovyo kabisa!
Tunachojua hasira zako zitaishia kitandani basi 😂😂
 
Back
Top Bottom