Juma Nyoso anahitaji msaada wa kitaalamu haraka

Juma Nyoso anahitaji msaada wa kitaalamu haraka

nabbingo

Senior Member
Joined
Mar 2, 2015
Posts
101
Reaction score
47
Kitendo cha mchezaji Juma Nyoso kurudia matendo ya udhalilishaji kwa wachezaji wenzake ni kwamba kitaalum hiyo ni "ACTIVITY ADDICTION" Na hii ni hali ya mtu kupendelea kufanya au kutenda jambo fulani mara kwa mara kupita kiasi. Na haya ni Maradhi au Ugonjwa.

Kwa wataalum wa masuala ya MENTAL HEALTH (Psychiatrics) wanalifahamu hilo, Kama mtakumbuka mchezaji wa Barcelona Surez alikuwa na tabia ya kuwang'ata wachezaji wenzake kila wakitofautina mchezoni na unaweza kujiuliza kuwa anashindwa vipi kujizuia asifanye kitendo hicho bila kujali yuko wapi, akinanani wanamwangalia ukitilia maanani kuwa ni mtu maarufuna kumbuka maradhi hayaangalii hadhi ya mtu na suala lake si la kufungiwa au kupelekwa police kama Mhalifu bali anahitaji msaada wa haraka kutoka kwa Psychiatric, na hilo ndo lilifanyika kwa Surez na hivi sasa hajafanya tena tukio kama lile.

Pia si kwamba mtu anapona kabisa maradhi hayo bali kinachofanyika baada ya kufanya "one on one counseling" kuna program maalum anayotakiwa kufuata ikiwa ni pamoja na kufanya kitu kiitwacho "GROUP THERAPY" ikiwa pamoja na kupata "SPIRITUALLY EXPERIENCE" ili kuboresha mahusiano mazuri na Mungu manake haya yanaonyesha ni jinsi gani mahusiano yao na MUNGU (THE HIGHER POWER) yamekufa hasa Juma Nyoso.

Na hii haijalisha una dini au la cha msingi ni kwamba haya yote yanafanywa kwa muda wa siku 90 (miezi 3)mfululizo kwa vipindi na muda maalum, akiwa sehemu maalum "sober house au rehabilitation centre".
 
Kwani kafanya kosa gani? Nilisikia kitu kama aligombana na John Boko uwanjani. Lakini sidhani kama hicho ndio kosa lake.
 
Kafanya nini nyoso???

Kamwingiza kidole CHA kati mchezaji wa AZAM Fc, katikati ya makalio, kitendo kama hicho amewahi pia kunfanyia AMIR MAFTAH akiwa Yanga, Joseph Kaniki, Elias Maguli na sasa John Bocco
 
Bange inamfanya ashindwe kuheshimu ajira yake...
Atafulia sasa ivi...
 
Joseph Kaniki alipona kumuua huyu dogo! Alimshika ta.ko na 'golota' akageuka na cross moja ya kulia ikatua kwenye taya la nyoso....akazima.

Lakini hajifunzi!
 
Back
Top Bottom