Tunajua kuwa Mh Juma Duni Haji alihamia Chadema ili kukidhi matakwa ya kikatiba na kuwa mgombea mwenza wa Lowassa wakati wa harakati za mabadiliko. Baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na Lowassa kushindwa, katika matukio mengi yanayohusha viongozi wa Chadema huwa namuona Lowassa, Mbowe, Mbatia, Sumaye na kiasi fulani Kingunge ndo wanaonekana. Nijuavyo mimi, Lowassa hana dhamana yoyote ya uongozi pale Chadema kwa kuwa yeye alikuwa ni mpeperusha bendera tu na hata Juma Duni Haji ilikuwa ni vivyo hivyo. Nini kinaendelea kwa Mh Jma Duni Haji kutoonekana kwenye matukio yanayohusisha Viongozi wa Chadema? Au amesharejea CUF Kimyakimya? Au ni ile Kansa ya Ukanda ndani ya Chadema inasababisha asionekane? Nini hatma yake kwenye Chama hicho mzee huyu ambaye ni Kipenzi cha Wazanzibar wengi hasa wana CUF?. Kwa mwana JF yeyote mwenye ufahamu wa kinachoendelea naomba atujuze.