COMMENT YA MCHANGIAJI
Lakini na wewe Mtatiro kwenye msiba wa Wilson Kabwe,ulilaani kitendo cha mtoto wa marehemu kutompa mkono Paul Makonda,ukasema si uungwana,unakumbuka?
Nilikukosoa na nikakuambia, kwangu mimi yule dada ni shujaa kwakuwa hakuwa na chembe ya unafiki kwa kile alichofanyiwa marehemu wakati wa uhai wake.
Leo naona majibu umeyapata,watu wanafiki haina haja ya kuwaficha,ukweli utakuweka huru,hapo SEIF kaonesha wazi kwamba moyo wake haupo na wanafiki wa CCM waliomuweka mzee Jumbe kizuizini miaka yote 32,pia wanafiki wanaowakamata na kiwatesa wafuasi wa CUF Znz.
Huo ndio ukweli na unapaswa kuwa wazi,ukweli uliojificha ni unafiki.
JIBU LA JULIUS MTATIRO
↓↓↓↓↓↓
Kuna tofauti kubwa sana kati ya tukio la Makonda na Mtoto wa Kabwe na hili. Kifo cha Kabwe hakikusababishwa Makonda. Kitendo cha Makonda kueleza tuhuma za Kabwe hadharani kilikuwa ni wajibu. Unafananisha suala hilo na hili la Shein kupora ushindi wa Wazanzibari waziwazi na kwa kutumia mabavu mwaka jana? Makonda is innocent, Shein will never be innocent kwa dhambi ya mwaka jana. Sikuwa mnafiki brother.